Dr.Myles Munroe na mke wake wafariki katika Ajali ya Ndege.

 

mwalimu wa Neno la Mungu,(Myles Munroe), mkewe (Ruth Munroe) na binti yao (Charisa Munroe), Enzi za uhai wao.
Taarifa ambazo zimeifikia Blog hii zinasema kwamba Mchungaji Kiongozi wa Huduma ya Bahama Faith Ministries Dr.Myles Munroe na mkewe Bi.Ruth wamefariki katika ajali ya ndege iliyotokea huko Grand Bahama.

The passengers preparing to board the ill-fated flight.
Ajali hiyo imetajwa kutokea siku ya Jumapili mchana na kupoteza maisha ya abiria wote Tisa (9) waliokuwemo katika ndege hiyo ndogo ya Binafsi.
 
Taarifa zinafafanua zaidi kua ndege hiyo ya binafsi iliondokaLynden Pindling International Airport (LPIA)  Nassau, Bahamas  ikiwa na abiria tisa (9) majira ya saa 10 na dakika 7, na baadae kupata ajali wakati ikijaribu kutua katika uwanja wa ndege wa Grand Bahama International Airpot majira ya saa kumia na moja na dakika 7,
 
Aida imeelezwa kua abiria wote hao waliku wakielekea katika Mkutano ambao ulikua umeandaliwa na Mchungaji Dr.Myles Munroe

Uchunguzi zaidi unafanyika leo ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.
 taarifa zaidi nitakuletea kadri zitakapopatikana
 

Itakumbukwa kua Mchungaji Dr.Myless Munroe na mkewe ni moja ya wahubiri na waalimu wanapendwa sana barani Afrika na Duniani ambapo,mwezi uliopita wa October2014, Dr. Munroe na mkewe walikuwepo hapa Dar es Salaam kwa semina maalum ambayo ilishirikisha Wajasiriamali,wachungaji mbalimbali  pamoja na Viongozi.na baadae akaelekea Kenya kushiriki katika Mkesha mkubwa wa AFLEWO ambapo alipata nafasi ya kuhubiri katika mkesha huo ujumbe uliowagusa watu wengi sana.
Hapa ni Mchungaji Dr.Myles Munroe akisalimiana na Dr.Ghalib Bilal Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,siku Mwalimu wa Neno la Mungu,(Myles Munroe), mkewe (Ruth Munroe) na binti yao (Charisa Munroe), walitwaliwa kwa pamoja katika ajali ya ndege yao. Na hata sasa, katika maandiko na machapisho yake, japo amelala mauti, tunajifunza na kujegwa. Mungu aliyempa mtumishi wake Myles Munroe vipawa vya kufundisha na kuandika, atukuzwe milele na mileel Amen.

Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi (YN 9:4 SUV).

Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao. (UFU. 14:13 SUV).

Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida. (FLP. 1:21 SUV).

Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake. (2 TIM. 4:6-8 SUV).

Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo? (YN. 11:25-26 SUV).

Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo. (1 THE. 4:13-18 SUV).

BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe (AYU. 1:21b)
alipokuwepo nchini Tanzania,jijini Dar es Salaam
 

Comments