MADAM RUTI WA JANA IMEPITA AMEACHIA ALBAMU YAKE YA PILI YA "KESHO YAKO INAKUJA"


Tumeimba sana wimbo wa Jana Imepita kwenye majumba yetu, kwenye matamasha, kwenye maharusi, maofisini mwetu na sehemu mbalimbali. Tumebarikiwa sana na uimbaji wa Madam Ruti katika albamu yake ya Kwanza ya Jana Imepita. Kuna baadhi ya watu wameokoka waliposikia nyimbo za mwimbaji huyu, na wengine imani yao imeongezeka ukifafananisha na hapo zamani wakati hawajasikia nyimbo zake. Kuna waimbaji wengine wamediriki hata kuingia katika uwanja wa uimbaji kutokana na kuvutiwa na uimbaji wa mwana dada wa Yesu Kristo Madam Ruti.
Hakika uimbaji wake umeleta mafanikio makubwa sana kwa wakazi wa Tanzania na Afrika Mashariki. Jana Imepita umekuwa kama wimbo wa Taifa, kwani hata mtoto mdogo hasa wale wanaotoka katika familia ya Kikristo wanajua kuimba wimbo huu.
Madam Ruti wa Kesho Yako Inakuja
Lakini sasa ameamua kuachia albamu yake ya pili ya KESHO YAKE INAKUJA. Humo ndani kuna ujumbe mzuri sana kwako kujua kuwa kumbe kuna kesho yako inakuja hata kama jana yako ilishapita. Jana yako inaweza ikawa imepita bila ya mafanikio lakini tambua kuwa Kesho yako inakuja na unaweza kupata mafanikio yako ambayo hukuyapata jana.

Hili ni kava la albamu ya KESHO YAKO INAKUJA



Kava la Madam Ruti, Kesho Yako Inakuja

Comments