MAKANISA SABA.*sehemu ya tatu na nne''

Camera360_2014_10_1_090914_jpg
Nikiwa natoa maelezo kidogo. Hapa ndipo kanisa la Sardi lililopokuwepo.
Bwana Yesu asifiwe…
Leo ni siku ya tatu tukisoma barua za Yohana kwa yale makanisa saba. Kumbuka tulikwisha jifunza kwa kifupi habari za kanisa la Pergamo,pamoja na habari za kanisa la Thiatira.
Siku ya leo tunaenda kujifunza kwa kifupi juu ya barua kwa kanisa la SARDI kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Ufunuo 3:1-6
Camera360_2014_10_1_100631_jpg
Kanisa la Sardi linavyoonekana kwa sasa.
●KANISA LA SARDI.
~Sardi ulikuwa ni mji wa zamani.
~ Sardi ilikuwa karibu kilomita hamsini kusini mwa Thiatira.
~ Hapa Sardi ndipo palikuwa na mungu mke aliyekuwa akiitwa Artemis( Artemis temple)
~Inaaminika kuwa alikuja mfalme anaeitwa MAIDASI alitawala mahali hapa (Spelling za maidasi haziko sawa,lakini ndivyo inavyotamkwa)
~Inasemekana kuwa mfalme huyu alikuwa ana uwezo wa kugusa kitu na kuwa dhahabu.
~Hivyo Sardi ukashamiri sana kwa biashara maana hata barabara muhimu tano zilikutana hapo,ambazo zilifanya  kuwepo kwa biashara iliyo hai na kuupa mji umaarufu.
~Eneo lililozunguka mji lilikuwa na nafasi nzuri ya kufuga kondoo,kwa hiyo Sardi ilikuwa kituo cha biashara ya manyoya na nguo.
~ Inasemekana hapo baadaye miaka ya 333 KK ,mfalme Alexandra mkuu akaja na huku,akakaa hapo.
◆ Ujumbe kwa kanisa la Sardi.
~ Ujumbe kwa kanisa hili unaanza kwa kumtaka malaika wa kanisa la Sardi,huku Bwana Yesu akijitambulisha kuwa ni Yeye ambaye mwenye hizo Roho saba za Mungu na zile nyota saba ( Ufunuo 3:1)
Bwana Yesu anajitambulisha kwamba Yeye ndie mwenye mamlaka juu ya hayo makanisa na nyota saba.
Katika barua ya kanisa hili,tunaanza kusoma
“… Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.” Ufunuo 3:1
Bwana Mungu anayajua matendo yako yote na wala hafichiki kwa chochote kile ukifanyacho.
Sikia hii;
~Mtu mmoja alinichekesha kwa matendo yake. Siku moja alifanya dhambi alitoka na mke wa mtu kwa kujificha ficha ili asije kuonekana na mke wake,ila hakujua kwamba Mungu aonaye sirini alikuwa akimuona. Na ndivyo watu wengi hufanya,utakuta watu wana waogopa watu wenzao kuliko Mungu ambaye anawaona kila kitu.
◆ Ukijificha kwa mwanadamu,kwa Mungu U wazi. Bwana awajua wote,biblia inasema;
” Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu. ” 2 Timotheo 2:19
~ Katika kanisa hili la Sardi walikuwepo watu wenye jina la kuwa hai,lakini kumbe wamekufa.
Kama vile leo hii;
Inawezekana una jina la Kristo,lakini umekufa kwa habari ya dhambi.Au
Inawezekana ni muuzuliaji mzuri sana wa kanisani,lakini umekufa kwa habari ya dhambi.
Na hata inawezekana una heshimika katika huduma fulani hapo kanisani kwako unapoabudu,lakini kiukweli  umekufa na hata nafsi yako inakushuhudia kwamba umekufa. Leo Bwana Yesu anakuhitaji uanze moja na Yeye yaani utengeneze mahali ulipoanguka.
Bwana Yesu asifiwe…
◆ Katika kanisa hili la Sardi,Bwana alipowaambia ya kuwa wana jina lililo hai,lakini wamekufa. Hapo haikutaja dhambi yoyote walioifanya kama jinsi yalivyo makanisa mengine.
Shida  kubwa inalolikumba kanisa la leo ni shida ile ile iliopo katika kanisa la Sardi,shida ya kuwa na jina lililo hai lakini kumbe wamekufa. Watu wengi wameingia kuitwa majina makubwa ya kitakatifu mfano watu hujiita ” makuhani ” hali matendo yao ya kiroho hayaendani na hadhi ya makuhani. Watu wa namna hii ni wana majina ya Kikristo hali wamekufa.
◆ Biblia hapa,inapozungumza kwamba mtu mwenye jina la Bwana hali amekufa. Huzungumzia mtu wa kanisa,mtu mkristo, mwenye jina la Kristo na wala si mtu wa mataifa. Neno ” kufa ” limetumika kuonesha kifo cha kiroho pasipo kujijua. Mfano mtu mwenye jina Kristo lakini amekufa kiroho kwa sababu ya dhambi.
Bwana Mungu amekupa nafasi ya kipekee siku ya leo,nafasi ya kutubia kila aina ya uovu wowote ulioufanya wenye kulichafua jina lako hata ukaitwa umekufa.
◆ Inawezekana yapo mambo yenye kulichafua jina lako la wokovu, na labda inawezekana ulikwisha kuomba lakini bado unajikuta ukiangukia katika dhambi. Sasa siku ya leo nataka niombe na wewe mpendwa wangu katika Kristo. Nipigie katika namba yangu hii;
Misingi ya kanisa la Sardi lilivyobaki hivi sasa. Na mtumishi Gasper Madumla.
Bwana Yesu asifiwe…
Karibu tuendelee ikiwa leo ni siku ya nne ya kujifunza habari za makanisa saba yalioandikwa katika kitabu cha UFUNUO 2 &3.
Kama tulivyokuwa tumejifunza wiki iliyopita juu ya kanisa la Sardi japo ni kwa ufupi. Leo kabla hatujaliangalia kanisa jingine basi ngoja tumalizie kujifunza hilo la Sardi tulilokuwa tumeshalianza.
Kumbuka kuwa,uchambuzi wa makanisa haya saba ninaufanya kwa ufupi kwa kila kanisa.

Tunasoma (Kwa habari ya kanisa la Sardi),
Imeandikwa;
” Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako.

Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili. ” Ufunuo 3:3-4
~Inaonesha kuwa,wapo watu katika kanisa hili la Sardi waliopata Neema ya kusikia mambo mazuri ya imani yao juu ya Bwana Yesu. Wanaambiwa wayashike sana na watubie. Mara nyingi neno la Bwana lijapo kwako yakupasa kulisikia kwa makini na kulishika,kisha kutubu mbele za Bwana Yesu.
Angalia;

◆Sardi anahimizwa kukesha.
~Kibiblia neno ” kukesha na Bwana”humaanisha kudumu katika mawasiliano na Mungu kama vile kwa njia ya maombi. Bwana Mungu anatutizamia tuokoke wote na tuishi maisha ya ushindi muda wote.

◆Sardi ilikuwa na wachache wenye kuishi katika maisha ya toba,watu hawa walikuwa safi na ndio hao Bwana anasema wataenda pamoja nao,kama vile Bwana atakavyoenda pamoja na watu wasafi wa leo.
◆ Pia ngoja nikueleze habari za kanisa jingine la nne,japo kwa ufupi mno (ni kanisa la nne lakini sio kwa mpangilio kama ulivyoorodheshwa katika biblia). Tujifunze ma barua kwa kanisa la Filadelfia.
[IV] KANISA LA FILADELFIA.
20141001_124638
Nikiwa na baadhi ya watumishi,hapa kwa nyuma inaonekana moja ya nguzo ya kanisa la Filadelfia. Mimi ni wa tatu kutoka kushoto waliosimama.
~ Filadelfia unaojulikana kwa jina la ALASEHIR maana ndio jina la mji huu,ulianzishwa na Attalos II ( 159-138 BCE)
~Filadelfia ukawa ni mmoja wa mji wa kirumi na utawala wa Byzantine.
~ Filadelfia ilikuwa yapata kilomita arobaini kusini mashariki mwa Sardi katika barabara kuu iliyounganishwa na miji mingine kama Smirna na Pergamo.

~ Umuhimu wa mji huu ulikuwa ni mdogo kuliko miji ile sita.
~ Filadelfia,kwa sasa ni magofu ya nguzo na misingi ndio iliyobakia.

~ Katika matamko yale sita kwa makanisa mengine,Filadelfia basi ni moja ya kanisa lililotamkiwa vyema sana kuliko mengine. Hivyo kila mmoja aliyebahatika kufika katika eneo lililokuwa kanisa hili,ni dhahili kabisa anaweza akafikiri kwamba kanisa hili li hai. Kumbe nalo limekufa!
~ Mji wa Filadephila unaitwa ALASEHIR.
~Asili ya umuhimu wa mji huu ni kuwepo kwa mashamba ya zabibu yaliyostawi katika uwanda wa Volkano.

~ Hivyo basi,watu wa mahali hapa wakajikuta wanamuabudu mungu “dionisio(dionysus)” mungu huyu alikuwa ni mungu wa divai.
~Watafiti wa mambo ya kale wanasema kuwa neno “Philadelphia ” lilitokana na neno upendo.
~ Filadelfia ilikuwa na ibada nyingi sana,lakini sio kubwa kama ile ya artemi huko efeso.

~ Palikuwa na desturi ya kuandika jina la raia mashuhuri katika nguzo za mahekalu haya.
~Hata hivyo,katika barua hii ya Filadelfia,hakukua na maonyo makali sana,ingawa kanisa la Filadelfia linaonekana halikuwa na nguvu sana.

~ Hivi sasa eneo la kanisa hili limebanwa sana,yaani padogo kuliko maeneo ya makanisa yote sita,tena pembeni mita chache mno kuna msikiti.
~Hakuna kinachoendelea mahali hapa zaidi sana imebakia kumbukumbu.

~ Watafiti wanasema kuwa,katika karne ya 17,kanisa hili lilikumbwa na tetemeko na likajengwa tena na Tiberius ambaye alipewa jina la pili akaitwa Neo-Caesarea.
~Katika mwaka wa 1391 mji ukatekwa na waturuki.

Katika kitabu cha Ufunuo 3:7-13-Habari za kanisa la Filadelfia;
Tunaanza kuona mpangilio hule hule unaofanana kwa makanisa saba. Mpangilio huu unaanza kwa kumtaja malaika wa kanisa husika lakini pili Bwana Yesu anajitambulisha. Kisha tunasoma sasa;

“Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu. “Ufunuo 3:8
~ Bwana Mungu ni Mungu aonaye sirini maana aliyajua matendo yote ya Filadelfia,kama leo jinsi ajuavyo matendo yako yote.
~Filadelfia lilipewa mlango,ikiwa na maana kuwa Filadelfia lilipewa mamlaka kwa sababu amelitunza jina la Bwana Mungu.

◆ Kumbe ipo mamlaka apewayo yule anayelishika jina la Bwana.
~Kulishika jina la Bwana ni kule kuokoka na kudumu katika neno laYesu.

◆ Kwa huduma ya maombi na maombezi,usisite kunipigia kwa namba yangu ya simu hii;
0655-111149.

ITAENDELEA…
UBARIKIWE.
By Mtumishi Gasper Madumla.

Comments