![]() |
Nyimbo hizi haziburudishi bali zinahudumia roho ya msikilizaji na kumuinua kutoka hatua moja ya kiroho na kumpandisha ingine. Wanaoweza kulithibitisha hili ni wale waliosikiliza baadhi ya nyimbo hizo, E. R. Mwansasu mkongwe wa nyimbo za Injili analo neno juu ya nyimbo hizi, mwimbaji Wito William anaelewa kilichosheheni kwenye albamu hii. Alex Joseck, Mimi Mwanakijiji, Magdalena Anthony na wengine wengi watathibitisha hili.
Hakuna lugha tunayoweza kusema zaidi ya hii; kwamba kaa mkao wa utayari kupokea Baraka zako kupitia usikizaji wa nyimbo hizi.
Hongera sana Mch. Daniel na endelea kunyenyekea Mungu akupe nyimbo zenye mafunuo zaidi na zaidi kwa ajili ya kuzihudumia roho za wana wa Mungu.
Hongera sana Mch. Daniel na endelea kunyenyekea Mungu akupe nyimbo zenye mafunuo zaidi na zaidi kwa ajili ya kuzihudumia roho za wana wa Mungu.
Comments