1. Mungu ana kazi na maisha yako bado na kama ana kazi na wewe, uwe na uhakika Mungu atayagharamia maisha yako katika maeneo yote… Lakini itatokea pale tu utakapojua kitu gani au jambo gani Mungu anataka ufanye kwa niaba yake na kuanza kulitenda
2. Mungu amekupa nafasi ya kuyagusa maisha ya weng
3. Mungu amekupa nafasi ya kuweka rekodi na alama ya
maisha yako hapa duniani… Rekodi au alama hiyo inaweza kuwa ya mema au
mabaya, uchaguzi ni wako, hata Mungu hawezi kuingilia
4.Mungu ameiondoa
jana, amekupa leo, Mungu anataka ujue kuwa haiangalii jana yako
kukutengenezea kesho yako njema. Hivyo jizoeze kuyasahau mabaya
yaliyopita, unaweza kuwa bora leo na kuandika historia mpya, unamkumbuka
Rahabu yule kahaba? Unamkumbuka Ruthu mkwe wa Naomi? Unamkumbuka
Yabezi? Wote hawa walikuwa na JANA/ HISTORIA MBAYA lakini walipoelewa
thamani ya LEO YAO kila kitu kikabadilika
5. Mungu anapokupa fursa ya
kuwa hai anataka ujue kuwa amekupa MTAJI WA KUPATATA YOTE UYATAKAYO hapa
duniani. Anataka ujue kuwa bila MAISHA/ UHAI yote uyatakayo
hautayapata… Anataka ujue kuwa ni BORA MARA MIA kuwa MBWA ALIYE HAI
kuliko kuwa SIMBA ALIYEKUFA!
6. Mungu anapokupa fursa ya kuwa hai,
anataka uutumie muda huo kujiandaa kwa ajili ya MAISHA YA MILELE, MAISHA
BAADA YA KIFO… Ndio maana Mungu anakupa nafasi kunisikia nikizisema
habari za Yesu, Msamaha wa dhambi, Uzima wa milele, Hukumu, Mbinguni na
Jehanamu nk.
Lakini UAMUZI NI WAKO… Ila uamuzi huo utakupa furaha au
kilio milele.
Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
Comments