TOFAUTI YA KWELI NA HAKI

BWANA YESU asifiwe!
Je unapenda kuijua kweli?
 Je unapenda kuishuhudia kweli?
Je unapenda kuiishi kweli ya MUNGU?
Je unalitimiza agizo la BWANA YESU la kuwataka watumishi wake waende ulimwenguni mwote, wakaihubiri injili kwa kila kiumbe ili kila aaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele?(Mathayo 28:20)
somo hili litawafaa sana wanaotaka kuijua kweli ya MUNGU na wale ambao wanatamani kuwashuhudia watu wengine kuhusu hiyo kweli ya MUNGU.

Nikiwa nashuhudia siku moja Kuna Ndugu mmoja  Aliniambia  Kwamba Kama Nataka Kwenda Peponi Lazima Nihamie Dhehebu Lake. Nikamuuliza Dhehebu Gani Akasema Dini ya HAKI. Mimi Nikamwambia Kwamba Kama Atataka Uzima Wa Milele Anatakiwa aje Kwenye Dhehebu La KWELI yaani kwa YESU KRISTO maana YESU ni kweli na siku zote Ukweli ni mzuri kuliko haki. (Yohana 14:6-7 ''YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na KWELI, na uzima; mtu haji kwa BABA, ila kwa njia ya mimi. Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na BABA; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. ). 
Hapo juu neno linasema kwamba YESU KRISTO ni Kweli na ni uzima.
Pia hapo juu kuna  neno njia, Njia maana yake ni dini.
Dini ni njia ya mwanadamu kumelekea Muumba wake (Ayubu 4:6)
Kwa sababu Dini ni njia ya mwanadamu kumwelekea Muumba wake  basi njia sahihi au dini sahihi ni kumpata BWANA YESU ambaye yeye ni Njia(Dini) na Ukweli tena na uzima, na Haiwezekani mwanadamu kuingia uzima wa milele ila kwa njia(Dini) ambaye ni yeye. Na njia hii ya KRISTO sina maana ya kuwa Mkristo bali namaanisha kumshika KRISTO mwenyewe, Kumtii na kumcha MUNGU kwa yeye.

Kuna kweli na kuna haki.

Ndugu zangu Kuna Tofauti Ya HAKI Na KWELI. 
Mfungwa Ana HAKI Kabisa Ya Kula Chakula Lakini Bado Ni Mfungwa. Lakini Kweli Inakuweka Huru(Yohana 8:34-36 '' YESU akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote. Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli. ). 
YESU akikuweka huru unakuwa huru kweli kweli.
Unaweza ukawa na haki ya kufanya maombi na ukaomba kwa juhudi kubwa lakini MUNGU hakujibu kwa sababu huna kweli yake

KWELI Inakupa Kibali Cha Ajabu Sana(Yohana 1:12-13'' Bali wote waliompokea(YESU) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU) 

Na Ndani Ya KWELI Kuna HAKI Ya Ajabu Sana, sio dini ya haki bali   ni haki ya MUNGU dhidi ya nguvu za giza na mipango mibaya ya wanadamu.(Isaya 54:17 Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA , na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA. ). 
Hii ndio haki pekee ambayo tunatakiwa kuwa nayo, sio dini ya haki bali haki ya MUNGU na haki hii ya MUNGU tunaipata baada ya kumpokea BWANA YESU kama BWANA na MWOKOZI wa maisha yate. 
-Ndugu achana na dini ya haki ila mkimbilie BWANA YESU anayeokoa.
-Ndugu achana na dhehebu lako la haki ila mkimbilie BWANA YESU anayeokoa.
-Ndugu achana na kusema kwamba ''Nimefuata dini ya baba yangu'' bali mshike BWANA YESU anayeokoa. Kama utaamua kumfuata baba yako mzazi au walezi wako, je utayafuata maangapi kwao? maana kama baba yako ni mchawi, je utaufuata uchawi wake? Kama baba yako anafuga majini je na wewe ufuge majini kwa sababu tu ya dini ya baba? kama baba yako ni mzinzi na amezalisha wanawake 4, je umfuate baba yako na uzinzi wake? Hapana ndugu yangu nakuomba mfuate BWANA YESU anayeokoa. Maana Hakuna mwanadamu hata mmoja ambaye aliishi duniani bila kutenda dhambi ila YESU KRISTO pekee, ndio maana Biblia inatushauri kumfuaata YESU pekee.

Dini yangu mimi  Peter Ni YESU KRISTO(Matendo 4:12), 
Katiba Yangu Ni BIBLIA(Zaburi 119:105
Na  Kiongozi Wangu Ni ROHO MTAKATIFU(Wagalatia 5:18, 25 ''Lakini mkiongozwa na ROHO, hampo chini ya sheria.Tukiishi kwa ROHO, na tuenende kwa ROHO ). 


Ndugu Huyo ambaye nimezungumza habari zake hapo juu ambaye nilikuwa namshuhudia habari za kumpokea YESU Aliupenda Ukweli Niliomweleza Na Sasa yuko kwa YESU (2 Kor 5:17'' Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya KRISTO amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. ). 
-Ndugu usiache kuwashuhudia wanadamu habari za uzima wa milele ambao pekee unapatikana kwa YESU KRISTO.
-Wambie wana haki ya dini yao na wana haki ya madhehebu yao lakini hawana Haki ya MUNGU, Haki ya MUNGU ni KRISTO, Haki ya MUNGU ni kumpokea YESU KRISTO. 

Ndugu niliyemshuhudia, kwa sasa Amepata  Furaha Kubwa Sana Ndani ya YESU KRISTO aliye hai  (Warumi 8:1''Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika KRISTO YESU. ). 

 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.

                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292
             mabula1986@gmail.com
  MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
  MUNGU Akubariki.
WHAT JESUS CHRIST CAN DO, NO MAN CAN DO.

Comments