SABABU ZA MAOMBI KUTOKUJIBIWA

Shalom wapendwa!
karibuni tujifunze sababu ambazo zimekuwa kikwazo katika kupokea majibu yetu kutoka kwa Mungu

SABABU ZA MAOMBI KUTOKUJIBIWA 

Na Nyandula Mwaijande

1) Kuomba kwa tamaa
Yakobo 4:3
Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.
1Wakorintho 10:31
Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.
Wakati mwingine unaomba maombi kwa ajili ya hisia ya tamaa uwe na uhakika hautapokea majibu ya maombi yako kutoka kwa Mungu. Ni lazima majibu ya maombi yako yawe kwa ajili ya utukufu wa Mungu na siyo kwa tamaa tu.
2) Roho zisizokuwa na msamaha
Mathayo 5:22-24
Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto. Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.
3) Kutunza sanamu ndani ya mioyo yetu
Ezekiel 8:5-18
5: Ndipo akaniambia, Mwanadamu, inua macho yako sasa, uangalie upande wa kaskazini. Basi nikainua macho yangu, nikaangalia upande wa kaskazini, na tazama, upande wa kaskazini wa mlango, ilikuwapo sanamu ile ya wivu, mahali pale pa kuingilia.
12: Kisha akaniambia, Mwanadamu, umeyaona wanayotenda wazee wa nyumba ya Israel gizani, kila mtu ndani ya vyumba vyake vya sanamu? Maana husema, BWANA hatuoni; BWANA ameiacha nchi hii.
18: Kwa sababu hiyo mimi nami nitatenda kwa ghadhabu; jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma, na wajapolia masikioni mwangu kwa sauti kuu, sitawasikiliza.
Ezekiel 14:1-4
3:Mwanadamu, watu hawa wametwaa vinyago vyao na kuvitia mioyoni mwao, nao wameweka kwazo la uovu wao mbele ya nyuso zao. Je! Ni laiki yangu niulizwe na wao katika neno lo lote?
Ukitunza sanamu na vinyago ndani ya moyo wako uwe na uhakika wa kutokujibiwa maombi yako. Sanamu na vinyago ni yale matendo uyatendayo ambayo hayampendezi Mungu, yaweza kuwa wivu, chuki, uongo, uzinzi, kiburi, masengenyo n.k.
4) Ukipingana/kupigana na watumishi wa Mungu uwe na uhakika utakapomwita Mungu hatakujibu
Zaburi 18:40-41
Naam, adui zangu umewafanya wanipe vizogo, Nao walionichukia nimewakatilia mbali. Walipiga yowe, lakini hakuna wa kuokoa, Walimwita BWANA lakini hakuwajibu.
5) Kuomba kwa mashaka/kutokuwa na imani ya kupokea majibu ya jambo unaloliombea
Yakobo 1:6-7
Ila na aombe kwa imani, pasipo na shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
Marko 11:23
Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.
6) Kutowahurumia maskini (wahitaji)
Mithali 21:13
Azibaye masikio yake asisikie kilio cha maskini, Yeye naye atalia, lakini hatasikiwa.
Ndugu zangu hizo ni baadhi tu ya sababu ambazo zinatufanya tushindwe kupokea majibu ya maombi yetu. Hivyo tujitahidi tutende yale yampendezayo Mungu na tuombe sawasawa na mapenzi yake ndipo tukimuomba Mungu atatujibu.

Mungu awabariki sana
By Nyandula Mwaijande.

Comments