EDSON MWASABWITE KUZINDUA ALBAMU YAKE YA "MUNGU AMENIHURUMIA 100%" NDANI YA KANISA LA KKKT SINZA KUMEKUCHA
![]() |
Edson Mwasabwite, Mwimbaji nyota ya mziki wa injili. |
Edson Mwasabwite ni mwimbaji wa nyimbo za Injili akitokea Tanzania, nyimbo zake zimekuwa zikipigwa kila sehemu na hasa katika sherehe za maharusi, kitcheni Party, makanisani, mitaani, kwenye vyombo vya usafiri, maredioni, luninngani n.k. Mungu amempa neema ya pekee mwimbaji huyu kwa kukubalika na jamii ya Kitanzania na nje ya Tanzania kwa ukarimu wake na upole wake.
Mwimbaji Edson Mwasabwite ni yatima (hana baba wala mama) ameishi katika maisha ya uyatima tangia akiwa mdogo sana, na ndio maana leo hii amefika hapa ni kwa neema ya Mungu.
Ndugu zake na marafiki zake wamekuwa watu wake wa karibu sana kumtia moyo na kumfariji pale alipokuwa akipitia magumu na majaribu. Watu wengi sana wamepokea miujiza yao kwa kupitia nyimbo zake zilizobeba ujumbe wa kufariji na kutia moyo. Watu wamempokea huyu Bwana Yesu Kristo kwa kupitia sauti ya Edson Mwasabwite.
Leo hii kuna watu wanaweza kukaa chini na kumsikiliza Edson Mwasabwite ambaye ni yatima na wakamshangilia, hakika hii ni kwa Neema na Rehema!!!
Siku ya Jumapili ni siku ya watu wote kukusanyika pamoja katika kanisa la K.K.K.T Sinza kumekucha kumsifu Mungu wetu na kumuunga mkono mtumishi wa Mungu Edson Mwasabwite. Hakutakuwa na kiingilio kabisa na tamasha litaanza mida ya saa 7:00 mchana na kuendelea.
![]() |
Comments