ROHO NYUMA YA MAFANIKIO YAKO – III

Na Frank Philip.


“Ndipo Daudi akashika nguo zake akazirarua na kadhalika watu wote waliokuwa pamoja naye; wakaomboleza, wakalia, wakafunga hata jioni, kwa ajili ya Sauli, na kwa ajili ya Yonathani mwanawe, na kwa ajili ya watu wa BWANA na kwa ajili ya nyumba ya Israeli; kwa sababu wameanguka kwa upanga.” (2 Samweli 1:11,12).

Nilipozidi kutazama habari za Daudi, nilizidi kuona mambo mengi, naam, mengine yakachosha akili za nafsi yangu, nami nikachoka sana. Wakati Bwana anamkataa Sauli asiwe mfalme, Bwana alisema “yuko mwingine mwema zaidi yako”, kumbe! Alisema habari za Daudi mwana wa Yese. Nikatafuta wema wa Daudi na kuuona, huu umepita akili yangu kuelewa. Kwa mfano, Iweje adui yako, aliyewinda roho yako na kukufukuza nyikani na milimani kwa miaka, afe, kisha uomboleze badala ya kusema, “asante Bwana kwa kuniokoa na adui zangu”? Kama haikuwa kwa dhati, kwanini Daudi na watu wake walilia na kufunga? Ona sasa, hata mleta habari, na mtu aliyeinua mkono juu ya Sauli alihukumiwa kifo! Akafa kwa upanga.

Nikatazama jambo hili, katika kufanikiwa kwake, Daudi akawa mtu mkuu sana. Katika kupanda kwake cheo na utukufu, hakubaki nyuma wenzake walipoenda vitani, naam, hata walipothubutu kupenya jeshi la Wafilisti, kuteka maji kutoka katika kambi ya adui, na kumletea Daudi bwana wao, alikataa kwa maana aliona “ni sawa na kunywa damu yao, kwa maana walihatarisha maisha yao sana ili kumpatia Daudi kikombe cha maji”. Daudi akaona bora akae na kiu kuliko kunywa maji ya namna hii! Hakusema, “naam, mimi ni mkuu, na nyie sio kitu uhai wenu, mmefanya vyema kunitumikia mimi mfalme wenu”.

Nikaona hukumu za Mungu juu ya Daudi nikasikia hofu kuu, nikamwogopa Mungu kuliko mwanzo, naam, mimi Frank nikamwogopa Mungu. Daudi alipomtwaa mke wa mtu, na kuingia kwake, na kisha kumuua mumewe, kwa maana mfalme aliona ni akili kusitiri uovu wake kwa njia hiyo, na kuona ni vyema kumwoa huyu mjane ili kumtendea wema. Je! Hii haikuwa chukizo mbele za Bwana? Ndipo Bwana akasema “nitainua uovu juu ya nyumba yako”. Ona sasa, ghafla! Absalomu, mwana wa Daudi anapindua nchi, anajitangazia ufalme, anashawishi watu kwa maelfu, hata sasa wanamwinda Daudi, babaye ili kumuua. Ndipo nilipotazama na kuona mfalme mkuu, jemadari wa vita, mtu mwenye cheo akikimbia nyikani kujificha kwa sababu ya kuogopa mkono wa mwana wa viuno vyake mwenyewe! Nikaona mfalme wa Israel, na Yuda, mtu mkuu sana, akipanda mlima huku analia, amechoka sana, anakimbia mkono wa Absalomu mwanae! Ndipo na mashujaa waliokuwa naye wakalia, wakipanda mlima huku wamefunika vichwa vyao.

Na hata sasa nikatazama jambo hili, Daudi alichukua mke wa mtu mmoja, kwake ikawa mara 10; Absalomu akalala na wakeze 10, mbele ya Israel wote, mchana peupe! Kila mtu akajua jambo hili, naam, hata Daudi akajua pia. Hili jambo likawa maumivu yaliyouchoma moyo wa Daudi, kama upanga wa moto uliopenywezwa katikati ya moyo wake bila ganzi. Na hata sasa, haikutosha, akiwa katika kukimbia kwake, anakuja mtu asiye kitu, hata anamtukana mfalme wa Israel, na kumnenea maneno magumu hadharani mbele ya watumishi wake, ndipo mashujaa waliokuwa pamoja na Daudi wakasema “kwanini tusiondoe kichwa cha huyu mtu mahali pake?” Bado Daudi alikataa! Akaona “amestahili hata hilo nalo”!

Nikajiuliza sana, kama Daudi alijua kupigana kuliko wanaume wengi wa Israel, naam, akiwa na wale 37, na wale 3 kati yao, ambao mmoja aliua watu mia nne kwa pamoja kwa shoka lake; na mwingine alipiga jeshi zima mwenyewe, kisha wengine wakaja kuchukua nyara tu; na mwingine aliua simba, watu wakubwa, mashujaa kama yule Goliathi wa kwanza, sio kwa upanga wala kwa mkuki ila kwa gongo tu; hawa ndio wale waliopenya kambi ya mashujaa wa Kifilisti, na kuteka maji ya adui, na kurudi na maji kwa amani bila kuonekana na mtu! Je! hawakuweza kumkamata Absalomu na kumfunga kamba kama ndama mchanga? La! Daudi hakupigana hapo, alijua kufanya mapenzi ya Mungu, alipigana na ADUI ZA MUNGU sio ADUI ZAKE! Je! Absalomu hakuinuka kwa sababu ya ule uovu wa Daudi? Basi Daudi akiwa na moyo wa akili sana, alijua kupita hapo, mahali pa moto, huku anamlilia Mungu na kutubu sana, yamkini wakati huu ndio aliandika ile zaburi ya 51, nani ajuaye? Daudi akatubu kwa dhambi na makosa yake. Ndipo nikajifunza maana ya gharama ya dhambi zetu!

Na hata sasa, watu kati ya mashujaa wa Israel, wakiwa pamoja na Daudi, wanapigana dhidi ya jeshi kubwa kama mchanga wa bahari, jeshi ambalo kiongozi wake ni Absalomu, mwana wa Daudi, akipigana dhidi ya babaye! Na sasa Daudi akijua jambo hili, na akijua ushujaa na uhodari wa watu wake, walikuwa wepesi kama kulungu, hata kama ni wachache kuliko adui zao, hawakawii kuondoa kichwa cha Absalom mahali pake, ndipo Daudi akawaonya na kusema “angalieni huyo KIJANA Absalom, msimtende jeuri”, Daudi alijua kwamba watamkamata kwa hakika, ila hakutaka auawe, licha ya kufanyiwa vurugu! Huyu ni adui wa Daudi aliyenyanyuka kinyume naye! Naam, na kuangusha ufalme wake, na kulala na wake zake 10. Bado Daudi alikuwa na rehema juu yake!

Na hata sasa, Absalom ameanguka juu ya nyumbu wake, kwa maana alinasa kwenye tawi la mti akiwa vitani dhidi ya Daudi, naam, hata mashujaa wa Daudi wakamfikilia. Lo! Tazama ni mwana wa mfalme ameanguka! Wakarejea nyuma kwa kuogopa kuunyoosha mkono wao juu ya mwana wa mfalme. Ndipo Yoabu, jemadari wa vikosi vya Daudi, akiwa na hasira, aliona haimpasi Absalomu kuishi japo kwa sekunde moja zaidi, akamkimbilia na kuteremsha ndevu zake kuzimu na damu. Ona jambo hili, siku ile, “walioliwa na msitu” walimokuwa wakipigana vita, ni wengi kuliko walioliwa na upanga! Naam, je! Si msitu pia uliomnasa Absalomu hata kuanguka chini? Na je! Siye Bwana aliyepigana kwa upande wa Daudi tena, japo alikuwa akimrudi huyo huyo? Je! Moyo wa Daudi ulishuka kwa marudia ya Bwana? La! Hasha, Daudi alijua kulindwa na GONGO la Bwana, na alijua kuchungwa na FIMBO yake pia; vyote viwili, gongo na fimbo za Bwana vilimfariji Daudi, hata ajapokuwa kwenye bonde la uvuli wa mauti hakuogopa mabaya. Na sasa, anasikia habari za kufa kwa adui yake Absalomu, Daudi analia na kuomboleza sana, na kusema, “Absalomu mwanangu, Absalomu mwanangu, aheri ningekufa mimi”!

Kwa habari za Daudi, nimeona mengi, naam, mengi yamenifundisha sana, ila nimeona hili pia; ana heri mtu yule asiyejua kulipiza kisasi, hasa kwa mapatilizo ya maovu yake mwenyewe, ila akajua kurudi kwa Bwana, kwa maana hapo kuna rehema na msamaha. Naam, kwa Mungu kuna msamaha, ili Yeye aogopwe. Hata kama dhambi zetu ni nyekundu sana, Yeye huzisafisha. Na je! Ni akili gani kufanya machukizo zaidi kwa sababu ya kutendewa mabaya? Je! Ubaya nitendewe mimi, halafu nimtende Mungu dhambi na kumkasirisha kwa sababu ya mwingine! Ndipo Suleiman, mwana wa Daudi, katika hekima zake akasema “Yeye arudishaye mabaya badala ya mema, Mabaya hayataondoka nyumbani mwake” (Mithali 17:13). Njia ya kushughulika na ubaya, uovu, na adui zetu ni kurudisha wema; na kukimbilia msalabani; sio kukimbilia kwa wanadamu na kwa Ibilisi. Je! BWANA Yesu hakutufundisha kuwapenda adui zetu na kuwaombea wanaotuudhi? Na kumtwika yeye fadhaha zetu kila siku? Basi tuone mtego huu tukiwa katika njia zetu za kufanikiwa ili uovu wetu, na wa wanetu, visiwe tanzi na mtego uangushao.

Frank Philip.
CANADA WASHUHUDIA MATENDO MAKUU YA BISHOP Z KAKOBE.ZIKO PICHA 8 HAPA On Saturday, November 8, 2014 the last but one day of the Soul Winning Gospel Crusade in Edmonton, Alberta; Bishop Zachary Kakobe requested each and every participant of the Crusade to write down on paper, ten personal prayer points and bring the said papers on the last day of the Crusade, Sunday, and the Servant of God said he shall pray for them and everyone will experience that God loves to answer our prayers. However, during the last day’s prayer session, before praying for them, a couple came out in front and gave the following testimony that inspired and stirred up the faith of all the participants, “In 2010, we attended Bishop Zachary Kakobe’s Crusade in Lusaka, Zambia where we lived at the time. During the last but one day of the Crusade, he requested us to bring with us ten personal prayer points on the last day of the Crusade. We did so and he prayed for us. Since then Jesus has answered nine out of the ten prayers. Time doesn’t allow me to tell it all but to put it briefly, one of our prayers was that we wanted God to open doors for us to live in Canada and shortly after the Crusade, God answered our prayer and we came here in Edmonton, where we now live. Moreover, we also wanted God to give us a second child. Our first born was 13 years old then and despite all efforts of doctors, we had no other fruit of the womb during all those thirteen years. And you know what, just shortly after the Crusade, my wife conceived and we got our second child. When we came to Canada, our second child was 6 months old. Thereafter, while we had already moved here, we got the third child. Currently our first born is in Africa and here with us are our miracle children, the second and the third child. Praise The LORD, we are a living testimony of how God loves to answer our prayers. When we heard the news that Bishop Kakobe will be coming to Edmonton, we were very excited and today we are here because we believe the answer to our remaining prayer point is on the way!” This testimony greatly inspired the Crusade participants resulting in many signs and wonders accompanying the preaching of the Word and the prayer of the Servant of God. To God be all the Glory, forever and ever!

Make Money at : http://bit.ly/copy_win

Comments