![]() |
Na Mchungaji Maxmiliani Machumu, Ufufuo na Uzima ,Kawe. |
“Wakafika
ng'ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi. Na alipokwisha kushuka chomboni, mara
alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu; makao yake yalikuwa
pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa
minyororo; kwa
sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile
minyororo, na kuzivunja-vunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za
kumshinda. Na
sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na
kujikata-kata kwa mawe. Na alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga
mbio, akamsujudia; akapiga
kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu?
Nakuapisha kwa Mungu usinitese. Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu,
mtoke mtu huyu. Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu,
Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi. Akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi
ile. Na hapo
milimani palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, wakilisha. Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke
katika nguruwe, tupate kuwaingia wao. Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu
wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote likatelemka kwa kasi
gengeni, wakaingia baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini. Wachungaji wao
wakakimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. Watu wakatoka walione
lililotokea. Wakamwendea
Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, naye
ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa. Na wale waliokuwa wameona waliwaeleza
ni mambo gani yaliyompata yule mwenye pepo, na habari za nguruwe. Wakaanza kumsihi
aondoke mipakani mwao. Naye alipokuwa akipanda chomboni, yule
aliyekuwa na pepo akamsihi kwamba awe pamoja naye; lakini hakumruhusu, bali alimwambia,
Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawahubiri ni mambo gani makuu
aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu. Akaenda zake, akaanza kuhubiri katika
Dekapoli, ni mambo gani makuu Yesu aliyomtendea; watu wote wakastaajabu.”
Marko5: 1 - 20
Mema
ni fungu la wana wa Mungu, lakini linayo gharama ya kulipia ambayo ni utii.
Kuna watu leo wamekataliwa kutenda na kupokea mema na shetani kwa kukosa utii.
Mgerasi
huyu anayeongelewa katika kitabu cha Marko alikataliwa mema kwa kuwahiwa kwenye
akili yake. Akashidwa kuwaza mambo mema. Akili ilipofungwa hakuwaza mema na
kwasababu hakuwaza mema hakutenda mambo mema na kwasababu hakutenda mema
hakupata mema pia. Akawa na mazoea ya kutenda na mwisho hatma yake haikuwa
njema. Tatizo la watu wengi ni mawazo yao. Unapowaza mawazo mazuri utatenda
mambo mema na mema yanakufuata. Waweza kuwa milionea leo lakini kama una mawazo
ya kimaskini ni muda tu kabla hujawa maskini.
Huyu
mgerasi aliwaza na miguu yake ikampeleka mpaka makaburini na midomo yake
ikaanza kupiga kelele na mikono ikaanza kujikata. Ni kwasababu ya mawazo ya
mashetani yaliyoingia ndani yake yalimpeleka makaburini mbali na makusudi
ambayo Mungu aliyaweka ndani yake. Kumbe kuna mawazo ambayo mtu huwaza na ni ya
kishetani na yana lengo la kumpeleka mbali na makusudi ya Mungu katika maisha
yake.
Watu
wengi leo wanaishi matokeo ya mawazo waliyowaza ambayo yalikuwa ya kishetani na
ndio yaliyowapelekea kupatwa na uchungu bila ya wao kujua. Unapoanza kuwaza
mambo yasiyo ya kawaida jua kwamba shetani anatafuta kitu ndani yako au
anajaribu kupindisha kusudi la Mungu katika maisha yako.
Kuna
mawazo mengine yanakuja ndani ya watu yanaonekana kana kwamba ni ya ki-Mungu lakini ni ya kishetani. Baadae mawazo haya huharibu mema ambayo Mungu
alipanga kwa ajili ya maisha ya mtu huyu. Na kawaida shetani akishakupa wazo
moja baya na wewe ukalipokea, shida itakapokupata atakupa wazo la pili na la
tatu mpaka ahakikishe amekutoa nje kabisa ya kusudi la Mungu. Kuna mawazo Mungu
ameshatuwekea ndani yetu ili tuwe watu wema na wenye kuzaa mema. Lakini shetani
kwa kulitambua hili huwahi ndani ya akili zetu na kupandikiza mawazo ya ubaya. Hivyo maisha ya mtu huyu yanakuwa yameandamwa
na kila baya; misiba, kushindwa, kukataliwa.
Na
ili usije ukahangaika na kupata akili zako tena, shetani huweka walinzi ili
wahakikishe hurudi kwenye kusudi la Mungu. Walinzi hawa ndio majini, mizimu na
miungu mbalimbali. Mfano yawezekana kuna mtu ambaye ukishirikiane naye katika
biashara utafanikiwa kwa sababu ipo baraka ya kiMungu kwa ajili yako ndani
yake; walinzi hawa huhakikisha wanakupindisha uende kwa mtu tofauti atakaye
kupeleka katika laana.
Lakini
ninayo habari njema kwako leo; ya kwamba hata shetani na mawakala wake
wakupeleke mbali kiasi gani na kusudi la Mungu yupo mwanaume Yesu atakufuata
huko huko. Kama alivyomfuata yule mgerasi kule makaburini na wewe pia
atakufuata. Simama leo, chukua nafasi yako kama mwana wa Mungu ukatii ili upate
kula mema ya nchi.
UKIRI
Kwa
mamlaka ya Jina la Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai ninawashia moto
mashetani wote mnaoniletea mawazo mabaya kwenye akili yangu, mnaopindisha
mawazo yangu ambayo Mungu ameniwekea kwa jina la Yesu. Ninawasha moto kwa
mashetani yote yanayonijia kupindisha njia zangu kwa damu ya mwana kondoo,
kuanzia leo mimi sio maskini kwa jina la Yesu. Imeandikwa; “mwana wa Mungu alidhihiriswa ili
azivunjee kazi za ibilisi kuzimu,” Ninazivunjavunja kazi zote za kuzimu
kwa jina la Yesu kristo, mnaopindisha mawazo ya maendeleo yangu ninawafyeka kwa
upanga wa Kristo. Katika jina la Yesu enyi jeshi la mashetani mliotumwa kuja
kuniletea matatizo kwenye maisha yangu ninawatetekeza kwa moto wa Mungu. Imeandikwa,
“neno
la Mungu ni moto ulao.” Ninawateketeza mashetani wote mliotumwa na
waganga wa kienyeji, wachawi mmetokea kuzimu ninawateketeza kwa moto wa Mungu
kwa jina la Yesu.
Asante Bwana Yesu kwa kunifuata na kuniokoa leo, nipe neema ya kuishi sawasawa na mapenzi yako ili niweze kupokea yale mema ambayo ni haki yangu kama mwana wa Mungu. Amina!
Comments