Mh Edward Lowassa amewahutubia waumini
wa kanisa la Ufufuo na Uzima katika Uzinduzi Wa helkopta ya Kuhubiri
Injili pamoja na kusaidia zoezi la uokoaji wa majanga mbalimbali kama
vile wakati wa Ajali,Mafuriko,Moto nk. Mh Lowassa amesema atashirikiana
nao na kuhakikisha wanapata eneo la kudumu la kuabudia.Kwa upande wake
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo Josephat Gwajima amesema Mpango wao
ifikapo mwezi kama huu mwakani watakuwa wameshaagiza helkopta nyingine
tatu kwa ajili ya kuhubiri injili na kusaidia katika shughuli za
kijamii.
|
Mgeni
Rasmi wa uzinduzi na uwekwaji wa Helkopta ya Kanisa la Ufufuo na Uzima
Mh. Edward Lowassa akisalimiana na baadhi ya wachungaji baada ya
kuwasili kanisani. |
|
Pastor Deo Lubala akisema neno... |
Mtume Venon Hernandez alikuwepo pia.
|
Mchungaji kiongozi wa kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima akisema neno wakati wa ibada ya uzinduzi leo |
|
Picha zote na kijana wa nguvu John Pazia |
Comments