MAOMBI NI NINI?

Math 7:7 "Ombeni,nanyi mtapewa,tafuteni nanyi mtaona,bisheni nanyi mtafunguliwa"

1.Maombi ni kutafuta,kubisha hodi kwa Mungu.Luka 18:1 "Akawaambia mfano,ya kwamba imewapasa kumwomba MUNGU sikuzote wala wasikatetamaa" 

2.Maombi ni kumwendea MUNGU
Ebr 11:6b "Kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko,na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao"


3.Maombi ni kuzungumza na Mungu Isaya 1:18 "Haya njoni tusemezane,asema bwana wa majeshi,
Na John Moshy.

4.Maombi ni kuweka wazi haja/mahitaji yetu mbele za MUNGU ,filip 4:6 "Msijisumbue kwa Neno lolote,bali katika kila Neno kwa kusali na kuomba,pamoja na kushukuru haja zenu na zijulikane na Mungu"

5.Maombi ni Ibada mbele za MUNGU..MDO 13:2 "Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga,ROHO MTAKATIFU akasema,


6.Maombi ni kupigana vita vya kiroho,EFESO 6:18 "Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho,mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu"


7.Maombi ni kutulia na MUNGU Isaya 30:15 "kwa maana Bwana MUNGU asema hivi,kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa,nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kumtumaini lakini hamkukubali"


KWANINI YATUPASA KUOMBA?? MATH 7.7

1..Tunaomba ili tupewe haja zetu, "Ombeni nanyi mtapewa",Tena neno la MUNGU linasema wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi,Yakobo 4:2 "Mwatamani wala hamna kitu,mwaua na kuona wivu,wala hamwezi kupata,mwafanya vita na kupigana,wala hamna kitu kwa kuwa HAMWOMBI"


2.Ni agizo kutoka kwa YESU..Luka 18:1 "Akawaambia mfano,ya kwamba imewapasa kumwomba MUNGU siku zote,wala wasikate tamaa"
1THES 5:17 "Ombeni bila kukoma"


3.kwa sababu kuomba ni Huduma..huponya taifa,familia,kanisa na watu wanaponywa magonjwa na shida zao na kazi yake Jehova hufanikiwa
2NYAK 7:14 "Ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu,watajinyenyekesha,na kuomba na kunitafuta uso na kuziacha njia zao mbaya basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na kuiponya nchi yao"


4. Isaya 59:16 "Akaona ya kuwa hapana mtu,akastaajabu kwa kuwa hapana MWOMBEZI basi mkono wake mwenyewe ndio uliomletea wokovu na haki yake ndiyo iliyomsaidia"
Yak 5:14-16 "Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa nao wamwombee na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule na Bwana atamwinua hata ikiwa amefanya dhambi atasamehewa Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi,na kuombeana mpate kuponywa,kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana akiomba kwa bidii"


5..Kwa sababu ya kujenga mahusiano yetu karibu na Mungu
YAK 4:8 "Mkaribieni Mungu naye atawakaribia ninyi,itakaseni mikono yenu enyi wenye dhambi na kuisafisha mioyo yenu,enye wenye nia Mbili"


6..Kwa kuwa MUNGU ni Baba na sisi ni watoto wake,yatupasa kumwomba haki zetu tukiwa kama watoto..
MATH 6:9 "Basi ninyi salini hivi,Baba yetu uliye mbinguni,jina lako litukuzwe,ufalme wako uje"


Mungu akubariki,usikose kufwatana nami katika namna ya kuomba kwa mafanikio..

ubarikiwe
By John Moshy

Comments