HISTORIA YA ASKOFU ZACHARIA KAKOBE(2)

Askofu Zakaria Kakobe akifundisha huko Kinshasa Kongo

Muujiza wa pili ulitokea katika mkutano niliufanya katika kijiji cha Chalinze, mkoani Pwani, mwishoni mwa mwezi Januari 1989; ulikuwa umefadhiliwa na Elim Pentecostal Church. Hapo, pia wanakijiji walikuwa wagumu kuingia kwenye mkutano kwa sababu hawakuamini katika miujiza. Katika siku ya kwanza ya mkutano, walikuwepo watu wachache sana mkutanoni. Wengi wa waliohudhulia, walikuja katika makundi, wakiambatana na mwanamke aliyekuwa bubu wa aina yake.Si tuu kwamba hakuweza kuongea hata neno moja kwa miaka mitatu, lakini pia kwa kipindi chote hicho, aliwika kama jogoo kila baada ya masaa matatu hadi manne. Kila mwanakijiji alimjua mama huyo kwa sababu ya aina yake ya kipekee ya ububu. Sayansi ya kitabibu haikuweza kuelezea kivipi mwanadamu angeweza kuwika kama jogoo! Watu waliniambia, “Mhubiri, kama maombi kwa Jina la Yesu yanaweza kumfanya mama huyu aongee, na kuacha kuwika, basi tutaamini mahubiri yako na kumfuata Yesu wako.”

Nikawaambia, “Nendeni mitaani mkawaalike watu wengi kadri muwezavyo, waje waone muujiza huu. Baada ya ombi fupi, ataongea kama kawaida, na kuwika kutamtoka.” Walikwenda mitaani na bila kitambo kupita hata kidogo, viwanja vilifulika mamia ya watu waliokuwa na shauku ya kuuona muujiza. Unajua nini! Baada ya ombi fupi, mama aliongea kawaida, na hapakuwa na kuwika tena. Masaa manne yalipita, na hapakuwa na dalili za kuwika. Wakamuangalia tena usiku wote na kwamshangao wa kila mtu, kuwika kulikuwa historia! Siku iliyofuata, karibu kijiji kizima, kilivutwa kweye viwanja vya mkutano, na mamia ya watu wakayakabidhi maisha yao kwa Yesu. Hii iliendelea kila siku, hadi siku ya mwisho ya mkutano; na muujiza huu pia uligeuka kuwa mada ya kijiji kwa miaka kadhaa baada ya mkutano.

Mkutano wa mwisho wa Kakobe, kati ya ile kumi, ulifanyika Kanisa la Pentekeste Kijitonyama Dar es Salaam. Hiyo ilikuwa ni mwishoni mwa mwezi wa Pili, mwaka 1989. Baada ya mkutano huu, alitenga muda kuwasiliana na wachungaji wenyeji wake katika mikutano yote kumi , ili kujua kama, kama ufuatiliaji mzito wa kina unahijika kwa waamini wote wapya walioamua kumfuata Yesu, katika mikutano hii, na kama imefanywa kisawasawa baada ya mikutano. Nia yake, tangu mwanzo, haikuwa tuu kuleta matunda katika mikutano, lakini kuhakisha kwamba matunda yake yalidumu; kwa sababu iliamini moyoni mwake kwamba yale ndiyo yalikuwa mapenzi ya (Yohana 15:16; 1 Wathesalonike3:5,8). Katika tathimini ya kazi iliyofanywa, aligundua kwa kuvunjika moyo, kwamba wengi wa wachungaji wenyeji wake hawakuwa wamechukua hatua madhubuti kuwafuatilia waamini wapya. Kwa namna flani walichukulia mikutano ya miujiza ya uponyaji, kama aina ya burudani tuu. Tena, baadhi yao walienda likizo mara tu baada ya mikutano. Tathimini hii ilimfanya Kakobe kuutafuta uso wa Mungu kisawasawa, na kumuuliza kama aendelee na mwelekeo huo, au vinginevyo. Baada ya kuomba kwa takribani mwezi mmoja na nusu, Bwana alimueleleza wazi wazi kuanzisha Kanisa, Full Gospel Bible Fellowship; ili aweze kuenda na kuleta matunda, na kuhakikisha kwamba matunda yanadumu.

Katikati ya mwezi wa Nne 1989,  aliwakusanya waumini vijana 13 na kuweka kambi nyumbani kwake Kijitonyama, Dar-Es-Salaam; kwa wiki mbili za kozi ya usomaji wa kina wa Biblia. Baada ya hapo, Jumapili ya tarehe 30, mwezi wa Nne, 1989, alianzisha huduma yake ya Kanisa akiwa na waumini 13, katika shule ya msingi ya Jamhuri, eneo la Mnazi Mmoja, Dar-Es-Salaam. Hivyo Neno la Bwana aliloambiwa Kakobe likatimilika. Sasa Kakobe alikuwa mchungaji, na mengi yalikuwa yanakuja! Akilini mwake akiwa pia na mafundisho ya wachungaji, miezi michache baadae, alianzisha darasa lake la Biblia kuelekea wito asili.

Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (F.G.B.F), Dar es Salaam, Tanzania.

Toka katika mwanzo huo duni , hadi sasa, Kakobe anachunga kanisa Kubwa sana Dar-Es-Salaam, ambalo ni kanisa mama na amewafundisha yeye mwenyewe na kuwatuma kwenye mashamba ya Bwana zaidi ya wachungaji 700.Jumapili, tarehe 7 Machi, 1993; aliwatawadha kundi la kwanza la wachungaji 28 (Wachungaji 19 na Wachungaji Wasaidizi 9); na kuwapa mamlaka ya kufungua makanisa tanzu ya kwanza 19 (au makanisa mtoto), katika makao makuu ya mikoa yote 19 iliyokuwepo Tanzania bara enzi hizo; na Februari 2000, Kakobe tayari Kakobe alikuwa amesha anzisha zaidi ya Makanisa tanzu 400 (au Makanisa mtoo) yaliyo tapakaa mikoa na wilaya zote za Tanzania bara.

Kanisa La Full Gospel Bible Fellowship (F.G.B.F), Dar es Salaam; Huduma ya Ibada ya Jumapili.

Nini siri ya kazi hii nzuri?Ishara na maajabu ndani ya huduma ya Kakobe, bila ya shaka imefanya kazi kubwa katika kushusha vifungo vizito na kuondoa vitu vyote vikubwa vinapingana na elimu ya Mungu, Tanzania; ardhi yenye asilimia nzuri ya waislamu. Kwa maneno yake mwenyewe, Askofu Kakobe anaelezea,"Mshindi wa roho, ni mvuvi wa wanadamu (Mathayo 4:18-19). Sisi ni wavuvi wa wanadamu. Katika uvuvi, mvuvi atatumia chambo, kufunika chembe na ncha za ndoano.Wavuvi hutumia wadudu, au dagaa, kama chambo, itakayovutia samaki. Wakati samaki anaposhawishika kwenda kugh’ata chambo, anajifuma mwenyewe kwenye ndoano ambayo imeshikizwa kwenye uzi wa ufito wa kuvulia samaki na hivyo hunaswa na mvuvi. Mvuvi hawezi kutumia ndoano isiyo na chambo na ategee matoke yanayovutia. Samaki wataikimbia ndoano isiyo na chambo. Kwa namna ile ile, Injilini kali kuliko upanga wenye makali kote kote. Ni kama ndoano. Mvuvi wa watu anaweza kukamata watu kirahisi kama atatumia “chambo samaki” au “chambo watu” ukipenda, kwenye “ndoano ya uinjilisti”,  kuwavutia wasioamini kusikia na kuiamini Injili.

Kwa kutumia misingi hii, Kakobe kaendesha mamia ya mikutano ya Miujiza ya Uponyaji ya kanisani na maeneo ya wazi nchini mwake tangu aanzishe Kanisa lake;  na mikutano hii imechangia sana kwenye mafanikio ya Usimikaji wa Kanisa. Kwa mfano, mwaka 2007 pekee, alifanya jumla ya Mikutano ya wazi ya Miujiza ya Uponyaji katika miji na vijiji tofauti tofauti 211; vilivyo tapakaa mikoa na wilaya zote za Tanzania bara, katika mda wa siku 256 tuu; kuanzia Januari 2007 katika Kijiji cha Mlali, Morogoro Vijijini; na kuhitimisha Septemba 17, 2007 katika kijiji cha Ngerengere, huko huko Morogoro Vijijini. Katika baadhi ya siku hizi, alifanya mikutano mitatu kwa siku, katika miji au vijiji vitatu tofauti, mkutano mmoja asubuhi, unaofuata mchana, na wa mwisho jioni; na katika baadhi ya siku alifanya mikutano miwili katika miji au vijiji viwili tofauti, kila siku.

Yote kwa yote, ndani ya muda huo wa siku 256, alifanya mikutano mitatu kila siku wa siku 10, mikutano miwili kila siku kwa siku 53 na mkutano mmoja kwa siku kwa siku 75. Hivyo idadi ya “Siku za Mikutano” kama ukipenda, ilikuwa 138 tuu na siku zilizobaki zilitumika kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, na pia kuchunga kanisa mama, jijini Dar-Es-Salaam. Alifanya mikutano hii si tu katika miji na majiji makubwa, lakini pia katika vijiji vya ndani ndani nchini kote ambako hakukuwa kufanyika mkutano wa injili.Kutoka kijiji cha Mahurunga, wilaya ya Mtwara vijijini Kusini-Mashariki, karibu na mpaka wa Tanzania na Msumbiji (Julai 28, 2007), hadi kijiji cha Wampembe wilaya ya Nkasi upande wa Kusini-Magharibi, katika fukwe za Ziwa Tanganyika (Mei 28, 2007); na kutoka Bwisya, katika kisiwa cha Ukara upande wa Kaskazini-Magharibi (Mei 12, 2007); hadi kijiji cha Duga Maforoni upande wa Kaskazini-Mashariki, karibu na Horohoro, mpakana mwa Tanzania na Kenya (Agosti 16, 2007) na kutoka kijiji cha Kabanga Magharibi mpakani mwa Tanzania na Burundi (Mei 16, 2007); hadi Kilindoni, kisiwa cha Mafia upande wa Mashariki (Juni 28, 2007), na kutoka kijiji cha Njani Marikanda wilayani Arumeru (Machi 26, 2007) na Loliondo (Machi 30, 2007),  zote upande wa Kaskazini; hadi kijiji cha Mpwayungu Wilayani Chamwino, katika ukanda wa kati(Machi 12, 2007); na Tunduru, upande wa Kusini (Julai 30, 2007).

Baada ya kuweka wazi siri zilizomwezesha Kakobe Kusimika huduma yake ya Kanisa, sasa tuende hatua moja mbele. Baada ya kutawaza kundi la jingine  la Wachungaji, Jumapili ya Januari 30, 2000; Kakobe alikuwa ametawaliwa na nia ya kufungua makanisa tanzu (mtoto) katika Nchi zingine duniani. Lakini, kabla ya kuendelea, aliamua kumuuliza Bwana kama nia yake ilikuwa sambamba na mapenzi ya Bwana kwenye huduma yake kwa wakati ule.

Baada ya kuomba kikamilifu, Bwana alimueleza wazi wazi kutofanya hivyo. Alimkumbusha wito wake kuhubiri injili kwa makundi makubwa ya watu, katika matifa mengi duniani, kwa ishara na maajabu makuu. Pia alikumbushwa kwamba, wakati anatonywa mwaka 1982, kazi hiyo ilipaswa kutekelezwa “miaka ya baadae” katika huduma yake.Bwana pia alimpa mpango mkakati wa utekelezaji wa kazi hiyo. Alisema kwamba, atakapo kwenda kuhubiri kwa Mataifa, atakuwa anafanya kazi kwa kushirikiana na Global Body of Christ; akiwezesha, akitayarisha na kutegemeza makanisa asilia (local) kutimiza majukumu yake. Pamoja na hayo, Bwana alisema kwamba lazima apitie katika mafunzo makali mpaka miaka ya baadae; atakapoachiliwa kiujumla kufanya huduma ya namna hiyo. Alimwambia kwamba kabla ya wakati huo, ataendelewa kuachiliwa kwa nyakati kuhudumu kimataifa, na kisha kurudi kwenye mafunzo; mpaka muda ulioteuliwa.Bwana alihitimisha kwa kumsihi kukumbuka daima kwamba, kwenye utumishi inaamuliwa, kwamba mteule awe mwaminifu daima.

Jibu hili kwa maombi yake, lilimfanya Kakobe akumbuke kilichotokea miaka kadhaa nyuma, ya kwamba, mwaka 1996 baada ya Mkutano wake wa kwanza wa kimataifa wa Miujiza ya Uponyaji katika Jiji la Pune, nchini India; na mda mfupi kabla ya jibu la maombi yake, ambayo in mwaka 1999, baada ya Mkutano wa Miujiza ya Uponyaji katika Jiji la Kandy, Sri Lanka; na katika makazi duni ya Mathare  jijini Nairobi, nchini Kenya. Idadi kubwa ya kumpokea Yesu na ishara na maajabu halisi yasiyo idadi na yenye kustajabisha katika mikutano hiyo, viliacha alama katika historia ya Mikutano ya Miujiza ya Uponyaji katika majiji hayo. Matukeo yake, kila moja ya Mikutano hii ilifungua milango mingi ya kuhudumu Kimataifa, lakini Kakobe, alipomuuliza Bwana juu ya kuendelea mbele, Roho hakumruhusu (Matendo ya Mitume 16:6-7).Sasa ilikuwa imedhihirika wazi kwamba, wakati ulioamuliwa , ulikuwa haujawadia. Kakobe alikuwa bado yuko msitu wa giza, akiandaliwa na kufundishwa na Mungu, katika nchi yake asilia, Tanzania, na hata Mikutano michache ya Kimataifa ya Miujiza ya Uponyaji iliyo ruhusiwa, ilikuwa pia, sehemu ya mafunzo

Tangu mwaka 2000, wakati Askofu Kakoba alipopokea toka kwa Bwana, miongozo kwa kuhudumu kwake Kimataia, Mungu ameendelea kumuachia mara kadhaa kuhudumu kimataifa, lakini matokeo ya Mikutano yake ya Kimataifa ya Miujiza ya Uponyaji, yamekuwa makubwa.Mwaka 2006; Mkutano ya wake wa Miujiza ya Uponyaji nchini Korea iliwashangaza waandaji wa mkutano, the Korea Revival Mission. Walisema, “Hatujawahi kuona kitu kama hiki kabla” Mwaka 2008; kwa siku sita tuu, huduma yake iliitikisha nchi nzima ya Burundi; na kila sehemu, mazungumzo yalikuwa ni kuhusu Yesu Kristo! Vivyohivyo, mwezi wa tano mwaka 2010, Mkutano wake wa kihistoria wa Miujiza ya Uponyaji katika Jiji la Lubumbashi, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ililishika Jiji zima na miji ya jirani, na Yesu Kristo alikuwa hai na halisi kwa wenye mashaka.Sawia, Agosti 2010, Mkutano wake wa siku tano wa Miujiza ya Uponyaji huko Lusaka, nchini Zambia, pia ilimfanya Yesu Kristo kuwa gumzo la Jiji na nchi nzima kwa ujumla.

Askofu Kakobe na Mkewe, Hellen

Na sasa, hatimaye! Habari za faraja zilizosubiriwakwa mda mrefu zimewasili!Hatimaye wakati ulioamuliwa umetimia! Ilianza mwaka 2010, kwa Uongozi wa Roho Mtakatifu, wakati Bishop Zachary Kakobe International Ministries ilisajiriwa nchini Marekani. Kisha baada ya kukaa katika maombi marefu tarehe 16 mwezi wan ne, 2012; miaka 30 baada ya wito wake kuhuduma, Askofu Kakobe hatimaye alitamka, " Kwa Neema ya Mungu, Leo, Nimeruhusiwa kabisa na Roho Mtakatifu Kuhudumu Kimataifa. Miaka ya baadae sasa imewadia!"Ndio! Askofu Zakaria Kakobe yuko hapa, akimtumikia Bwana wa Mavuno kama chombo cha ufufuo kwa Mataifa. Nia yake kubwa ni kuja Jijini kwako Duniani kwa kazi moja tu; kuliinua Jina la Yesu juu, na juu zaidi! Kwa Mungu, na Baba yetu, utukufu una yeye milele na milele, Amina (Wagalatia 1:4-5).

Askofu Zakaria Kakobe ni mme wa mke mmoja, Hellen. Walioana Desemba 11, 1979; na kwa pamoja wana watoto wanne.

BWANA YESU asifiwe Mwana Maisha ya ushindi mwenzangu. Kuanzia leo nakuletea Historia ya kuvutia sana ya huduma ya Askofu Mkuu wa FGBF Zacharia Kakobe, Nimependa sana kukushirikisha na wewe maana kihuduma kanisa hilo mwaka huu wameadhimisha miaka 25 ya huduma tangu lianzishwe Mwaka 1989, usikose hapa hapa hapa Maisha ya ushindi blog. Karibu san

Copy n Win at: http://bit.ly/copyandwin
BWANA YESU asifiwe Mwana Maisha ya ushindi mwenzangu. Kuanzia leo nakuletea Historia ya kuvutia sana ya huduma ya Askofu Mkuu wa FGBF Zacharia Kakobe, Nimependa sana kukushirikisha na wewe maana kihuduma kanisa hilo mwaka huu wameadhimisha miaka 25 ya huduma tangu lianzishwe Mwaka 1989, usikose hapa hapa hapa Maisha ya ushindi blog. Karibu sana

Comments