BWANA YESU ATAKUJA TENA DUNIANI KWA JINSI GANI?


BWANA YESU asifiwe.
Karibu tujifunze ujumbe wa kurudi kwa KWANA YESU na jukumu letu la leo kama wanadamu wanaotamani kuingia uzima wa milele.

Katika Luka 9:23-25 Biblia inasema, “Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha. Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza, au kujipoteza mwenyewe?''
 Dini Ni Mpango Wa Mwanadamu Kumtafuta Mungu, Na WOKOVU Ni Mpango Wa MUNGU Kumtafuta Mwanadamu. Hivyo jambo kubwa na la maana kabisa ambalo mwanadamu yeyote duniani anatakiwa kulifuata ni WOKOVU.
Wokovu ni kumpokea BWANA YESU.
 1 Yohana 1:7  "tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake YESU, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote."

Kama Mashariki Na Magharibi Zilivyo Mbali Ndivyo MUNGU Atakavyoziweka Dhambi Zako Kama Tu Ukiamua Kumpokea YESU Kama BWANA Na MWOKOZI Na Ukaanza Kuukulia Wokovu Kwa Kujifunza Neno La MUNGU Katika Kanisa La Kiroho Wanaokemea Dhambi Hadhalani.

 Ana Heri Mtu 1 Anayeokoka Na Kuacha Dhambi Kuliko Watu 99 Ambao Hawana Haja Ya Kutubu.
 Kila Mwanadamu Anamhitaji YESU Kwa Ajili Ya Uzima Wa Milele, Kama Humhitaji Leo Basi Utamhitaji Siku Ukielekea Jehanamu Ila Utakua Umechelewa. Neno La MUNGU Halipitagi bure Bali Linapita Ili Likupe Ufahamu, Ujitambue Na Ili Uamue Kuupokea Uzima.
  Luka 15:7 ''Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu.''

 Safari 1 Huanzisha Nyingine, Safari Ya Kwenda Kufanya Dhambi Za Uzinzi, Uchawi, Ujambazi au dhambi yeyote ile Inaweza Kabisa Kwako Ikaanzisha Safari Nyingine Ya Kwenda Jehanamu. Ndugu Ogopa Dhambi, Ikemee Dhambi, Ichukie Dhambi, Ikimbie Dhambi Na Usitende Dhambi. BWANA YESU Anakupenda Sana Na Yuko Tayari Kukubadilishia Mwenendo Wako Mbaya Kama Tu Ukimpokea Leo.

MUNGU Mwenyezi anatutarajia sisi wanadamu wote kufanya yafuatayo ili tuwe na tiketi ya uzima wa milele na ili tutimize jukumu letu la duniani.


WAJIBU WETU KWA MUNGU.

(1) Tutubu Dhambi Zetu Kwa YESU KRISTO Ili Tusamehewe{1 Yohana 1:9, Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. }.
(2) Tumwamini YESU KRISTO Ili Tuokolewe{ Matendo 16:31,Wakamwambia, Mwamini BWANA YESU, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. }.
(3) Tumpende MUNGU Wetu Kwa Roho Zetu Na Kwa Mawazo Yetu Yote{ Mathayo 22:37, Akamwambia, Mpende BWANA Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. }.
(4) Ni Lazima Tumkiri YESU KRISTO Mbele Ya Watu Wote{Mathayo 10:32-33, Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za BABA yangu aliye mbinguni. Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za BABA yangu aliye mbinguni. }.
(5) Tuishi Maisha Ya Kmpendeza MUNGU{1 Thesalonike 4:1, Iliyobaki, ndugu, tunakusihini na kuwaonya kwamba mwenende katika BWANAYESU; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza MUNGU, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana. }.

 Wenye Haki Wataingia Mbinguni, Wenye Dhambi Wataingia Motoni. YESU KRISTO Anauwezo Wa Kuwafanya Wenye Dhambi Wasiende Motoni Bali Waende Mbinguni Kama Tu Wakiamua Kumpokea Leo Kama BWANA Na MWOKOZI Wa Maisha Yako, Kisha Wakashika Utakatifu Na Neno Lake.

BWANA YESU ATAKUJA KWA NJIA GANI?

1. Kuja kwake kutakuwa kwa ghafla, Mathayo 24:27  ''Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. ''

2.Atakuja juu ya mawingu angani mwenye nguvu na utukufu mwingi sana, Mathayo 24:30-31 '' ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu. ''

3. Siku akija kila Jicho litamuona, Ufunuo 1:7 ''Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina. ''
4.Parapanda kuu italia siku hiyo , 1 Thesalonike 4:16-17 '' Kwa sababu BWANA mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya MUNGU; nao waliokufa katika KRISTO watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki BWANA hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na BWANA milele. ''
5. Atakuja huku watu wakimuona , Matendo 1:11 '' wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu YESU aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni. ''

Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani.
ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana
Ni mimi ndugu yako katika BWANA YESU.
Peter M Mabula
0714252292
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments