UWEKEZAJI NA UJASIRIAMALI KWA WANANDOA

Na Frank Philip

Definition: kwa mtazamo wangu, “Ujasiriamali sio biashara wala mradi, ila ni hali ya moyo (state of mind), inayompelekea mtu kufanya mambo fulani, yenye uwezo wa kuingiza kipato, au kuboresha maisha, kwa njia ambazo ni rahisi (uwekezaji wa muda, nguvu na mali uwe kidogo kuliko faida) na halali.” Kwa lugha nyingine, kuna wajasiriamali wengi sana BADO hawana mradi/biashara, nk., hawajathubutu bado. Kikwazo cha kwanza cha mtu KUSHINDWA sio kukosa mtaji, ila MOYO wa KUTHUBUTU. Kuacha kazi SIO ujasiriamali, japo wajasiriamali wengi sana huacha kazi za kuajiriwa baada ya MIRADI yao ikishamiri!

Nakubali kwamba kuna watu wanahitaji symbolic language, (mambo halisi ya kuwasukuma kufanya wito wao, iwe ni kwa kiboko, kufukuzwa kazi, vurugu za hapa na pale, nk.,) ndio wasikie (wachukue hatua), hao ni wengi, na baadhi yao huacha kazi, kisha wakibanwa na maisha au hali fulani ngumu, hupata NGUVU ya ndani ambayo itachochea ule ujasiriamali ndani yao, nao huanza kufanikiwa. Kumbuka, kwa mtazamo wangu, hao watu walikuwa wajasiriamali tayari kabla ya mradi wowote kuwapo, na hiyo ndio tafsiri yangu ya ujasiriamali.

Nimewahi kufuatilia mafundisho na ushauri mbali-mbali juu ya UJASIRIAMALI na UWEKEZAJI, yakiambatana na KUACHA kazi ya kuajiriwa. Nakubaliana KIMSINGI na mawazo hayo, kwa maana mimi ni MUUMINI wa MAFANIKIO ambayo chanzo chake ni KAZI ya HALALI hasa ile ifanywayo PEMBENI au SAMBAMBA na ajira rasmi.

Sio kila mtu ataanza na WAZO la biashara, na kuingia kwenye biashara na KUFANIKIWA. Kweli wapo watu wataanzia mahali pa juu, ila wengi wataanzia mavumbini na kupanda taratibu, kulingana na KIASI cha IMANI, familia walizotoka, viwango vya elimu, marafiki wanaokuzunguka, nk.

Inapofika kwenye ndoa, kumekuwa na shida ya watu kutaka kufanya MAAMUZI magumu, bila kujali wenzao wanaelewa au la, na hii imesumbua familia sana. Kwa mfano, utakuta baba ANAMLAZIMISHA mama aache kazi ili WANZISHE biashara! Ni sawa, ila angalia hapo, kama unamtakia MEMA huyo mama, na akili yake ielewe, ANZISHA hiyo biashara ili uone FAIDA, ndipo na mama atakuwa na AMANI ya kuacha kazi yake na kuendelea na huo UJASIRIAMALI, angalia tena, "kuendelea na ujasiriamali", sio kuanza ujasiriamali baada ya kuacha kazi!

Katika biashara, miradi, nk., SWALI langu kubwa ni, je! hali ya UHUSIANO wa NDOA sio msingi wa mafanikio ya maeneo mengine? Jifunze kujua life philosophy yako na mwezio (sio imani tu), angalia mwenzako anaamini (belief system) nini? anamtizamo gani wa maisha, familia, biashara, ajira, nk. Kama kuna kitu kinanistua ni pale ninaposikia mtu anasema ANAACHA kazi ili AANZE ujasiriamali! Kama mtu akisema AMEACHA KAZI KWA SABABU YA UJASIRIAMALI, hapo sawa! Tena akiniambia kwamba AMEGUNDUA kwamba KAZI ZAKE ZA ZIADA (sio wazo lake tu) zinamwingizia KIPATO hadi amefika mahali akaona AKIACHA KAZI ATAPATA MUDA ZAIDI katika UJASIRIAMALI wake, ili kuboresha KIPATO na HALI ya maisha, hapo nampa PONGEZI, ni hatua njema.

Ukisikia mtu anasema “acha kazi TUANZISHE biashara/miradi,nk.", huyo nitamtazama kwa MASHAKA makubwa kwa maana NAAMINI katika EXPERIMENTATION & TESTING, Je! hilo wazo lako umelijaribu? Je! hilo wazo lako la biashara umelifanyia kazi na KULIPIMA na kujua kwa HAKIKA kwamba UTAZALISHA NA KUPATA FAIDA, ona hapa, "FAIDA ZAIDI YA KAZI YAKO YA SASA?" Mtu asipojibu maswali hayo hapo, nakushauri katika jina la BWANA, usinyanyue mguu hapo maana kama MUSA alikuwa nabii, na bado alituma watu kuipeleleza nchi kabla ya KUIVUKIA, usivuke hapo kwa IMANI, pata DATA, and quantified TRUTH/FACTS (figures and numbers) before you take a move. Usijifanye MJASIRIAMALI kwa IMANI, utaumiza familia yako bure, ANZA KWA VITENDO ndipo "umburute" na mwenzako huko, usimfanye mateka/mtumwa kwa sababu ya ndoa tu, eti, akuheshimu hata kama haoni FUTURE hapo. Akina mama wanataka assurance, security, etc., Take your own risk baba, kama unaacha kazi, acha wewe, mkeo mwache na yeye aone ataachaje, ILA kama UMESHAWEKEZA kuwekeza/kuanzisha miradi au biashara na KUONA MATUNDA ya nchi (usha pima nguvu ya majitu nakuona unayashinda, na umeyashinda majitu kadhaa tayari ya kuelezea ushindi wako kwa MIFANO), mshawishi/shauri mwenzio polepole with SOLID facts (vichala vya zabibu) ili akuunge mkono katika huo ujenzi wa miradi ya familia nanyi mtakula ASALI na MAZIWA kwa kweli, kwa maana BWANA ataibariki kazi ya mikono yenu.

Kumbuka siku ZOTE, hakuna aliyefanikiwa bila kuchukua some amount of RISK. The higher the risk, the higher the return BUT learn how to calculate the risks, and dare to go ahead. The biggest risk of all times is to avoid to take risks. Success has a nickname “daring”, if you don’t dare, you won’t succeed, hata kama imani yako ni ya kuangusha milima, lazima uchukue hatua, ili imani yako iitwe imani. Imani pasipo matendo imekufa “nafsini” (mawazoni/ideas) mwako.

Siku zote, usisahau, Daudi aliaminiwa kwa MIFANO ya simba na dubu alioua huko nyikani, ndipo watu wakamwamini kwa habari ya kumkabili Goliath pia. Don’t come by the name of faith kama huna kitu mkononi cha kuonesha watu, fanya kazi, chukua hatua, weka matunda mezani peupe machoni pa watu kabla mwenzako hajaanza kukuuliza MASWALI ya msingi na wewe ukaona unavunjiwa heshima baba.

This applies to women; don’t put your husbands into temptations (msiwamtie waume zenu majaribuni). Umesikia wanawake wenzako wanaenda China kufunga mzigo, ghafla! na wewe unaanza kumdai mumeo mitaji kwa UGOMVI na MATISHO, eti, unataka kwenda China! Ok, yamkini humdai mumeo, ila unatumia njia zako zingine bila makubaliano ya msingi, unaanza biashara bila kujua njia za hizo biashara, hatimaye unajikuta unafanya ‘MAMBO’ ya kuharibu HATMA yako, au ya ndoa yako. Hakuna mtu anayefanikiwa kwa KUIGA-IGA tu, jifunze SIRI ya kila jambo na kulijua kabla ya KUJIRUSHA kulifanya. Angalia mama, ndoa yako ina thamani kubwa kuliko PESA na MIRADI yako yote utakayowahi kupata au kufanya maishani mwako, uwe na moyo wa akili, busara, na hekima, UTAFANIKIWA tu.

Frank Philip.

Comments