JIFUNZE KUMWITA MUNGU KATIKA TESO LAKO .


Neno la Mungu linasema Musa alipokutana na mateso alimlilia Mungu."Bwana akamwambia Musa, mbona unanililia?Waambie wana wa Israeli waendelee mbele. Nawe inua fimbo yako, ukanyooshe mkono wako juu ya bahari,na kuigawanya;nao wanawa Israeli watapita kati ya bahari"(Kutoka14:15-16)
Ebu tujifunze kitu hapo, jiulize swali hili hivi Musa asinge mlilia Mungu je! angevuka hapo? Au je! angepata maarifa kutoka kwa Mungu ya kutumia fimbo hiyo ili watoke katika teso lao?
Kama Musa alilia ndipo Mungu alipompa maarifa ya kufanya, je! wewe na mimi? Watu wengi wamekwama kwenye mateso yao miaka mingi sana kisa ni hiki KIWANGO CHAO CHA KUMWITA NA KUMLILIA MUNGU KWENYE SHIDA YAO NI KIDOGO. Ebu tujifunze wapendwa kwa Hana pia. Alimlilia Mungu kwa kiwango cha juu kiasi hata kuhani alifikiri amelewa pombe. Ebu fikiri alikuaje? Ngoja kidogo nikuulize, umewahi muona mlevi aliyelewa mpaka akashindwa kusema ila midomo yake ikicheza? Basi picha hiyo ndiyo iliyokua kwa Hana. alililia weeee!!! Nguvu zikamwishia za kusema midogo ikawainacheza, kuhani akafikiri kazidiwa na pombe.
Unajua kunawatu wanajiliwa na hali hiyo ila hawajui kuitumia. Siku ukilifikilia teso lako, na ukajisikia kuugua na machozi yakawa njiani kutoka nakwambia fahamu huenda ni siku ya kujiliwa kwako. USIJIKAZE JIACHIEEE!!!
Kama ndiyo kulia liasana, utashangaa mkono utakuwa juu yako na kukutoa kwenyeshida yako. "Nimechoka kwa kuugua kwangu; Kila usiku nakieleza kitanda changu; Nalilowesha godoro langu kwa machozi yangu"(Zaburi 6:6) Angalia maneno haya pia, "Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, pindi wanaponiambia mchana kutwa, yuko wapi Mungu wako"(Zaburi42:3).
Sikiliza neno hili, "Wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha" (Zaburi126:5). Ebu jiruhusu kumlilia Mungu kwenye hilo teso lako. naamini atakuja kukutoa na kukupeleka kunako WINGI.
na Mwl Steven Gwasa Mwakatwila

Comments