HELIKOPTA YA GWAJIMA IKO TAYARI KWA KAZI YA MUNGU.

Helikopta ya kanisa la ufufuo na uzima ambayo ipo tayari kwa ajili ya kuhubiria injili.
Kanisa la ufufuo na uzima ambalo linaongozwa na Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima limetoa taarifa kupitia page yao ya facebook kwamba Helikopta yao ambayo wameinunua miezi michache iliyopita kwa sasa iko tayari kwa ajili ya kazi ya MUNGU. 

Ndege hiyo ya kisasa ambayo Ufufuo na uzima kwa kushirikiana na watumishi wa MUNGU wa nchini Japan wamefanikisha ununuzi huo kwa lengo la kuhubiria injili. 

Ni jambo jema sana hili na hakika injili ya KRISTO lazima isonge mbele



Comments