JINSI MAOMBI YATAKAVYO KUSAIDIA KUJUA MPANGO WA MUNGU KWAKO.


Bwana Yesu asifiwe!
Na Emmanuel Kamalamo.
Mara nyingi maombi yanaonekana kama mzigo kwa baadhi ya wakristo na kuona nikama adhabu kwao, na kushindwa kuomba hata saa moja kiwango ambacho ni cha chini.
Lakini huwezi KUFANIKIWA kama hutawekeza MUDA katika maombi. Na kama unataka kumpata MKE /MUME SAHIHI ATOKAYE KWA BWANA lazima uwekeze muda mwingi kwenye maombi ili Mungu akuongoze.
Yesu Kristo kwa sehemu kubwa maisha yake yalitawaliwa na maombi, na ndiyo maana alifanikiwa maeneo mengi kwa njia ya MAOMBI. Waebrania 5:7"YEYE, SIKU HIZO ZA MWILI WAKE, ALIMTOLEWA YULE, AWEZAYE KUMWOKOA NA KUMTOA KATIKA MAUTI, MAOMBI NA KULIA SANA MACHOZI AKASIKILIZWA KWA JINSI ALIVYOKUWA MCHA MUNGU"
TAFUTA MPANGO WA MUNGU
KWAKO.

Ukisoma maneno ya Yeremia 29:11-13 utaona ndani yake kuna mambo au mipango Mungu ameiweka ili tuipate, na ili tuweze kuipata njia pekee lazima "TUOMBE KWA BIDII" na kama hatutaomba hatutaweza kupata.
Yeremia 29:11 "Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho".
Kwa kiingeleza anasema.."For I know the plans I have for you, say the Lord, plans for welfere and not for evil, to give you a future and hope.

Lile neno "MAWAZO" limetumika kama "PLANS" maana yake mipango.Na kama ni mipango lazima ina majibu yote ya maisha yako, ndiyo maana kuna neno pale "FUTURE" maisha yako ya baadaye.Na "HOPE" yaani "TUMAINI", tafsiri nyingine za biblia limetamkwa kama "PROSPERITY" yaani "MAFANIKIO"
Tafsiri ya kisasa inasema.."MAANA MIMI MWENYEZI-MUNGU NINAJUA MAMBO NILIYOWAPANGIA. NIMEWAPANGIENI MEMA NA WALA SI MABAYA, ILI MPATE KUWA NA TUMAINI LA BAADAYE."
Hivyo tutasema.."MUNGU ANAJUA MIPANGO ALIYOTUPANGIA, SI MIPANGO MIBAYA , NI MIPANGO YA KUTUFANIKISHA BAADAYE"
Kwa mantiki hiyo, kuna kufanikiwa katika maisha kunakoletwa na Mipango ya Mungu aliyoiandaa tayari ili kukufanikisha KIFEDHA, KIAFYA,KUKU MKE/ MUME NK. Ili uione MIPANGO YA MAFANIKIO kwako lazima uuombe kwa bidii, mstari 12-13 anasema..."NANYI MATANIITA, MTAKWEDA NA KUNIOMBA. NANYI MTANITAFUTA NA KUNIONA, MTAKAPONITAFUTA MOYO WENU WOTE.NAMI NITAONEKANA KWENU, ASEMA BWANA" Kuonekana kwa Mungu kwako ni kujidhihirisha kwako kwa namna ya kukupa majibu ya maombi yako yaliyoombwa kupitia mpango wake.
Ok, tumwangalie Yesu jinsi alivyowapata WANAFUNZI wake. Luka 6:12-13 "Ikawa siku zile aliondoka kwenda mlimani kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu....aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili ambao aliwaita mitume."
Ili Yesu awajue walioandaliwa na Baba yake kwa ajili ya kutembea nao na watakao kabidhiwa majukumu ya baadaye ili mpasa "KUOMBA" kwa maombi mazito ya usiku kucha ili ajue ni nani kakusudiwa maana wanafunzi walikuwa ni wengi, kwa jinsi ya mwili asingeweza kuwajua.
Kwa hiyo kaa ukijua kama utakuwa mvivu katika MAOMBI hutaweza kujua mpango wa Mungu kwako.
Paulo alimwambia Filemoni hivi.."NA PAMOJA NA HAYO UNIWEKEE TAYARI MAHARI PA KUKAA; MAANA NATARAJIA YA KWAMBA KWA MAOMBI YENU MTAJALIWA KUNIPATA". Filemoni 1:22.

Paulo alijua ya kwamba wanamuhita na wamekuwa wakiomba wampate, hivyo Paulo alijua kwa maombi yao watampata basi waandae mahari pa yeye kukaa .
KAMA HUJAOKOKAOKAKA LEO
BAADA YA KUFA NI HUKUMU
(Waebrania 9:27)

MUNGU WANGU AKUBARIKI
By Emmanuel Kamalamo.

Comments