MAKANISA SABA Sehemu ya kwanza na ya pili.

76
Kanisa la Pergamo linavyoonekana sasa.(Na mtumishi Gasper Madumla.)
Bwana Yesu asifiwe…
Basi nakusalimu ndugu mpendwa katika jina laYesu Kristo,nikisema;
Haleluya…

Nakukaribisha katika fundisho hili linalohusu yale makanisa saba tunayoyasoma katika kitabu cha ufunuo kuanzia sura ya pili na sura ya tatu.
Watu wengi wameshindwa kuelewa mafunuo au kile kilichoandikwa katika makanisa saba.

Watu wengine wanadhani kuwa makanisa haya saba ni kama hadithi ya kufikirika hivi. Lakini mimi leo nakuambia kwamba makanisa haya saba sio makanisa yakufikilika bali ni makanisa yaliyopata kuwepo kiuhalisia kabisa.
Hivi karibuni nimepata bahati ya kuyatembelea kanisa moja hadi kanisa jingine na ndio maana leo nimeamua nikuandikie wewe mpendwa usomaye ujumbe huu sasa.

Makanisa saba yameandikwa katika kitabu cha ufunuo (Ufunuo sura ya 2 & 3).
Kitabu cha ufunuo ni kitabu cha kipekee kabisa maana chenyewe muandishi anajitambulisha kwa jina lake kwamba ni yeye aliyeandika lakini kile alichokiandika si chake,bali ni cha Bwana.Yohana mtume anajitambulisha kuwa ni yeye aliyesikia na kuyaona maono hayo na kuyaandika, maana tunasoma;

” Nami Yohana ndimi niliyeyasikia na kuyaona mambo hayo…. “Ufunuo 22:8
Pia hata mwanzoni mwa kitabu hiki cha ufunuo tunaona akianza kijitambulisha kwamba ni yeye Yohana ndie aliyekuwa katika kisiwa cha Patmo kwa ajili ya Neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu ( Ufunuo 1:9)
Lakini kile alichokiandika hakikutoka kwake Yohana bali kimetoka kwa Bwana Yesu,maana imeandikwa;

” Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi. “Ufunuo 22:16
●Hivyo basi,Yohana katika makanisa saba na kitabu chote cha ufunuo amefanyika kama malaika wa Bwana Yesu.
Neno malaika katika lugha ya Kiyunani lina maana ya mjumbe. Yohana ni mjumbe aliyeambiwa ayaandike mambo yote aliyoyasikia na kuyaona.

Neno ” saba” huwakilisha ukamilifu. Ujumbe wa makanisa saba ni ujumbe wa makanisa yote yaliyo chini ya Kristo katika ukamilifu wake. Hivyo haimaanishi ujumbe ule ni kwa yale tu makanisa saba,bali ni ujumbe wa makanisa yote bali yale saba ni kielelezo tu kwa habari ya makanisa yote ulimwenguni.
● Makanisa sita kati ya yale saba hayako hai. Isipokuwa kanisa moja tu ndilo li hai mpaka sasa. Nisemapo kwamba makanisa sita hayako hai nina maana kuwa makanisa hayo sita yamebakia magofu tu,yamekufa isipokuwa kanisa moja tu ndilo linalodumu kuwa na ibada zake mpaka leo,nalo kanisa hilo ambalo limebakia kuwa hai ni kanisa la SMIRNA ( Ufunuo 2:8).
Watu wengi hudhania kuwa makanisa haya saba hupatikana Israeli sababu wanajua kwamba Israeli, Yerusalemu ndipo alipotokea mwokozi Bwana Yesu. Lakini kumbe sivyo!
Makanisa haya yapo Asia ndogo Uturuki.
Asia ndogo ndipo kuna mambo mengi ya kujifunza yahusio imani yetu ya ki-Kristo.
Ikumbukwe kuwa ;
nchi ya Uturuki ilikuwa miongoni mwa nchi ya kiKristo,lakini sasa ni nchi yenye waislamu wengi kuliko wakristo. Inakadiriwa kuwa asilimia 99 ni waislamu na asilimia 1 ni wakristo.

Zipo sifa kuu nne zinazofanana kwa makanisa haya yote,nazo ni;
01. Makanisa yote yameandikiwa ujumbe unaoanzia kwa neno la ” KWA MALAIKA WA KANISA”
~Kumbuka hili;
Nilikuambia neno malaika kwa Kiyunani ni mjumbe. Hivyo yule msimamizi wa kanisa husika ni mjumbe wa siri za ufalme wa Mungu. Siku ya leo,mchungaji ni mjumbe au malaika.
Kazi moja wapo ya mjumbe ni kupeleka habari sahihi kwa watu sahihi na kwa muda sahihi.
Mchungaji pia kwa sababu yeye ni mjumbe amepewa kazi hiyo ya kupeleka ujumbe wa Mungu kwa watu sahihi na wakati sahihi. Atakiwi kuongeza wala kupunguza ujumbe aliopewa na Mungu kama vile alivyokuwa malaika aliyesema naye Yohana.

02.Yesu Kristo amejitambulisha uweza wake katika makanisa yote saba.
Ukisoma kitabu cha Ufunuo,
Ufunuo 2:1b,8b,12b,18b, Ufunuo 3:1b,7b,14b.
Utagundua kwamba yapo maneno yenye kuonesha utambulisho wa nguvu na mamlaka ya jina la Yesu.

03.Makanisa yote saba yamepewa maonyo makali.
04.Makanisa yote yalipoandikiwa,yameambiwa “
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.”
~Hii ikimaanisha kwamba ,ikiwa umesikia maagizo ambayo Roho amekuambia basi huna ujanja wa kukwepa maagizo hayo,kwa sababu ulisikia.

● Bwana Mungu wetu ni Mungu mwaminifu sana maana kile alichokisema kwa yale makanisa saba ndicho kilitokea,tazama sasa makanisa haya yamebakia ni mapango ya watalii,badala ya kuwa ni nyumba za ibada. Kile kinachoonekana sasa ni kwamba watu hawa wa kale walijihusisha pia na kuiabudu miungu mingine hata ikawa ni chukizo kwa Bwana Mungu. Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu,hataki uwe mzinzi wa kiroho yaani uabudu miungu.

● Wagunduzi wa mambo ya kale wamegundua kuwepo kwa kisima cha ubatizo wa maji mengi karibu katika kila kanisa.Ingawa visima hivyo vya ubatizo wa maji mengi havitumiki kwa sasa sababu ya kubomolewa kwa makanisa hayo lakini ile namna tu ya kuwepo kama magofu,ni ishara tosha kwamba suala la ubatizo lilikuwa ni UBATIZO WA MAJI MENGI na wala si ubatizo wa kunyunyizia.
● Hapo mwanzo waamini walipoliamini jina la Yesu,basi saa ile ile walibatizwa kwa maji mengi kama vile Kristo Yesu alivyobatizwa,ambaye Yeye Yesu ndie kielelezo chetu,hivyo nasi hatuna budi kubatizwa kwa maji mengi.
Siku ya leo tunaanza kujifunza kwa kulichambua kanisa la Pergamo japo ni kwa ufupi kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Ufunuo 2:12-17.
01.KANISA LA PERGAMO.
57
Kanisa la Pergamo linavyoonekana kwa sasa.
74
Kanisa la Pergamo,linavyoonekana kwa sasa.
~Neno Pergamo limetokana na neno mwinuko. Kanisa la Pergamo lipo juu ya mlima mlefu ambapo kwa sasa kama mtu atahitaji kwenda huko juu,basi hana budi kutumia ” cable car”- Cable car ni lifti ya umeme mfano wa gari linalosafili upande mmoja hadi upande wa pili wa mlima.
~Pergamo ulikuwa mji upo ndani ya Asia ndogo.
~Kanisa la Pergamo lilikuwa takribani kilomita 100 kaskazini mwa Smirna na kilomita 25 kutoka pwani. Umbali huu wa kutoka katika kanisa la Pergamo hadi kanisa la Smirna ni sawa na umbali wa kutoka Dar es salaam hadi Chalinze,kwa wakazi wa Dar.

~Hivyo utagundua kwamba,kulikuwa na umbali mkubwa sana kati ya kanisa hadi kanisa,
Lakini watumishi hawakusita kuyatembelea makanisa haya.
Je ingelikuwa leo,unafikiri ingelikuwaje?maana wakristo wa leo kwa vizingizio vya kuchoka! Ni hatari!

~Mji huu ulikuwa ndio makao makuu ya mamlaka ya kirumi. Na ndipo mahali ambapo ibada za Kaisari zilikuwa zikifanyika.
~ Alikadhalika,palikuwa na hekalu la mungu zeu akiabudiwa, (Matendo 14:13)
Ndio maana pale tusomapo barua hii,utakuta biblia ikisema;

“Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani;… ” Ufunuo 2:13
~Hivyo,ile namna ya kumuabudu mungu mwingine ilikuwa ni chukizo sana kwa Mungu wetu,Yesu alipafananisha mahali hapo na kiti cha enzi cha shetani.
~ Pergamo ulikuwa maharufu sana kwa kuwa na maktaba kubwa ya vitabu.Kupitia maktaba hii,watu wa Pergamo walianza kujitengenezea vitabu vyao wao wenyewe kwa kuandika katika ngozi za wanyama.

56
Kanisa la Pergamo,linavyoonekana kwa sasa.
~Nyenzo hii ya kuandika maandishi katika ngozi ya wanyama wakaliita kwa jina la “perchment”yaani gombo.
~Kanisa hili,linakadiliwa kudumu ndani ya miaka 225 hivi,yaani kutoka mwaka wa 313 B.K hadi mwaka wa 538 B.K.

Bwana Yesu asifiwe sana…
Bwana Yesu anaanza kuwasifu waamini wa kanisa hili,kwamba ni watu walioshika sana jina lake ingawa wanakaa katikati ya kiti cha enzi cha shetani. Tena Yesu anasema kwamba watu hawa hawakuikana imani yao kwake ingawa wakizungukwa na maovu.(Ufunuo 2:13)
◆ Waamini wa kanisa hili walijua siri ya kulishika jina la Bwana.
◆ Waamini hawakuzingatia maasi yote yaliyowazunguka.
◆Mungu aliwaona tangia mbali.

Jambo moja kubwa tunalojifunza kupitia kanisa hili la Pergamo ni;
◆Kukaza kulishika jina la Bwana Mungu katikati ya maovu ya dunia hii.
Endapo kama hatutaikana imani yetu tuliyoipokea kwake Bwana Yesu,basi ushindi ni haki yetu.
Siku zote mazingira huzungumza kinyume kabisa na imani yetu,lakini yatupasa kulishika jina la Bwana. Yatupasa kudumu katika imani ile ile ya maisha ya wokovu.

~ Shida kubwa ya kanisa ili ni kuwa na baadhi ya watu ndani ya kanisa wenye kuyashika mafundisho ya walimu wa uongo. Tazama imeandikwa;
” Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.
Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile. “Ufunuo 2: 14-15.
◆ Mafundisho ya Balaamu,na ya Wanikolai ni mafundisho ya walimu wa uongo. Maana imeandikwa;
” Tazama, hawa ndio waliowakosesha wana wa Israeli, kwa shauri la Balaamu, wamfanyie Bwana dhambi katika hilo jambo la Peori, na kwa hivyo pigo lilikuwa katika mkutano wa Bwana. ” Hesabu 31:16

Watu wa kanisa na watu wa mji huu,wakajisahau na kuyashika mafundisho ya walimu wa uongo na hatimaye adhabu ile ile waliostahili waipate walimu hawa,ndio iliwapata watu hao.
Kumbe!
~Ukiambatana na waovu basi adhabu yako ni sawa na wale waovu.

Mafundisho ya uongo wa Balaamu na ya Wanikolai ilikuwa ni kuwafanya wana wa Israeli wawe wazinzi. Uzinzi unaozungumzwa hapa ni ule uzinzi wa kiroho,kwa kumuacha Mungu wa kweli na kuigeukia miungu kwa kuiabudu.
Mungu wetu siku zote ni mwaminifu mmno,maana hata wakati ule aliwapa muda wa kutubia uasi huu wa kuambatana na mafundisho ya walimu wa uongo. Hata leo pia ameachilia nafasi hii ya kutubia maovu yako yote,ili uwe safi ukaendelee kumtumikia katika roho na kweli. Lakini usipotubu utaangamia katika uovu huo!
◆Kwa huduma ya maombi na maombezi,basi usisite kunipigia kwa namba yangu hii;
0655-111149.

ITAENDELEA…
@ Mtumishi Gasper Madumla.
UBARIKIWE.

Mtumishi Gasper Madumla.

Comments