HAKUNA WOKOVU NJE NA YESU KRISTO.

Na Nyandula Mwaijande.
Nawasalimu katika Jina la Yesu Kristo! Bwana Yesu Asifiwe!
KARIBUNI TUTAFAKARI JUU YA UWEZO WA JINA LA YESU KRISTO!
i. Hakuna Wokovu katika mwingine
Matendo 4:12 - Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Mathayo 1:21 - Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.
Yohana 1:12-13 – Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.

Warumi 10:12-13 – Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye Yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.
ii. Ni amri kuliamini jina la Yesu Kristo - Sio ombi
1Yohana 3:23 – Na hii ndiyo amri yake, kwamba tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi, kama alivyotupa amri.
Yohana 3:18 – Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.

iii. Kuna uponyaji katika Jina la Yesu Kristo
Marko 16:17-18 – Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.
Yoeli 2:32 – Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la BWANA ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama BWANA alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao BWANA.

iv. Lolote ulifanyalo – lifanye katika Jina la Yesu Kristo
Wakolosai 3:17 – Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.

v. Kuomba na kupewa katika Jina la Yesu Kristo
Yohana 14:13-14, 26 – Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
Yohana 16:23-24 – Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.

vi. Jina la Yesu Kristo ni Jina lipitalo kila Jina
Wafilipi 2:9-11 – Kwa hiyo Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Mungu akubariki sana kwa baraka za Rohoni na Mwilini kwa kusoma na kutafakari ujumbe huu.
By Nyandula Mwaijande.

Comments