JINSI YA KUISHI MAISHA MAPYA NDANI YA KRISTO UWAPO DUNIANI.

By Emmanuel Kamalamo.

Bwana Yesu asifiwe!
Ninayofuraha kubwa ndani ya Kristo Yesu kwa ajili yako mpenzi nikupendaye katika Kristo. Fuatana nami ktk somo hili na Mungu atakubariki, Amen.
Tunaposema "MAISHA MAPYA NDANI YA KRISTO" maana yake ni mwito wa kuishi mfumo wa maisha matakatifu yasiyo TAWALIWA au KUONGOZWA na mfumo wa dunia hii inayo tawaliwa na DHAMBI.
Maana dunia hii ina mungu wake na watu wake, pia mfumo wa maisha yake ni matendo maovu (dhambi)

Paulio alipoliandika kanisa la Korintho alisema..."Kwa kanisa la Mungu lililo Korintho, wale waliotakaswa katka Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu..". Sasa ukisoma huo mstari kuna neno limesema "WALIOTAKASWA" kwa kiingeleza ni "SANCTIFIED" au "SANCTIFICATION" maana yake "UTAKASO" Ok..Nini maana ya "UTAKASO" ? Utakaso ni hali ya KUTENGWA na Mungu kwa kutolewa katika mambo ya dunia hii kwa ajili ya KUSUDI MAARUMU.
Kwa mantiki hiyo, kuokoka si maneno tu bali ni wito na ni badiliko la kimaisha linatokea ndani ya mtu.
Ndiyo maana si watu wote wanaweza kuishi katika wito huu kama hawajaukubali wito huo. Kama uamini soma Biblia utaambiwa...."MAANA MUNGU HAKUTUITIA UCHAFU, BALI TUWE KATIKA UTAKASO" 1 Wathesalonike 4:7. kama wewe unapenda uchafu wa POMBE, UZINZI, UASHERATI, WIVU, HASIRA, MASENGENYO nk. wewe haujaitwa, si mimi nimesema ni neno limesema.
Ndiyo maana Paulo anasema.."BASI IKIWA MTU AMEJITAKASA KWA KIJITENGA NA HAO, ATAKUWA CHOMBO CHA KUPATA HESHIMA, KILICHOSAFISHWA, KIMFAACHO BWANA, KIMETENGENEZWA KWA KILA KAZI ILIYO NJEMA" 2 Timotheo 2:21
UTAWEZAJE SASA KUISHI MAISHA MAPYA?
Utaweza kuishi MAISHA MAPYA NDANI YA KRISTO utakapoita wito wa kumpokea Yesu Kristo awe Bwana na Mwikozi wa maisha yako.
YOHANA 1 12 "Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu..".
Kumpokea Kristo ni kukubari WITO wa Mungu ili uupokee na ukuunganishe na Yesu ili uwe NDANI YAKE na Yesu NDANI YAKO.."Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya" 2 Wakorintho 5:17 na hapo Kristo anaishi ndani yako kwa mfumo mpya, na mayokeo ya Yesu kuishi ndani yako yataoneka katika maisha yako hapa dunia, na ndipo utaoneka tofauti na wasiookoka ktk MAVAZI, MAZUNGIMZO, MATENDO yako na hapo utasema..."WALA SI MIMI TENA, BALI KRISTO YU HAI NDANI YANGU." Wagalatia 2:20


Tunaendelea...

KAMA HUJAOKOKAOKOKA LEO
BAADA YA KUFA NI HUKUMU
(Waebrania 9:27)

MUNGU WANGU AKUBARIKI.
By Emmanuel Kamalamo

Comments