
Mh. Fredrick Sumaye
Tamasha hili litaambatana na uimbaji kutoka kwa waimbaji mbalimbali kama vile Christina Shusho, Madam Ruti, Christopher na wengine wengi. Uzinduzi utafanyika siku ya Jumapili 02/11/2014 kuanzia saa 8 mchana, kwahiyo unaombwa kuwahi mapema ili ujipatie nafasi nzuri ya kukaa. Mbali na uzinduzi tamasha hili limeandaliwa kwaajili yako wewe kuja kumsifu Mungu, na hakuna kiingilio kabisa.

Victor Aron
Victor Aron ataimba LIVE nyimbo zaidi ya tano kwa utukufu wa Mungu.Akiongea na Rumafrica, alisema yeye na crew yake wamejiandaa vya kutosha na hawana wasiwasi kabisa siku hiyo, kwahiyo anaomba sana watu wafike na ikiwezeka kila mmoja aje na marafiki zake kupokea baraka zao kwa njia ya sifa.
Comments