Sio kitu rahisi kuwakalisha watu wenye pesa zao, wakabaki
kukuangalia wewe na kukufurahia huku wameacha kazi zao za msingi za
kuigiza mafedha katika makampuni yao. Ninamuangalia Masanja ninashindwa
kumumaliza, hakika ukifanya kazi ya Mungu kwa uaminifu na kutumia kile
kipaji alichokupa mwenyezi Mungu vizuri na kwa faida ya jamii
inayokuzunguka nakuambia Mungu hatakuacha.
Angalia hizi picha, watu
wamebaki wanashangaa mavituzi anayoachia mtumishi wa Mungu Masanja
Mkandamizaji, wengine wamebadilisha hata mkao wa kukaa, akili zao na
mawazo yao ni kwa Masanja Mkandamizaji. Kijana anazidi kukandamiza Neno
la Mungu kwa nguvu zake zote na akili zake zote akiongozwana Roho
Mtakatifu. Ukisikiliza shuhuda zake, kuna shuhuda huwa inanichosha sana
hasa ile ya miguu yake kuliwa funza akiwa kijijini kwao huko Njombe kama
sikosei.

Masanja amekuwa akisema majukwani kuwa mwendo anaotembeaga siku hizi sio ule wa zamani akiwa na mafunza, ila anajaribu kubadilisha ili alingane na watu wa mjini, kuna kipindi huwa nanajisahau na kujishtukia anatembea ule mwendo kipindi ameliwa na funza. Lakini leo hii watu wanamtamani hata kama ni kijana kutoka kijijini na aliliwa na funza..Yesu amemtengeneza na kuwa asali na ua ridi. Angalia miguu yake...amepiga ndula ya nguvu na suti ya nguvu huku akiwaacha watu hoi kwa kuwachekesha na pia kufundisha Neno la Mungu.

Ninachotaka kusema kwako ni kwamba, heshimu hiyo nafasi aliyokupa Mungu na itumie kipindi hiki ungali hai. Utafika umri au wakati utashindwa kufanya kazi ya Mungu na hicho kipaji chako kikabaki kuwa historia tu na kutupwa kapuni. Huu ni wakati wa kuonyesha maajabu na kufanya kazi ya Mungu kama huna akili nzuri. Ninampenda sana Masanja Mkandamizaji, ananipa changamoto sana kazini kwangu, ninamuombea sana mwenyezi Mungu azidi kumbariki na azidi kukichochea hicho kipaji chake ili kifanyike baraka kwa watu wa Mungu na jamii inayomzunguka. Watu wakapate kuokoa na kutangaza Neno la Mungu duniani kote.
MUNGU awabariki sana.
By Rulea Sanga
Rumafrica.

Comments