
Kama hiyo haitoshi,mwimbaji wa nyimbo za
Injili kutoka ndani ya jiji la Mwanza,anayetamba na Albam yake ya KUNA
NGUVU,Betty Lucas aliwabariki kwa nyimbo zake nzuri zenye mafundisho
mengi..
Akiongea na mtandao huu,mkazi mmoja wa
Bunda ambaye alihakikisha hakosi semina hiyo adhimu Bwana Nyang'ari
alisema"Muda mrefu nimekuwa nikitamani kumuona Betty Lucas,namshukuru
Mungu kwa kuwezesha ndoto yangu kutimia."
Aliendelea kusema kuwa katika waimbaji wanaomvutia hapa Tanzania Betty Lucas ni namba moja kwake.
"Napenda sana nyimbo zake,zinanitia moyo hasa ule unaoitwa kuna nguvu katika maombi,naupenda sana."
Hizi ni baadhi ya picha kutoka kwenye mkutano huo...
Picha zote kwa hisani ya Mwimbaji wa nyimbo za injili BETTY LUCAS
Comments