MLINZI WA KWELI NI YESU PEKE YAKE.

Na Godfrey Miyonjo
""BWANA asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure"" ZABURI 127:1.
Mtu awaye yote asipojisalimisha kwa YESU, huwa hatarini daima,
Asipoamua kuwa na ushirika na BWANA wa mabwana, hakika aweza tekwa muda wowote.
Asipotambua uwepo wake YEHOVA, huyo ni mtumwa wa shetani.
Mtu huyo hata kama atalindwa na majeshi yooote ya hapa duniani, haitamfaidia kitu chochote,
Kwa maana hao wamlindao mtu asiye na YESU, biblia inasema wafanya kazi bure,
Kwasababu pamoja na kumlinda kwao, mtu huyo huweza kuvamiwa na jeshi la mapapepo.
Pamoja na kusimama na mitutu yao, lakini mtu huyo huweza kuvamiwa na wachawi na kumfanya vile watakavyo.
Tumewaona wengi walio na walinzi wao wakiangushwa na mapepo,
Watu na heshima zao, wanaweweseka usiku wa manane kwa kuona maluelue katika ndoto au dhahiri/hadharani.
Watu wanahama nyumba zao zilizo na mageti ya nguvu pamoja na walinzi wa kutosha kwasababu ya kuwaogopa wachawi.
Hii ni kwasababu hawana ule ulinzi wa kiroho,
Walinzi wao huwalinda mwilini tu, lakini rohoni waweza kutekwa na wao wakiwa wamesimama na mitutu yao, na wasiweze kuwasaidia lolote,
Ndiyo maana ninasema, mlinzi wa kweli ni YESU peke yake,
Yeye akikulinda wachawi hawawezi kukugusa,
Majini yanateketea kwa moto wa damu ya YESU kabla hayajakufikia.
Mapepo yanakatwakatwa kwa upanga wa Roho Mtakatifu, kabla hayakuvamia na kukugalagaza,
Hakika Kwa YESU kuna usalama wa kutosha.
NINATAMANI WATU WOTE WAMWAMINI YESU.
MUNGU akubariki sana.
By Godfrey Miyonjo.

Comments