ROSE MUHANDO KUSHIRIKISHWA KWENYE KOLABO NA HUYU MUIMBAJI WA KENYA.

Gospel Star Rose Muhando malikia wa muziki wa injili Tanzania  wiki tatu zilizopita alikua nchini Kenya kihuduma ambapo alipata wasaha mzuri kukutana na baadhi ya waimbaji nchini Kenya.
Moja kati ya muimbaji ambaye ni rafiki yake kwa muda
Maryanne Tutuma alipata bahati ya kufanya kolabo na Rose.
Maryanne na Rose Muhando. 

Maryanne ni muimbaji anayefanya vizuri kenya tofauti na hapa nyumbani Tanzania,ni muimbaji aliyepata airtime nzuri kwenye vituo vya kidini Kenya.Ukiacha hilo Maryanne Tutuma ana ufahamu vizuri muziki wa injili wa Tanzania hivyo kupitia Rose Muhando anaamini kolabo hilo litakua la kuotea mbali alisikika akisema Maryanne.
 Maryanne amekua akifanya nyimbo nyingi za kikabila ila kwa sasa wamefanya kolabo na Rose ikiwa katika lugha ya kiswahili.
 
endelea kufuatiliaa.

Comments