KIPIMO CHA IMANI YAKO NI MWENENDO WAKO

Na Frank Philip


"Menendo" kwa tafsiri yangu, ni mjumuisho wa mambo matatu: kuwaza, kunena na kutenda.

Pamoja na kwamba mara nyingi sana mwenendo unachukuliwa kama ni matendo tu, ziku zote huwezi kutenda bila kuwaza. Kwa hiyo KUWAZA kwako ndiko kunapelekea MATENDO yako. Kwa upande mwingine, hata kama hukutenda, jinsi unavyozungumza, inaonesha UWAZANYO au UWEZO WAKO wa KUTENDA jambo. Kwa ujumla, mwenedo wako (mawazo, maneno na matendo yako) utaonesha KIWANGO cha imani yako. Unawazi nini, unasema nini, na unafanya nini, hapo ndipo imani yako ilipofikia.

Kwa bahati mbaya sana, watu wanajua kwamba "imani huja kwa KUSIKIA Neno la Kristo", ila mwenye imani ni yule ATENDAYE sawa na Neno la Kristo, sio aliyesikia tu, ndio maana tunaambiwa "imani bila matendo imekufa nafsini mwake". Sasa ona hapa, "imekufa nafsini mwake", sio haipo nafsini mwake, ila imekufa, kwa sababu moja tu, iko kama "WAZO" tu ndani ya nafsi/moyo ila matendo yako ni TOFAUTI na hilo WAZO nafsini/moyoni mwako. Basi, lile Neno la Kristo ndani ya nafsi yako ambalo "hujalitenda", jua ni kama imani mfu ndani yako, na halizai kitu.

"Kwa imani wakapita kati ya Bahari ya Shamu, kama katika nchi kavu; Wamisri walipojaribu kufanya vivyo wakatoswa. Kwa imani kuta za Yeriko zikaanguka, zilipokwisha kuzungukwa siku saba. Kwa imani Rahabu, yule kahaba, hakuangamia pamoja na hao walioasi; kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi kwa amani. Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii; ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni. Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa. Lakini wengine waliumizwa vibaya hata kuuawa, wasikubali ukombozi, ili wapate ufufuo ulio bora; wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani; walipigwa kwa mawe, walikatwa kwa misumeno, walijaribiwa, waliuawa kwa upanga; walizunguka-zunguka wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi; walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya; (watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao), walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika na katika milima na katika mapango na katika mashimo ya nchi. Na watu hao wote wakiisha kushuhudiwa kwa sababu ya imani yao, hawakuipokea ahadi; kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi" WAEBRANIA 11:29-40).

KILA SIKU UKITAJA IMANI, LAZIMA USEME UMEFANYA NINI SIO UNAJUA NINI!

Frank Philip.

Comments