JINSI WAZAZI WAMECHANGIA UHARIBIFU WA MAANDALIZI YA WATOTO WA KIZAZI HIKI

Na Mchungaji Peter Mitimingi, mkurugenzi wa The Voice of Hope Ministries (VHM).

Wazazi Wanaoshiriki Kuwaibia Watoto Wao Mitihani Ili Wafaulu
Wazazi wanashiriki kuiba mitihani wanahonga ili watoto wao wafaulu mitihani yao vizuri. Mzazi anaenda kwa mwalimu na kumwambia unaona binti yangu sasa anaingia fomu four, anasema ngoja nikuonyeshe. Anahesabu hela na kumpa ili mwanae afaulu, chukua hii utakunywa soda si unajua mitihani ya siku hizi. Mzazi anaiba mitihani ili mtoto wake asipate shida, afaulu tu. Ndo mana kizazi hiki nakiita kizazi cha mdebwedo. Amekaa anangojea tu. Anamwambia mama shughulika, ashughulike nini, ongea basi na walimu ili mambo yawekwe sawa. Mtoto anataka apatiwe mitihani ili aweze kufaulu. Mzazi unanunua mitihani ili mtoto wako afaulu. Je huyu kafaulu au kaiba mitihani. Wakati itakapoanza kumgeukia sasa katika utekelezaji wa kazi na maisha, mtoto atamlaumu mzazi na kumchukia sana.Hivi mama alikuwa anawaza nini kuniibia mitihani angalia nilipofika sasa.
PATA NAKALA YA KITABU HIKI SASA UPONYE MAISHA YA WATOTO!
wasiliana na Mchungaji Peter Mitimingi kwa ajili ya kukipata kitabu hiki  kwa namba   0713 183939.

Comments