MAOMBI MAKALI YA KUMTESA SHETANI.

Na Peter Michael  Mabula.
WAPIGE KWA MOTO WA JINA LA YESU KRISTO MASHETANI WOTE WANAOHARIBU MAWAZO, Omba maombi haya.

Kwa mamlaka ya Jina la YESU KRISTO mwana wa MUNGU aliye hai ninawashia moto mashetani wote mnaoniletea mawazo mabaya kwenye akili yangu, mnaopindisha mawazo yangu ambayo MUNGU ameniwekea kwa jina la YESU KRISTO . Ninawasha moto kwa mashetani yote yanayonijia kupindisha njia zangu kwa damu ya mwana kondoo, kuanzia leo mimi sio maskini kwa jina la YESU KRISTO. Imeandikwa; “mwana wa MUNGU alidhihiriswa ili azivunjee kazi za ibilisi kuzimu,” Ninazivunjavunja kazi zote za kuzimu kwa jina la YESU KRISTO, mnaopindisha mawazo ya maendeleo yangu ninawafyeka kwa upanga wa KRISTO. Katika jina la YESU enyi jeshi la mashetani mliotumwa kuja kuniletea matatizo kwenye maisha yangu ninawatetekeza kwa moto wa MUNGU aliye hai. Imeandikwa, “neno la MUNGU ni moto ulao.” Ninawateketeza mashetani wote mliotumwa na waganga wa kienyeji, wachawi mmetokea kuzimu ninawateketeza kwa moto wa Mungu kwa jina la YESU KRISTO.
Asante BWANA YESU kwa kunipa ushindi mkuu.
Ni katika jina la MUNGU BABA, MUNGU MWANA na MUNGU ROHO MTAKATIFU nimeomba. Amen.


MWITE SHUJAA WA MSALABA YESU KRISTO KWA MAOMBI HAYA NA UTASHINDA.

Tunawafuata adui zetu palepale walipo, tunawatokea kwenye ulimwengu wa Roho na kuwakanyaga na kuwanyanganya mali zetu na vitu vyetu vyote kwa nguvu ya msalaba wa YESU KRISTO . Kwa jina la YESU nimepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yule adui kwa jina la YESU. Kwa nguvu ya msalaba ninawafuata wachawi, waganga wa kienyeji na adui zangu wote katika ulimwengu wa roho waliokaa kikao kinyume na mimi, ninawaponda vichwa kwa jina la YESU KRISTO. Imeandikwa wakamshinda kwa damu ya mwanakondoo, ninawashinda kwa damu ya YESU KRISTO. Ninazikanyaga mamlaka zote za giza kwa damu ya mwanakondoo. Kwa nguvu ya msalaba, kwa damu ya mwanakondoo ninawashambulia wote mnaotumia baraka yangu, ninauponda uzao wa joka katika jina la YESU KRISTO. Ninawashambulia mashetani katikati ya uzao wa wanadamu kwa jina la ESU. Kwa damu ya mwanakondoo, ninavifuatilia vipawa vyangu vilivyofichwa katika mashimo kwa jina la YESU. Ninaitumia nguvu ya msalaba kwa jina la YESU KRISTO, waliofichwa kwenye mashimo, kwenye mapori, baharini, kwenye mwezi, kwenye, kwenye anga ninawarudisha kwa damu ya YESU KRISTO. Kwa jina la YESU KRISTO ninaamuru warudishwe, natumia nguvu ya msalaba kwa damu ya YESU KRISTO, biashara zilizofungwa, kazi zilizofungwa ninazifungua kwa jina la YESU KRISTO. Nakwenda msalabani, msalaba wa furaha, msalaba wa ukombozi, msalaba wa ushindi, msalaba wa nguvu, msalaba wa maarifa nakata rufaa hapo kwa jina la YESU KRISTO. Asante BWANA YESU kwa ajili ya kunifia msalabani, asante kwa ajili ya nguvu iliyomo ndani ya msalaba. Asante kwa ukombozi, uponyaji na msamaha wako. Ni katika jina la YESU KRISTO nimeomba .
Amen.


 JIFUNIKE KWA DAMU YA YESU SIKU ZOTE KWA MAOMBI HAYA.

BWANA MUNGU Ninakushukuru Kwa Kunilinda, Asante Kwa Damu Ya Mwanao YESU KRISTO Inenayo Mema Siku Zote. Najifunika Kwa Damu Ya YESU KRISTO, Ninawafunika Ndugu Zangu Wote Kwa Damu Ya YESU KRISTO, Nafunika Familia Yangu, Ndugu Zangu, Nyumba Yangu, Biashara Yangu, Ofisi Yangu, Chakula Changu, Fedha Zangu, Kiwanja Changu, Rafiki Zangu, Majirani Zangu Huduma Yangu Na Kila Kinachonihusu Kwa Damu Yenye Nguvu Ya YESU KRISTO Wa Nazareth. Ninalifunika Anga Lote, Nchi Yote Na Bahari Yote Kwa Damu Ya YESU KRISTO. Imeandikwa Katika Ufunuo 12:11 " Nao Wakamshinda(shetani) Kwa Damu Ya Mwana Kondoo(YESU) Na Kwa Neno La Ushuhuda Wao" Ewe shetani, Nimeitumia Damu Ya YESU KRISTO Kukushinda Sasa Na Hata Milele Katika Jina La YESU KRISTO, jini mahaba nakutetekeza kwa jina la YESU KRISTO maana Neno la MUNGU katika Yeremia 1:10 kwamba MUNGU ameniweka juu ya falme zote za mashetani ili kuwang'oa mashetani, na kuwabomoa na kuwaharibu na kuwaangamiza kwa jina la YESU KRISTO. Sasa nawaangamiza majini wote waliotumwa kwangu kutoka kuzimu kwa jina la YESU KRISTO Amen.

Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292

mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.
MUNGU Akubariki.

Comments