JE NABII ISSA(AS) NDIYE YESU KRISTO?

Mtume Peter Rashid Abubakar ambaye ndiye mwanzilishi wa huduma ya Glory to God Miracle Center(House of Prayer For All Nations) Tanzania jijini Dar es Salaam
BWANA YESU asifiwe.
Kuanzia leo tutakuwa tunakuletea  ujumbe huu ambao utawafungua maelfu ya watu.
Msimuliaji ni msomi na mtaalamu kabisa wa dini maana amewahi kuwa shehe na kusomea kila elimu ya dini ya kiislamu ila BWANA YESU akamukoa na sasa anatumika katika viwango vya juu sana, yaani kama unasumbuliwa na nguvu za giza kimbilia kanisani kwake mbezi  mwisho jijini Dar es salaam, mimi binafsi huwa ananibariki sana maana kama unasumbuliwa na mapepo yeye anayajua yote majina yao hivyo hata hasumbuki sana maana utasikia tu kwamba '' jini jabali toka kwa jina la YESU KRISTO, wewe shamsa toka kwa jina la YESU KRISTO'' na  mgonjwa anapona 
Karibu  na huu ndio ujumbe kutoka kwa Mtume Peter Rashid Abubakar

JE NABII ISSA(AS) NDIYE YESU KRISTO?

 Hebu fuatana naye...watu wengi (hususani waislam) huwa wanasema kuwa Nabii Issa aliyetajwa ndani ya Quran ndiye Yesu kristo, hata wanapokuwa wanaongelea jambo linalomhusu Yesu kristo hutoa maandiko yaliyomo ndani ya Quran na kumtaja Issa kana kwamba ndiye Yesu kristo. Hata wanapoupinga uungu wa Yesu huwa wananukuu maandiko yaliyo kwenye Quran ambayo yanamtaja nabii Issa. Hutumia andiko la ndani ya Quran Suratul Al-Nissaa 4:157(wanawake) inasema kwa ajili ya kusema kwao kuwa sisi tumemuua masihi Issa mwana wa mariam, hawakumuua wala hawakumsulubu walakini walibabaishiwa mtu mwingine.... Hivyo wanavyowachanganya Yesu na Issa wakidhani kuwa ni mtu mmoja!! Kwa maana hiyo haiwezekani katika Biblia, Yesu aseme imempasa kwenda Yerusalemu na kuuawa na siku ya tatu kufufuka Mathayo 16:21-23 na kauli ya Quran inapingana na maneno ya yesu. Sasa basi hebu tuangalie vipengere vifuatavyo:-

1. Majina na maana yake na asili yake, maana ya jina Issa na maana ya jina Yesu.
2.Kuumbwa kwa Issa na je Yesu kaumbwa?
3. Je manabii waliwatabiri?.
4.Nasaba(wazazi wao).
5. Kuzaliwa kwao.
6. Mamlaka.
7.Hukumu.
8. Kufa kwao.
9. Kurudi mara ya pili duniani.
10. Na kazi watakazokuja kufanya.
Sasa kama itaonekana mambo hayo yaliyotajwa hapo juu, wote wanayo ama wamehusika basi atakuwa mmoja na tofauti itakuwa majina kama wanavyodai au kusema. Neno tofauti kwa kiarabu nasema (THINAIN MUTAFARIKAN.) Sasa naanza kufafanua.


1. MAJINA(MAANA NA ASILI YAKE).
ISA-maana yake ni wekundu uliochanganyika na weupe(Albino au zeruzeru). Kwa hiyo Isa ni jina la kiarabu. Ushahidi huu hupatikana katika tafsiri ya Imamu Baidhawi vol; 1 ukurasa 160. (Idh Qafallah yaa-Issa Inniy mutawaffiyka warafi-uka ilayyakaa...) Kumbuka aliposema allah ewe Issa mimi nitakufisha na nitakuinua kwangu....Quran 3:55 ndivyo linavyosomeka jina la ndani ya kitabu cha Quran.
YESU-Jina la Yesu lilikuwa jina la kawaida la kiyahudi nalo linaonekana katika lugha ya kiyunani kwenye agano Jipya, likiwa sawa na jina la Yoshua la kiebrania katika agano la kale. Maana ya jina hili ni Yahweh(Yehova) ni mwokozi wetu hivyo lilifaa kuwa jina kwa yeye ambaye angeokoa watu wake, yaani watu wa Yahweh kutoka dhambi zao Mathayo 1:18-21.
Huu ni ushahidi.

ITAENDELEAAAAAAA......
USIKOSE. 

Watu wengi saana wafunguliwa  katika kanisa la
Glory to God Miracle Center(House of Prayer For All Nations). Mbezi Mwisho jijini Dar es salaam.

Comments