IJUE MAMLAKA YA KUTUMIA JINA LA YESU ILI LIKUSAIDIE KATIKA SHIDA YAKO.


Bwana Yesu asifiwe!
Na Emmanuel Kamalamo.
Ni muhimu ujue jambo hili kwako wewe uliye mkristo, na uliyezaliwa mali pili kwa NENO LA MUNGU… (1 Petro 1:23 "Kwa kuwa mzaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele") Na kuzaliwa huko kumekuweka katika NAFASI iliyo kuu sana katika FALME na MAMLAKA katika ulimwengu wa Roho.
Kama Yesu yuko ndani yako inamaanisha umebeba NENO, maana NENO ni YESU KRISTO...Maandiko yanasema ("NAYE NENO ALIFANYIKA MWILI, AKAKAA KWETU; NASI TUKAUONA UTUKUFU WAKE, UTUKUFU KAMA WA MWANA PEKEE ATOKAYE KWA BABA; AMEJAA NEEMA NA KWELI" Yohana 1:14) na hilo neno ndilo linakuzaa mara ya pili. Ndiyo maana Yesu akamwambiaj Nikodemo Mkuu wa Wayahudi mtu asipozaliwa mara yapili [KWA MAJI NA KWA ROHO] hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Maji kama maji hayawezi kubadilisha maisha yako mpaka maji yapite kwenye NENO, lasivyo utaogeshwa majini na utatoka na utaendelea na dhambi kama kawaida. Paulo anasema,.. "KAMA KRISTO ALIVYO LIPENDA KANISA, AKAJITOA KWA AJILI YAKE; ILI MAKUSUDI ALITAKASE NA KULISAFISHA KWA MAJI KATIKA NENO" Waefeso 5:25-26.
Nakupa msingi wa kujua jinsi unavyofanyika ndani ya KRISTO YESU ili tunapoondelea mbele kama ulikuwa hujui kuomba uanze kuomba mwenyewe na kukemea MAPEPO, MAJINI na MAGONJWA yote wewe mwenyewe.
JINSI YA KUPATA MAMLAKA
YA KUTUMIA JINA LA YESU

LAZIMA UOKOKE.
Warumi 10:9 "Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
Kwa hiyo "KUOKOKA" ni kutoka katika "HATARI YA KIFO" iliyo katika ufalme wa giza, na unaingizwa katika "USALAMA'' uliyo katika ufalme wa nuru. Wakolosai 1:13"Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa mwana wa pendo lake".
Hivyo unapokuwa ndani ya UFALME HUU unakuwa chini ya MAMLAKA ya YESU KRISTO ili uweze kupewa MAMLAKA. Huwezi kuwa na mamlaka kama hauko chini ya mamlaka, mfano, huwezi kuwaambia wananchi wajenge choo cha shule kama hauko chini ya mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya inakupa mamala ili ukisema wananchi wakusikili, kama nakutania kajaribu kuwaambia wananchi wafagie barabara ujue watakwambi"UNATWAMBIA KAMA NANI? Lakini akisema Mwenyekiti wa mtaa hakuna atakaye bisha.

Nataka kusema nini? Yesu anapokuokoa anakupa MAMLAKA ya kulitumia Jina lake kwa sababu uko chini yake, lengo uweze kuwa na MAMLAKA YA YESU ili ushinde mamlaka ya giza. Waefeso 6:12"KWA MAANA KUSHINDANA KWETU SISI SI JUU YA DAMU NA NYAMA; BALI NI JUU YA FALME NA MAMLAKA" Ufalme huu wa shetani una WACHAWI, MAPEPO, MAJINI, MIZIMU, WAGANGA WA KIENYE nk.
Yesu anasema.."NIMEPE
WA MAMLAKA YOTE MBINGUNI NA DUNIANI". Mathayo 28:18
Maana yake nini? Ni ili aliyeokoka ukisema jambo dunia na mbinguni Yesu analikubari, ukisema"NAFUNGA ANGA LA ENEO LA NYUMBA YANGU WACHAWI WASIPITE KWA MAMLAKA YA JINA LA YESU" ooh!... Ujue mwenye MAMLAKA mbinguni na dunia Yesu Kristo atakubari KUFUNGA UKO MBINGUNI na matokeo ya KUFUNGIWA mbinguni kwa MAMLAKA yako uliyosema hapa duniani kwenye anga la mji wako hawatapita, kama uamini soma biblia yako maandiko yanasema....."YOYOTE MTAKAYO YAFUNGA DUNIANI YATAKUWA YAMEFUNGWA MBINGUNI; NA YOYOTE MATAKAYO MATAKAYO YAFUNGUA DUNIANI YATAKUWA YAMEFUNGULIWA MBINGUNI" Mathayo 18:18

Usifanye mchezo kuwafungia wachawi wasipite kwako kama huna Mamlaka ya Yesu Kristo ndani yako, maana wanakujua kabisa wewe ni mkristo tu wa jumapili ndoyo maana wengine wanalazwa nje bila wao kujua asubuhi wanajikuta wako nje, juu ya pati au porini na alikuwa amelala ndani.
Ili uweze kuwa kuwa dhibiti OKOKA leo.

Kesho tutaangalia eneo jingine ambalo aliwahusu tu MITUME, MANABII, WACHUNGAJI, WAINJILISTI NA WAALIMU.
MUNGU WANGU AKUBARIKI.
By Emmanuel Kamalamo

Comments