UZINZI NA UASHERATI NI MAANGAMIVU MAKUU.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze kitu cha msaada sana kwa kusaidia kutoka ubayani na kuingia uzimani.
Leo nazungumzia  jambo ambalo linawatesa maelfu ya watu yaani uzinzi na uasherati.Yeremia 23:10 ''Maana nchi imejaa wazinzi; kwa sababu ya kuapa nchi inaomboleza; malisho ya nyikani yamekauka; mwenendo wao ni mbaya, na nguvu zao si za haki.''
Kuna wengine hata kwenye kitabu cha uzima mbinguni hawamo na kila siku wanaenda kanisani tatizo ni uzinzi na uasherati ambao  wanauendekeza kwa siri. ni mbaya sana.

MUNGU Amekataza Wanadamu Kuzini "Usizini-kutoka 20:14". -Wanaozini Ni Waasherati Na Wazinzi. 
-Waasherati Ni Wale Ambao Hawajafunga Ndoa Wakifanya Ngono Wao Kwa Wao Au Hata Wakifanya Ndoa Na Wale Walio Kwenye Ndoa Ni Dhambi Kuu, 
-Wazinzi Ni Wanandoa Wakitoa Nje Ya Ndoa Zao Ni Machukizo Makuu. 

Ndugu Zangu Kuzini Ni Dhambi. 
Walawi 20:10 Biblia Inasema "Na Mtu Aziniye Na Mke Wa Mtu Mwingine, Naam, Yeye Aziniye Na Mke Wa Jirani Yake, Na Mume Aziniye, Na Mwanamke Aziniye, Hakika Watauawa.". 
Zamani katika Israeli MUNGU aliagiza wazinzi na waasherati kuuawa mara tu wakikamatwa.
MUNGU anapokataza dhambi ni kwa sababu ya upondo wake mkuu kwetu.
Kuzini kuna madhara mengi sana ya kimwili na kiroho pia.
Kuzini ni agano la kipepo kati ya wahusika hao waliofanya hivyo.
Kuna vijana maagano hayo hata leo yanawasumbua.
Kuna wengine kuolewa leo imekuwa shida kwa sababu ya uasherati walioufanya zamani.
Kuna wamama wengine wameshindwa kuzaa leo kwa sababu ya maagano ya kishetani ambayo waliingia na wanaume siku za nyuma. Sehemu za siri zina kazi yake kwenye ndoa tu, Kuna watu leo ni tasa na wagumba kwa sababu tu ya kunyonywa sehemu za siri wakati hawajaolewa, ni hatari sana na kuna siri nyingi za kipepo kwenye hilo hata ni aibu kueleza.
Ndugu zangu, MUNGU anapokataza uzinzi na uasherati anakuwa na maana kubwa sana.
 Ndugu Zangu Vijana Wa Kiume Na Vijana Wa Kike "Ni Heri Kuoa/kuolewa Kuliko Kuwaka Tamaa- 1 Kor 7:9". Pia waliofunga ndoa takatifu wanatakiwa kuwa waaminifu kwenye ndoa zao, ndoa iheshimiwe na kila mwanandoa, kuna Adhabu kwa wazinzi. Waebrania 13:4 '' Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi MUNGU atawahukumia adhabu. ''
  Uzinzi Na Uasherati Ni Moja Ya Dhambi Zinazowakosesha Wengi, shetani Amewakamata Vijana Wengi Kwenye Dhambi, shetani Amewakamata Wanandoa Wengi Kwenye Uzinzi Nje Ya Ndoa Zao. Ndugu Yangu Unaesoma Ujumbe Huu Tambua Huu Ni Wakati Wa Kuacha Uzinzi Na Uasherati, Hakuna Wakati Mwingine Wa Kuacha Kuzini Ila Ni Wakati Huu. Tumtii MUNGU Kwa Kuikimbia Dhambi Hii Mbaya, Epuka Vishawishi Vya Uzinzi Na Uasherati Maana Ni Dhambi Mbaya Tena Ni Kovu la kudumu.
YESU anasema 
Mathayo 5:32 '' lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.''

Kuna Watu BWANA YESU Kila Siku Anagonga Hodi Kwenye Milango Ya Mioyo Yao Ili Awaokoe Wasiende Jehanamu, Lakini Watu Hao Wameshupaza Shingo Zao Ambazo Karibia Zinavunjika kwa sababu ya dhambi kama hizi Na Wokovu Hawajaupata. Ndugu Ukiisikia Sauti Ya BWANA YESU Kupitia Ujumbe Huu Au Ujumbe Wa Wateule Wengine Usishupaze Shingo Bali Mpokee BWANA YESU.Yavue Matendo Yako Ya Kale Na Uvae Jina Safi La YESU.
1 Kor 5:10-11'' Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang'anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia. Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang'anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.''

Wengi mnaona kuwa huu ni wakati wa kuponda raha hizo za kipepo kumbe ni kujiangamiza.
- Mwanadamu Mtenda Dhambi Je Unalingia Nini? 
-Unalinga Kutekwa Na shetani? 
Kuna Watu Wanamikiwa shetani, Yaani shetani Anamiliki Vinywa na miili yao yao Ndio Maana Vinywa na miili yao inawakosesha mbingu. 

Yakobo 4:4 '' Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa MUNGU? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa MUNGU. ''
Kuna Watu Miili Yao Anaitumia shetani Kwa Kuwafanyisha Uzinzi Na Uasherati. Mwanadamu Mtenda Dhambi Unalingia Nini? Wewe Ni Kama Maua Yatachanua Leo Na Kesho Yatanyauka. YESU Anakuhitaji Tena YESU Anakupenda Sana, Anataka Kukuokoa, Mpokee YESU Leo. Dhambi Hazitakufikisha Popote,
  Ufunuo 21:8 '' Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili''.
Ni Heri Kujikabidhi Kwa BWANA YESU Anayeokoa. 
-Dhambi Inaua, 
-Dhambi Inaharibu Uhusiano Wako Na MUNGU, 
-Dhambi Yako Inaifanya Mbingu Iwe Mbali Sana Kwako.
 YESU KRISTO Anaokoa, Ukiamini leo Utaokoka.
Mathayo 15:19-20 ''Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;
hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mtu unajisi. ''


 Wenye Haki Wataingia Mbinguni, Wenye Dhambi Wataingia Motoni. YESU KRISTO Anauwezo Wa Kuwafanya Wenye Dhambi Wasiende Motoni Bali Waende Mbinguni Kama Tu Wakiamua Kumpokea Leo Kama BWANA Na MWOKOZI Wa Maisha Yako, Kisha Wakashika Utakatifu Na Neno Lake.

'' Maana Haya Ndiyo Mapenzi Ya MUNGU, Kutakaswa Kwenu, Mwepukane Na Uasherati- 1 Thesalonike 4:3.'' 
MUNGU Hataki Wateule Wafanye Uzinzi Na Uasherati, Uasherati Ni Maagano Mabaya, Ni Kongwa, Ni Machukizo Makuu. Ni Dhambi Hadi Kwenye Mwili. Sodoma Na Gomora Waliangamia Kwa Sababu Ya Dhambi Hasa Uzinzi Na Uasherati. MUNGU Anakuambie Leo "epukana Na Uasherati". 
Siku Hizi Mabinti Wadogo Kabisa Yaani Miaka 13 Au 14 Au 15 Tayari Wengi Wao Wameshaingia Kwenye Maagano Haya Ya Miili, Wanaharibiwa Maisha Yao Na Wazee Wa Zaidi Miaka 55 Kwa Sababu Ya Uasherati. 
1Kor 10:8 ''ala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu. ''
Ndugu Yangu, MUNGU Anasema "epukana Na Uasherati".
- Kataa Roho Ya Yezebeli, Kataa Dhambi Hii, Ogopa Dhambi Hii, Ikimbie Dhambi Hii Na Usikubali Kufanya Dhambi Hii. 
 Waefeso 5:3-5 '' Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;  wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru.  Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa KRISTO na MUNGU. ''
Wababa Na Wamama Jiepusheni Na Dhambi Hii, Hata Kama Hujamzaa Binti/Kijana Huyo, Kwanini Kuzini Nae, Ana Umri Sawa Na Mtoto Wako Au Mjukuu Wako Kwanini Kumwingiza Kwenye Dhambi Hii Mbaya? Walawi 19:29 "Usimnajisi Binti Yako, Ili Kumfanya Awe Kahaba; Isiwe Hivyo Nchi Kuuandama Ukahaba, Na Nchi Kujawa Na Uovu Mkuu."

 Ndugu Yangu Mtenda Dhambi Hata Kama Utajiosha Kwa Sabuni Ya Omo Ukiongezea Na Sabuni Ya Komoa Kama Hujatubu Kwa MUNGU Aliye Hai Kupitia YESU KRISTO Dhambi Yako Haijafutika.
Warumi 10:9-13 ''Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka.
Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika. Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni BWANA wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la BWANA ataokoka. ''


 BWANA YESU Anaokoa, Ukimwamini Leo Wewe Mwenye Magunia Ya Dhambi Unaokoka.
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani.
ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana
Ni mimi ndugu yako katika BWANA YESU.
Peter M Mabula
Maisha ya ushindi Ministry.
0714252292
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments