MATOKEO YA IMANI HUTEGEMEA KIWANGO CHA NGUVU YA NENO LA MUNGU KILICHO NDANI YAKO

Na Emamuel Kamalamo.


Bwana Yesu asifiwe!
Msingi wa Neno letu ni Waefeso 3:20 "Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote yuyaombayo au tuyawazayo kwa kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu.
Wakristo wengi tunakwama katika eneo hili la IMANI ambalo ni chanzo au njia ya kupokea ahadi za Mungu.
Kwa sababu tunataka MATOKEO tunayotarajia lakini tunakwama kujenga kinachopitisha tunavyotarajia.

Utasema wapi tunakwama?...... Sikia, kwenye NENO LA MUNGU! kama huna Neno la Mungu huna IMANI. Maandiko yanasema… "Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo" Warumi 10:17.
Unapoambiwa.. "NENO LA KRISTO LIKAE KWA WINGI NDANI YENU" maana yake, ule wingi wa Neno ndani yako unakupa chanzo cha IMANI kitakacho pitisha ahadi za Mungu. Ndiyo maana huwezi kupokea mambo makubwa ambayo ni haki uyapate, sababu IMANI ni ndogo, kama ni ndogo basi kiwango chako cha kulisikia NENO LA MUNGU na kuliweka ndani yako ni kidogo kwa hiyo utapokea kwa kadri ya IMANI yako.
Ulishawahi kujiuliza kwa nini Yesu aliwauliza wale vipofu wawili waliotaka uponyaji kwake, aliwauli hivi ... "MNAAMINI KWAMBA NAWEZA KUFANYA HILI? Unajua walisemema nini? Waliseme.. "NAAM, BWANA" Yesu akaawaambia….. "KWA KADRI YA IMANI YENU MPATE" Mathayo 9:27-31. Sasa sikia, Yesu alitaka kujua ni KIWANGO gani walichonacho cha IMANI kilichotokana na KUSIKIA kwao juu ya Yesu anaponya, maana hawakusoma mahari popote bali "WALISIKIA" Na tumejua Imani chanzo chake ni kusikia.
Kilicho wapa kupokea uponyaji wa kufumbuliwa macho ni IMANI yao iliyojengwa katika kusikia, na wakaiweka katika matendo ya kumtafuta Yesu wapokee uponyaji.
Kwa mantiki hiyo IMANI ina kazi ya kupitisha au kupokea ulichokitarajia katika ahadi ya Mungu, kwa maana IMANI ni kama mfereji wa maji, ili maji yafike kwako lazima uunganishe bomba lije kwako ndipo utapata maji.

Tunaendelea…
MUNGU WANGU AKUBARIKI.
By Emmanuel Kamalamo.

Comments