MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI ELIZABETH NGAIZA SASA KUSAMBAZA DVD YAKE YA "SEMA NAO BWANA" KATIKA GARI YAKE

Huu ni ubunifu wa kipekee sana, watu tunatakiwa kuiga mfano wa huyu mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania ambaye kwa sasa ameweza kununua gari lake kwaajili ya kusambazia kazi zake. Elizabeth ambaye anakuja kwa kasi sana katika kumuinua Mungu wetu kwa njia ya uimbaji, hivi sasa ameweza kutoa DVD yake mpya inayoitwa SEMA NAO BWANA, na katika albamu hiyo kuna baadhi ya nyimbo amewashirikisha waimbaji wakubwa sana Tanzania ambao ni Atosha Kissava na Ambwene Mwasongwe hasa katika wimbo wake wa AMELAANIWA.

Katika wimbo wa Amelaaniwa, utaweza kuona Atosha Kissava anavyoteseka na maisha akiwa na mwanae ambaye amezaa nje ya ndoa, anaingia katika shughuli za kuuza pombe bar, anakosa wateja wa kununua pombe na anajikuta maisha yanamwendea sivyo,  anaamua kumshauri mume wake ambaye ni Ambwene Mwasongwe kwenda kwa mganga ili wapate mali na utajiri. Mganga wakienyeji anawapa masharti ya kuleta mbuzi, na baadae wanajishtukia mtoto wao anapata ugonjwa wa akili na kuwa zezeta.

Maisha yao yanabadilika na kuwa maisha mazuri sana mpaka inafika kipindi wananunua hata gari, wakati mtoto wao amebaki kuwa zezeta kutokana na mganga kumharibu akili bila hata kuwajulisha wazazi wake. Baada ya kuona maisha ya kuishi bila kumjua Mungu sio mazuri hata kama wana fedha nyingi zinazotokana na matambiko na njia za kisheatani kutoka kwa mganga wao wa kienyeji, sasa wanaamua kuokoka na kumtumika Mungu.

Sasa huna haja ya kuhangaika kujipatia hii DVD kwani utaletewa mpaka mlango kwako, unachotaka kufanya ni kuchukua hiyo namba ya simu kwa mawasiliano zaidi. Ushauri wako waimbaji, umefika wakati wa kubalia na wabunifu wa kusambaza kazi zetu wenyewe ili tuweze kupata faida na tusitegemee kusambaziwa. Mungu ametupa akili na maarifa na tunapaswa kutumia. Leo hii Elizabeth Ngaiza amefikiria kutumia gari kama duka la kusambazia kazi zake, wewe waweza kuja na njia nyingine na ukawajulisha na wenzako ili waweze kutumia kusambaza kazi zao ili wanufaike na kazi yaoo wanayofanya kwa gharama kubwa.
MUNGU AKUMBARIKI SANA na MUUNGE MKONO ELIZABETH NGAIZA kwa kumunua DVD zake au kumualika kanisani kwako, katika mikutano na makongamano, sherehe na sehemu mbalimbali ili aje amtukuze Mungu na watu waweze kuokoka kwa kupitia huduma yake ya uimbaji.

Design and Branding by
RUMAFRICA FOR ALL NATIONS
+255 715 851 523.

Comments