SALAMU KWA DARASA LA SABA WANAOFANYA MITIHANI LEO NA EV. GASPER MADUMLA



Bwana Yesu asifiwe sana...
Nawapongeza wanafunzi wote wa darasa la saba walioanza mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi.
Nasema nawapongeza sana maana hiyo hatua waliyoifikia ya kumaliza elimu yao ya msingi ni hatua ya awali tena ni mojawapo ya hatua kubwa sana ya kumaliza elimu ya msingi na kuikaribisha elimu ya juu. Elimu ya msingi ni moja ya elimu kubwa sana kuliko vile watu wanavyojua. Sababu elimu ya msingi ndio inayotumika katika maofisi na taasisi zote za kiserikali na zisizo za kiserikali,hata katika mabenki.
Unaweza kuniuliza elimu ya msingi inatumikaje huko kote?
Jibu lake ni rahisi kabisa;
* Ukiwa unafanya kazi katika maofisini,kitu cha kwanza unachotakiwa kujua ni hesabu za kutoa,kujumlisha,kuzidisha na kugawanya,na mambo mengineyo ni ya ziada tu.

* Hesabu hizi hufundishwa katika elimu ya msingi.
Hata katika mabenki yetu,hesabu zao ni kutoa,kujumlisha,kugawanya na kuzidisha,hawana hesabu nyingine,yaani hawana hesabu za kuchora magrafu,au kutafuta pai,Au hesabu za kutafuta thamani ya x na y! Masomo mengine wayapatayo watu katika elimu za juu,ni masomo ya ziada,ambapo hata application za masomo hayo ya elimu ya juu hazipo kabisa katika maofisi yetu,au muda mwingine kuna-application kidogo sana.
Ni lazima ifike wakati wa kujua kwamba watoto wetu wanaofanya mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi hawakupangiwa kufeli
Kufeli mitihani ni mpango wa adui,bali Bwana anawatazamia mema siku zote.
Ukiona mtoto amefeli basi ujue yamkini maandalizi yake ya mtihani hayakuwa mazuri,pia adui shetani huchangia sana.

Wapo wanafunzi waliojiandaa vizuri sana kuifanya mitihani yote,ila ifikapo siku moja kabla ya kuingia katika chumba cha mitihani,wanafunzi wengi hujikuta wakipata hofu kubwa,wengine hujikuta wakianza kuumwa kwa gafla,wengine hujikuta wakisahau mambo yote waliojifunza awali. Hofu za namna hii hazikutoka kwa Mungu Baba yetu,bali zatoka kwa yule muovu.
• Na ndio maana nakuambia kufeli kwatoka kwa yule muovu.
Bwana Yesu asifiwe...
Mpango wa Mungu ni kuona wanafunzi wakifaulu katika viwango vya juu kwa ajili ya utukufu wake. Maana wasomi wanahitajika sana katika injili.
Watu wengi huzania kwamba watumishi wa Mungu hawana elimu,au huzani kwamba kumtumikia Bwana Mungu ni kufeli mambo yote kisha ndipo uanze kumtumikia Bwana Mungu.

Kwa taharifa yako;
Bwana Mungu anawahitaji watu wenye akili mno kuliko unavyofikilia. Bwana Mungu kamwe hamchukui mtu mwenye hasara.

Wale wote tunaowasoma katika maandiko matakatifu,walikuwa ni watu wenye faida,watu walioamua kuipiga hesabu kali kwa habari ya injili.
Labda tumtizame mtu mmoja aliyekuwa amejaa elimu;

• LUKA.
Luka alikuwa ni msomi,daktari mzuri. Biblia inamtambulisha kuwa Luka ni tabibu,tazama;

" Luka, yule tabibu mpendwa, na Dema, wanawasalimu. " Wakolosai 4:14
Na ikumbukwe kuwa,ni Luka ndio aliyeandika kitabu cha matendo ya mitume na wala sio Paulo aliyeandika kama wengine wadhaniavyo. Luka alimfuata Bwana Mungu,akiokoka katika mikutano ya Paulo,hivyo alikuwa mmoja wa wanafunzi wake Paulo. Ndio maana ukisoma nyalaka ya 1 Timotheo 5:23 tunamuona Paulo akimshauli Timotheo kitabibu kwa habari ya magonjwa ya tumbo yaliyokuwa yakimpata Timotheo,anamwambia;
" Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara. " 1 Timotheo 5:23
Ushauli huu alioutoa Paulo unatoka kwa Luka ambaye haswaa ndie mwenye fani ya kitabibu.Alikadhalika Paulo naye anasemekana alikuwa ni mmoja wa wanasheria ndio maana nyalaka zake ni ngumu mno. Pasipo kuongozwa na Roho mtakatifu,huwezi kuelewa nyaraka yoyote ile.

Wasomi wanahitajika kwenda kuifanya kazi ya Bwana Mungu kama akina Luka na wengine.
Watoto wa darasa la saba wanahitajika wafaulu sana tena sana,maana hawa ndio chanzo cha kuwa maprofesa wa baadaye watakaoishika nchi hii huku wakiwa na Yesu.
Na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla
Nami natumia fursa hii kuwapongeza hata wazazi wote waliowahimiza na kuwasimamia watoto wao kuisoma elimu hii ya awali,na hatimaye leo wameimaliza.
• Kwa huduma ya maombi na maombezi,nipigie;
0655-111149.

UBARIKIWE.

Comments