WENYE WOKOVU TU NDIO WATAKAOUPATA UZIMA WA MILELE.


 

BWANA YESU asifiwe ndugu yangu.

Karibu tujifunze habari za uzima, habari za wokovu mkuu.

Wokovu ni maana yake ni kuishi maisha ya ushindi dhidi ya dhambi.

Wokovu ni kukombolewa kutoka kwenye hali mbaya na kuingia kwenye hali nzuri. BWANA anasema katika Isaya 51:6-7 ‘’ Inueni macho yenu mbinguni, mkaitazame nchi chini; maana mbingu zitatoweka kama moshi, na nchi itachakaa kama vazi, nao wakaao ndani yake watakufa kadhalika; bali WOKOVU wangu utakuwa wa milele, na haki yangu haitatanguka. Nisikilizeni, ninyi mjuao haki, watu ambao mioyoni mwenu mna sheria yangu; msiogope matukano ya watu, wala msifadhaike kwa sababu ya dhihaka zao. Maana nondo itawala kama vazi, na funza atawala kama sufu; bali haki yangu itakuwa ya milele, na WOKOVU wangu hata vizazi vyote.  ‘’

Wokovu ni ukombozi.

Wokovu ni muhimu sana kwa kila mwanadamu.

Wasio na wokovu wataangamia milele lakini waliokombolewa na kukubali kuishi maisha ya wokovu watapona na kuingia katika raha ya milele.

Watakatifu wote siku ya mwisho watakubali kwamba wokovu una MUNGU kupitia YESU KRISTO pekee Ufunuo 7: 9-10 {Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao; wakilia kwa sauti kuu wakisema, WOKOVU una MUNGU wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo.  }

Wokovu unapatikana sasa.

Wokovu ni zaidi ya huduma yako.

Wokovu ni zaidi ya kipaji chako.

-Wokovu sio kuwa Askofu wala mzee wa kanisa .

-Wokovu sio kuwa mchungaji wala shemasi.

-Wokovu sio kuwa umesoma sana Biblia.

-Wokovu sio kwenda kusali tu.

-Wokovu sio kuwa tajiri.

-Wokovu ni kumpokea BWANA YESU.

-Wokovu ni kuliishi neno la MUNGU.

-Wokovu ni kuishi katika neno la MUNGU.

-Wokovu ni kutenda mema ambapo ni kumshika BWANA YESU.

Wokovu ni muhimu sana.

Maisha ya wokovu ni maisha ya mtu aliyeokoka.

Wokovu haupatikani kwengine ila kwa BWANA YESU. Matendo 4:12 (Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.)

Ndugu kama unataka wokovu lazima umpe YESU maisha yako na uliishi neno lake.

Wengine hudanganywa na kuambiwa kwamba kuna wokovu mwingine kupitia wengine. Ndugu zangu hakuna wokovu au ukombozi kwingine kokote ila kwa YESU KRISTO.

Kama unataka uzima wa mielle lazima umhitaji BWANA YESU maana hakuna wokovu kwingine.

Na kama umeokoka harafu kwa sasa umeanza kuuchoka wokovu basi tambua kwamba, ukianza kuuchoka wokovu basi hakika umeanza kuuchoka uzima wa milele. Na kama umeanza kumchoka BWANA YESU basi hakika jehanamu inakuita maana hakuna wokovu kwingine kokote.

Ndugu yangu hakikisha BWANA YESU ni Nuru yako na Wokovu wako(Zaburi 27:1-4 ‘’ BWANA ni nuru yangu na WOKOVU wangu, Nimwogope nani? BWANA ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?  Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka.  Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumaini.  Neno Moja nimelitaka kwa BWANA, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa BWANA Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa BWANA, Na kutafakari hekaluni mwake.)

Tena ndugu yangu  hakikisha unaipokea chapeo ya wokovu ( Waefeso 6:17”T ena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa ROHO  ambao ni neno la MUNGU;  ‘’
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                     MUNGU akubariki sana .
                      Ni mimi ndugu yako
                       Peter M Mabula
                 Maisha ya Ushindi Ministry.
                           0714252292
 

              mabula1986@gmail.com
  MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
  MUNGU Akubariki.

Comments