USIWE MWEPESI WA KUTOATOA SADAKA KWA KILA MADHABAHU, MADHABAHU ZINGINE NI MADHABAHU ZA SHETANI.

""Ujihadhari usitoe sadaka zako za kutekezwa katika kila mahali upaonapo"" KUMBUKUMBU LA TORATI 12:13.
Ewe mtu wa Mungu uliye na shauku ya kutaka kuona Mungu akikukumbuka na kujishughurisha na mambo yako kupitia sadaka zako ninaomba ulielewe hili.

Na  Godfrey Miyonjo.
Ni kweli kabisa kuwa baraka zote za Mugu, zile za mwilini na zile za rohoni hupatikana kupitia utoaji,
Ninakubali kuwa sadaka ndiyo hazina pekee ambayo mtu akijiwekea haiwezi kuharibiwa na nondo wala kutu, tena wevi {wezi} hawawezi kuvunja na kuiba.

Hakika sitaweza kusimama na kupinga juu ya utoaji wa sadaka.
Tusiache kutoa sadaka kila iitwapo leo, tena tutoe sana, kwani imeandikwa "apandaye haba atavuna haba,".

Ila Katika kutoa kwetu inatupasa tujiulize, je! hapo tunapotoa ndipo mahala ambapo BWANA ametuamuru tuwe tunatoa sadaka?
Kama Mungu alivyotukataza kuwa tusiwaendee wenye pepo {waganga wa jadi} na kutoa sadaka huko, ndivyo alivyotukataza kwa habari ya kutoatoa sadaka kila mahali.

Katika dunia hii siyo kila madhabahu iliyojengwa na kulitaja jina la Mungu ni madhabahu ya Mungu, hata shetani naye anaitwa "mungu wa dunia hii".

Zipo madhabahu nyingi tu za shetani ambazo zimesimama kwa jina la Mungu, ukitaka kuzijua zipime kwa neno la Mungu. 

Kwahiyo unapotoa sadaka katika madhabahu yoyote ile ujue kuwa wewe una ushirika na madhabahu hiyo, yaana madhabahu hiyo ina uweza wa kutamka laana au Baraka juu yako, ina uweza wa kufunga au kufungua mambo yako.

Sadaka inapotolewa mahala popote pale, iwe kwa nabii wa uongo, iwe kwa mganga wa jadi, iwe ni kwa makaburi au ni kwa Mungu, sadaka hiyo huendelea kubaki kama ukumbusho na kuendelea kunena.

Musa alilijua hilo ndiyomaana aliwaonya wana wa Israel kutoatoa sadaka kila mahali{kutoa hovyohovyo}.
Aliona wakifanya hivyo itafika mahali watamkosea Mungu kupitia matoleo/sadaka.

Nami ninakuambia kuwa, siku hizi kumekuwepo na manabii wengi sana, tena wengi wao mafundisho yao makubwa ni "kutoa na kubarikiwa".

Kama ulikuwa hujui, tambua sasa kuwa Sehemu kubwa ya hao manabii ni manabii wa uongo.

Hivyo ninakuambia ujiadhari kutoa sadaka kwao, hata kama umeahidiwa muujiza mkubwa kiasi gaini, ni vyema kabla ya kutoa hiyo sadaka yako umwulize Roho Mtakatifu, akueleze kama hapo unapotaka kutoa sadaka ni mahala ashihi ama siyo sahihi?
Kama Roho Mtakatifu akikuruhusu na utoe, na asipokuruhusu usitoe.

Kwani ukitoa sadaka kwa madhabahu ya shetani, wewe moja kwa moja ni mwana wa jehanam, kama usipotubu.
Na ni mbaya sana mtu kutenda dhambi pasipo kujua, kwani hujihesabia haki, hujiona yuko sawa na kushindwa kuiendea toba.
Biblia inasema dhambi ya mtu itakuwa juu ya kichwa cha mtu huyo aliyeitenda, iwe ametenda kwa kujua au kwa kutokujua, katika hili usifirie kama kutakuwa na kujitetea.

Pia ninakushauri, usiwe ni mtu mwenye kutangatanga kwa kutafuta/kufuata miujiza, acha miujiza ikufuate.

KWA MAANA UKWELI NI KWAMBA, MUUJIZA MKUBWA KULIKO MIUJIZA YOTE NI KUMWAMINI YESU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO {KUOKOKA}.
""asomaye na afahamu""
MUNGU akubariki sana.
By Godfrey Miyonjo.

Comments