UMESHIKILIA MNYORORO UPI


Kuna Wakristo wengi sana ambao kwa kweli wameshikilia minyororo mizito sana na wengine kudiriki kuikumbatia kabisa hiyo minyororo pasipo kuona shida yeyote.
Baadhi ya majina ya minyororo hiyo ambayo watu wengi sana wameishikilia na kuona kuwa ni sawa tu kuwa na hiyo minyororo.


Minyororo hiyo ni

-TAMAA-1 Petro 2:11 ''Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho. ''
 
-KIBURI-Mithali 16:18 ''
Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko. ''
 
-MATUKANO-Waefeso 4:29 ''
Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia. '',Wakolosai 3:8 '' Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu.   ''
 
-UASHERATI-1 Wakorintho 6:18 ''
Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.   '',1 Wathesalonike 4:3 '' Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; ''.
 
-UCHUNGU MOYONI-Waefeso 4:31 '' 
Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; '',Matendo 8:23 '' Kwa maana nakuona u katika uchungu kama nyongo, na tena u katika kifungo cha uovu. ''.
 
-UONGO-1 Timotheo 4:2 ''
kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; ''
 
-MAWAZO MACHAFU-Warumi1:21 '' 
kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. ''
 
-UOVU-1 Petro 2:1 ''
Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote. ''

-KUJICHUA- 1 Petro 2:11 ''
Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho. ''

Nataka kukuambia kuwa kama Yesu Kristo aliacha kiti chake cha enzi huko mbinguni chenye kila aina ya uzuri,utukufu na nguvu na akaja duniani kuja kufa cha aibu kabisa kwa ajili yangu na wewe.
Kwanini basi hutaki kuiacha hiyo minyororo(dhambi) na uje kwake leo hii ili uokoke (Yohana 3:16,
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. ).
Kama ungependa kuokoka na kwa ushauri zaidi usisite kutafuta kanisa la kiroho ambao wanaifundisha kweli ya MUNGU.
Ubarikiwe sana katika jina la Yesu!!

By Godwin Mlay.

Comments