NIkweli imetokea! Ni kwenye Kanisa la Paradise Internation 
Ministries lililoko Karakata Ukonga jijini Dar, mwanamke mmoja (pichani)
 anayedaiwa mchawi alidondoka usiku wa saa saba na kujikuta hawezi 
kutembea.
Tukio hilo lilijiri Septemba 13, mwaka huu wakati waumini wa kanisa hilo wakiwa wamezama kwenye maombi ya kufunga.
Ilidaiwa kuwa, waumini wa kanisa hilo wakiwa katika maombi 
hayo, Nabii Gideon Parapanda aliwahakikishia kuwa usiku huo kutatokea 
mambo ya ajabu kufuatia maombi hayo.
Inadaiwa ilipofika saa saba usiku mwanamke huyo akiwa na 
wenzake watatu, walidondokea kanisani hapo na kusababisha taharuki kwa 
waumini waliokuwa wakifanya maombi ndani. Mwanamke huyo alikuwa na 
kitambaa chekundu kikidaiwa ni hirizi, fimbo  nyeusi iliyozungushiwa 
shanga na alikuwa amejipaka masizi mwilini.
Akizungumza na Uwazi, Nabii Parapanda alisema watu hao 
walidondoka watatu, wawili walifanikiwa kukimbia akabaki huyo mmoja 
aliyejitambulishwa kwa jina moja la Aisha, mkazi wa Mwananyamala A 
jijini Dar.
Baada ya tukio hilo vyombo vya ulinzi, askari wa JWTZ na 
polisi walifika kwa lengo la kuhakikisha usalama wa eneo  hilo lakini 
nabii huyo aliomba mtu huyo asichukuliwe hadi atapofanyiwa maombi 
maalum.
Ombi la kiongozi huyo lilikubaliwa ambapo Aisha 
alipandishwa  madhabahuni na kukiri kuwa alikuwa na wenzake watano 
lakini katika kuanguka walikuwa watatu, wawili walifanikiwa kukimbia 
bila kusema walikuwa wakitoka wapi kwenda wapi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Mary Nzuki alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo alisema:
“Ni kweli tukio hilo limetokea na watu wameshuhudia, mwanamke huyo bado yuko kanisani hapo kwa maombi.”
“Ni kweli tukio hilo limetokea na watu wameshuhudia, mwanamke huyo bado yuko kanisani hapo kwa maombi.”
Comments