KUITII SAUTI YA MUNGU

Na Mchungaji Yoshida kutoka Japani akihubiri katika madhabahu ya kanisa la Ufufuo na uzima , kawe.
Tunapomsifu Mungu, Mungu anatenda kazi, kupitia maombi Mungu atatenda kazi pia. Sisi wakristo tunatakiwa tuamini Mungu anatenda kazi sehemu yeyote bila kujali mazingira tuliyo nayo. Kwake Mungu hakuna kitu kisichowezekana na tunatakiwa kumwangalia Mungu aliye juu Mbinguni.
Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima na mchungaji Yoshida kutoka Japani

Sisi tunamwamini Mungu ambaye anatenda mambo yote, uraia wetu ni Mbinguni na ni lazima twende mbinguni. Kupitia maombi Mungu anatusikia, tunapata amani, tunakuwa pamoja na Mungu na tunatenda mapenzi yake. Kila wakati unapomuomba Mungu mlango unafunguliwa. Unaweza kupokea baraka nyingi ukisikia sauti ya Mungu na kuitii. Tunatakiwa tuitii sauti ya Mungu. kwa maana sauti ya Mungu inasikika. Mungu wetu ni Mungu  wa uponyaji, tukiwa na imani Mungu anatenda kazi.
Kwenye maisha yetu kuna matatizo mbalimbali na ili kuyakabili tunatakiwa tuombe na kwa uwezo wa Roho mtakatifu Mungu anatusaidia kupitia Roho mtakatifu kwa neno lake. Mungu anatenda kazi  kwa mbegu ya neno lake tunalo panda kwenye Roho zetu.

Mathayo17:26

26 Naye aliposema, Kwa wageni, Yesu alimwambia, Basi, kama ni hivyo, wana ni mahuru.

Tukitoa sadaka kwa moyo wote Mungu anakusaidia kulingana na haja ya moyo wako. Tukiomba kwa nguvu zetu zote Mungu anatenda kazi kwa maana baraka za Mungu hazina mipaka. Ni muhimu sana kuvunja mapenzi yetu binafsi na kufuata mapenzi ya Mungu. Kuna watu wengi wamefanikiwa kwa kuyafanya mapenzi ya Mungu. Mungu wetu ni Mungu wa ahadi,miujiza, Mungu anayetimiza ahadi zake ni Mungu wa Rohoni. Kuna ahadi Ishirini na saba(27) ambazo Mungu ametuahidi na kati ya hizo ahadi kila kitu tunachokihitaji kimo ndani ya hizo ahadi zake.

Kwenye kitabu cha mwanzo Mungu anasema iwe nuru na ikawa, maana yake Mungu anatupa mahitaji yetu kupitia neno laketunatakiwa kila wakati tuwe tunamwomba Mungu kwa kumaanisha kwa Roho na kweli. kwenye kitabu cha Yoeli Mungu amesema wakati unakujaatamimina Roho yake juu yetu na huo wakati ndio huu.
Yoeli 2: 28.
Ufufuo na Uzima,Tanganyika parkers Kawe
28 Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;

Comments