YESU KRISTO NI MWANAKONDOO WA MUNGU AONDOAYE DHAMBI ZA ULIMWENGU.

.BWANA YESU asifiwe
Karibu tujifunze mambo ya uzima.
'' Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako. -Isaya 43:25''
Kwa Upendo Wa Ajabu Sana BWANA YESU Alitoa Maisha Yake Kuniokoka Mimi Na Wewe Kutoka Dhambini, Kifo Chake Na Kumwagiga Damu Yake Isiyo Na Hatia Ilikuwa Ni Sadaka Ya Kuchukua Dhambi Zetu. 
Katika Waebrania 9:22 Tunasoma Kwamba YESU Asingemwaga Damu Yake Tusingepata Ondoleo La Dhambi. YESU Alikuwa Kafara Ya Kweli Kwa Sababu Hakuwa Na Dhambi. Katika Yohana 1:29 Tunaambiwa Kwamba "Huyu Ndiye Mwanakondoo Wa MUNGU Aondoaye Dhambi Ya Ulimwengu.". 

Hakuna Mwingine Yeyote Ambaye Angekufa Msalabani Ili Kuziondoa Dhambi Zetu, Pesa, Wanyama Wala Vitu Haviwezi Kuwatakasa Wanadamu Ila Damu Ya YESU KRISTO. 1 Petro 1:18-19 Biblia Inasema " Maana Mnajua Kwamba Ninyi Mlikombolewa Katika Mwenendo Wenu Usiofaa Ambao Mliupokea Kutoka Kwa Wazee Wenu, Si Kwa Vitu Vya Kuharibika; Kwa Fedha Na Dhahabu Bali Mlikombolewa Kwa Damu Tukufu Ya KRISTO, Ambaye Alikuwa Kama Mwanakondoo Asiye Na Dosari Wala Doa."  
Ndugu Zangu, MUNGU Alituthamini Sana Kwa Kutuletea YESU Ili Tupate Uzima Wa Milele Bure, Ndugu Hakikisha Unapata Uzima Wa Milele.
 ''Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na MUNGU huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.1 Yohana 5:4''


 BWANA YESU Alitoa Maisha Yake Bure. 
Yeye Anasema Katika Yohana 10:18 Kwamba "Hakuna Mtu Anayeninyang'anya Maisha Yangu; Mimi Nayatoa Kwa Hiari Yangu Mwenyewe. Ninao Uwezo Wa Kuyatoa Na Uwezo Wa Kuyachukua Tena. Hivi Ndivyo BABA Alivyoniamuru Kufanya. " 
 Ndugu Zangu, 
YESU Ana Uwezo Wote Alitoa Maisha Yake Kwa Ajili Ya Watu Wa Mataifa Yote Ili Kwamba Wote Wamwamini Na Kuokolewa. Ni Heri Ndugu Uhakikishe Kwamba Wewe Ni Mmoja Wa Wale Waliookolewa Na BWANA YESU. Ufunuo 5:9 Inasema "Basi Wakaimba Wimbo Huu Mpya, Wewe Unastahili Kukitwaa Hicho Kitabu Na Kuivunja Mihuri Yake. Kwa Sababu Wewe Umechinjwa, Na Kwa Damu Yako Umemnunulia MUNGU Watu Kutoka Kila Kabila, Lugha, Jamaa Na Taifa.". 

 Ndugu Zangu, 
YESU KRISTO Anatupenda Sana, Anataka Wewe Unayesoma Ujumbe Huu Uende Uzima Wa Milele, Mpokee Tu BWANA YESU Leo Ili Jina Lako Liandikwe Kwenye Kitabu Cha Uzima Mbinguni. Ubarikiwe Sana Wewe Unayependwa Sana Na BWANA YESU. Simama Kwa BWANA, Songa Mbele Kwa BWANA, Mche BWANA Na Mtii BWANA.
YESU anasema ''Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.-Yohana 15:4''
Watu wengi wanamkataa YESU kwa sababu tu ya kutekwa na shetani au kuwafuata wazazi ambao wala hawana mbingu ya kuwapeleka lakini napenda kusema neno hili kwamba 
 '' Sio Lazima Kumpa YESU Maisha Yako Ila Haiwezekani Kuingia Uzima Wa Milele Kama Huna YESU.''
 ''Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa. -Mithali 29:23''
Parapanda Italia, Kila Mtu Atalipwa Kama Matendo Yake Yalivyokuwa, Waliokataa YESU Siku Hiyo Watamkubali Lakini Watakuwa Wamechelewa.BWANA YESU Atawapeleka Uzima Wa Milele Wateule Wake Na Watakaobaki Wataenda Kwao Jehanamu. Ndugu Unasubiri Nini Kuokoka?
''Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa Bwana; Hakika, hatakosa adhabu. -Mithali 16:5''

Kuna watu ambao wana majina la kuwa hai lakini wamekufa. pia kuna wenye majina ya kuwa wakristo lakini vitendo vyao ni dhambi mbele za MUNGU aliye hai.
Jifunze kitu hapa chini.

 UNAWAJUA WAKRISTO JINA?

- Wanamiliki Bar Na Kanisani Wanaenda,
-Ni Wachawi Na Wanahudhuria Ibada,
-Wanawachukia Watu Na Kanisani Wanaenda,
-Ni Wazinzi Wanafanya Kanisa Sehemu Ya Kufichia Maovu Yao,
-Wanaukataa Wokovu Wa YESU,
-Wanaabudu Sanamu,
-Wameweka Matumaini Yao Kwa Watu Badala Ya BWANA YESU,
-Hawataki Mahubiri,
-Hawamtii KRISTO,
-Wanamwabudu MUNGU Kwa Midomo Yao Huku Mioyo Yao Iko Mbali Nae,
-Sio Waombaji,
-Hushika baadhi tu ya Sheria za MUNGU na zingine wanaziacha

 -Mwongozo Wao Sio Biblia Ila Ni Vitabu Walivyojitungia Wao,
-Wanaombea Wafu,
-Hawamtaki ROHO MTAKATIFU,
-Huenda Kanisani Jumamosi Au Jumapili Tu,
-Wakitoa Sadaka Hudhani Wanamtolea Mchungaji Na Sio MUNGU,
- Husema Uongo Hadharani,
-Hudhani Kwamba Watakaoenda Mbinguni Ni Dhehebu Lao Tu,
-Hudhani YESU Ni Malaika Tu Mwenye Cheo,
-Huchukia Semina Na Mikutano Ya Injili
-Na Hawana Hofu Ya MUNGU.

Ndugu Zangu Mtume Paulo Anasema juu ya watu kama hawa kwamba ''Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao YESU KRISTO aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili?- Wagalatia 3:1,3 ".  
BWANA YESU Anasema  anawaambia watu hawa kwamba   ''Imeandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.-Mathayo 21:13''

 Ndugu ni hatari sana kuwa mkristo jina tu, ndugu  huwezi kuokoka roho harafu nafsi ikawa haijaokoka.
Kama wewe ni mkristo jina badilika leo na uwe Mkristo aliye hai, mwenye hofu ya MUNGU, Mwenye nguvu za ROHO MTAKATIFU, unaongozwa kwa ROHO  MTAKATIFU na tena hutazamii tamaa za mwilini. 
''Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu. -Isaya 62:2''

Kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisha kanisani.
ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana
Ni mimi ndugu yako katika BWANA YESU.
Peter M Mabula
Maisha ya ushindi Ministry.
0714252292
Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments