
Mmoja wa majeruhi waliookolewa kwenye kanisa hilo akiwa hajitambui.
LAGOS –
Idadi ya watu waliokufa kwenye ghorofa moja ambalo lilikuwa kwenye ujuenzi kwa ajili ya kulala wageni la makao makuu ya Kanisa la SCOAN
(Synagogue Church of All Nations) la Nabii TB Joshua wamefikia 50.
Jengo hilo
la ghorofa tano ambalo lipo makao makuu ya kanisa ni nyumba ya kulala
wageni na liliporomoka Jumamosi wakati ujenzi ukiendelea.
Hadi kufikia jana Jumapili jumla ya watu 41 walikuwa wameripotiwa kufa, lakini maiti nyingine tisa zimeongezeka leo hii.
Uokoaji bado unaendelea na watu wengine 124 walikuwa wameokolewa wakiwa hai hadi kufikia jana Jumapili.
Comments