MATOKEO YA IMANI HUTEGEMEA KIWANGO CHA NGUVU YA NENO LA MUNGU KILICHO NDANI YAKO (SEHEMU II)


Bwana Yesu asifiwe!
Namshukuru Mungu kwa nafasi hii tena, ambayo ambayo ametupa ili tujifunze zaidi Neno ili tujue kile anachotaka tujue katika Neno lake.
Na Emmanuel Kamalamo.
Tuliangalia jinsi IMANI ilivyo njia ya kupitisha na kupokelea kutoka kwa Mungu yale uyaombayo. Lakini, hiyo IMANI ina chanzo chake ambacho lazima uwe umekianzisha mwenyewe kwa NENO LA MUNGU. (Basi Imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa Neno la Kristo Warumi 10:17)
Ndyo maana ukijaza NENO LA MUNGU ndani yako siku zote utatamka kupata mambo makubwa sana ambayo mtu akikutaza kwa jinsi ya mwili atakushangaa, kwa nini akushangae?.... Kwa sababu umetaja mambo makubwa ambayo kwa akili zake hatagemi wewe kuyapata maishani mwako.
Lakini hajui kwamba wewe unaishi kwa NENO, na kama unaishi kwa NENO maana yake unajua kuwa Mungu anakutendea mambo makubwa kuliko hayo uombayo au uwazayo kwa kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yako.

ILI UONE MUNGU ANAFANYA
MAMBO MAKUBWA NDANI
YAKO ISHI KWA IMANI.

Habakuki 2:4 "...Lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake. Kwa tafsiri nyepesi tunasema… "ALIYEOKOKA ATAISHI KWA NENO" Utauliza mbona hakusema "NENO" amesema "IMANI" sasa fikilia pamoja na mimi, kama IMANI inachanzo chake ambacho ni NENO LA MUNGU lazima uishi kwa Neno la Mungu, kama huna Neno basi IMANI haiwezi kuwa imani.
Kama uamini nenda kwenye Biblia yako uwe na uhakika lazima Yesu atakwambi… "MTU HATAISHI KWA MKATE TU, ILA KWA KILA NENO LITOKALO KATIKA KINYWA CHA MUNGU" Mathayo 4:4. Ni mtu yupi hataishi kwa chakula? Mtu wa ndani(aliyeokoka). Neno la Mungu ni chakula cha MTU WA ROHONI ni si wa MWILINI, ndiyo maana mtu wa mwilini hapokei NENO LA MUNGU kwa sababu mtu wa ndani(yaani nafsi na roho imekufa)
Kwa mantiki hiyo, kama hujaokoka huwezi kuishi kwa IMANI, kwa sababu umekufa ingawa unaisha….. Sisi mimi nimesema, Neno limesema…. "NANYI MLIKUWA WAFU KWA SABABU YA MAKOSA NA DHAMBI ZENU" Waefeso 2:1 Kwa hiyo Habakuki anaposema "MWENYE HAKI ATAISHI KWA IMANE YAKE" ok! Haki unaipata wapi? Unaipata unapookoka, Neno linasema, Yesu asiyejua DHAMBI alifanywa DHAMBI ili sisi tupate HAKI.

Kwa hiyo tuliokoka tuliyozaliwa mara yapili kwa Neno la uzima tuwapo duniani tunaishi kwa IMANI… Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona. (2 Wakorinto 5:7) Ibrahimu alipoambiwa aende katika nchi asiyoijua alikwenda kwa Imani, maana yake alikwenda kwa kutarajia mambo yasiyooneka.
Tunaendelea….
KAMA HUJAOKOKOA WOKOVU
NI SASA SI KESHO.

MUNGU WANGU AKUBARIKI.
By Emmanuel Kamalamo.

Comments