Historia ya muziki katika maisha yake alianza akiwa
mtoto mdogo katika ibada za Sunday School,maisha yake yote alikua kanisani akiimba kwaya ya watoto na baadae kuamia kwaya ya vijana.Ukoo wake pamoja na baadhi ya ndugu kama Mashangazi,Baba zake wadogo ni waimbaji mpaka sasa hivyo walifanyika msaada hasa katika kukuza kipaji chake
Kwa sasa Anna Gideon Nyaupumbwe a.k.a Anna Boneka anatamba na kibao chake (Kama Si Wewe) kwenye Christian Radio,ni wimbo uliopo kwenye album yake yenye nyimbo 8 ikiwa imepewa Title ya MWALIMU MWEMA.Album yote imesimamiwa na Supar Produz PG kuanzia Vocal pamoja na mixing.
Ukiacha hilo Anna tayari ana album ya Video yake iliyo tayarishwa na Director wangu wa karibu Debro Gabriel Ngoy chini ya kampuni yake ya Eagle View.Anna yupo mbioni kuanda uzinduzi mkubwa katikati ya mwezi wa kumi na moja akiwa na matarajio ya watu mia nane....hatua za uzinduzi huo zimeshaanza ila kwa sasa jina la mgeni rasmi lipo kwenye () mabano.Ili kuweza kuwasiliana na Anna kwajili ya kujitolea kusupport huduma yake au kushiriki katika event hiyo soon,wasiliana naye kwa simu namba....0714-419047 au 0754-463563.




Director wangu wa karibu Debro Gabriel kikazi zaidi..

On Set Anna na Eagle View Location.

Hata wamasai walihusika katika video kuleta mnogesho mdau wangu.
.

Wakiwa kikazi zaidi mtu wangu

Kaa tayari soon na kuletea Audio za nyimbo zake mbili kutoka kwenye album yake.
Source: Uncle Jimmy
Comments