ALIYEACHA MKEWE NA KUOA MKE MWINGINE ANAZINI PIA MWANAMKE ALIYEACHA MUME NA KUOLEWA NA MUME MWINGINE ANAZINI (LUKA 16:18)



KWA YESU HAKUNA TALAKA KWA KISINGIZIO CHOCHOTE
Nyakati tunazoishi ni nyakati za hatari Maandiko yanasema kutakuwa na Waalimu wa UONGO>2PETRO 2:1-3. Waalimu hawa wa uongo ni wale ambao watakuwa wanatafuta tu kipato hivyo watageuza injili ya Yesu kuwa kitegauchumi chao, Kumekuwa na wimbi kubwa sana la watu kufunga ndoa za bandia ndoa za HARAMU ambazo Yesu alizikemea sana tangia wakati wa mwili wake hata alipopaa mbinguni na baadae kushuka Roho mtakatifu bado alikemea sana vitendo hivyo, na hii ni kwasababu Ndoa sikitu cha kimwili tu kama watu wadhaniavyo no bali ni tendo la kiroho pia, ambalo linaunganishwa katika tendo la ndoa, kuungana na kuwa mwili mmoja hutokana na lile tendo lenyewe la ndoa ndilo huwaunganisha watu na kuwa mwili mmoja.

Roho mtakatifu ananena kwa kinywa cha Apostle Poul kwamba YEYE ALIYEUNGWA NA KAHABA NI MWILI MMOJA NAYE MAANA IMEANDIKWA HAWA WAWILI WATAKUWA MWILI MMOJA>1KORINTHO 6:16. Hii inamaanisha kwamba kila watu wanapoingiliana kimwili wanakuwa ni mwili mmoja, Kuna muunganiko kuna mnyororo unaowaunganisha kwenye ulimwengu wa roho na ule mnyororo unazidi kuenea kwa kadiri ya mtu anavyokuwa malaya hivyo mtu mmoja anweza kuunganishwa na watu zaidi ya 1000 pasipo yeye kujua, mfano mtu anapokutana kimwili na mwanamke kisha yuke mwanamke akaenda kukutana kimwili na mwanaume mwingine hii inawaunganisha hawa wanaume wawili kwa kupitia mwanamke mmoja na hii ni njia pekee sana ambayo Shetani anaitumia kupitishia maroho yake ya uchafu kwaa jamii kubwa ya watu kupitia zinaa,

Mtu anapofunga ndoa na mwanamke wa kwanza au hata kama hawajafunga ndoa ila tu kama wameishi miaka kadhaa na kufanikiwa kuzaa watoto na wazazi wa mwanamke wakaridhia hilo na kutambua binti yao anaishi na mtu fulani kama mume na mke watu wa jinsi hiyo Mungu anawahesabu kuwa ni mke na Mume na hawaruhusiwi kuachana kwa sababu yoyote ile, ndoa ni makubaliano ya watu wawili waliyopendana haijalishi itakuwa imefungiwa wapi kanisani au kwa mganga wa kienyeji endapo tu watu hawa wamekubaliana basi na wazazi au walezi wa mwanamke wakamkabidhi binti yao kwa mwanaume huyo na katoa mahari hiyo ni ndoa na Mungu anaitambua sema tu haina ulinzi wa Mungu maana haijabarikiwa na Mungu kwasabu watu wakiisha kupatana kwa lolote Mungu huwa katikati ya hilo na maandiko yanasema mtu akilala na binti wa ntu sharti akamtolee mahari kwao. Wanaume tumekuwa waonevu sana tunatumia nguvu na maumbile yetu kuwaonea wanawake unakuta mtu wameishi miaka mingi na mkewe amemzalisha watoto wa nne eti leo anamwacha kisa ameokoka maana anajua kabisa kuwa huyu mama hawezi kuolewa tena ila mimi mwanaume naweza kuoa Mungu ameruhusu tu kutengana endapo mke mwenyewe ataamua kuondoka kutokana na sababu za kiimani na anapoondoka huyu mume haruhusiwi kuoa tena mpaka huyu mwanamke afe lakini mtu anapookoka kama alikuwa anaishi na mwanamke kienyeji hatakiwi kumwacha bali anapaswa kwenda kwao kumtolea mahari na kubariki ndoa madhabahuni, kitendo cha kumwacha ni uonevu na niuzinzi maana huyu umeshaungana naye tayari kwa tendo la ndoa.

UBISHANI WA VIONGOZI WA KIDINI NA YESU JUU YA TALAKA
Baadhi ya Mashekhe Mapadre na Ustandhi na wachungaji vipofu, walimfwata Yesu na kumwambia kwamba Musa aliruhusu kutoa hati ya Talaka, Lakini Yesu aanwajibu kwa kusema Musa aliruhusu kwasababu ya ugumu wa mioyo yenu lakini tangu mwanzo haikuwa hivi>MAHTAYO 19:7-8. Sasa hwa wazee na makanzu na majoho yao huku wamejaa ndevu videvuni mwao walimkuwa ndani ya miyoyao wanamchukulia mwanamke ni kama chombo tu cha kukidhi haja na kukitupilia mbali lakini, lakini siku zote ili ujue thamani ya mwanamke ni lazima urudi mwanzo ndipo Yesu akawaambia Hamkusoma tangu mwanzo?>MATHAYO 19:4. Yesu aliwarudisha mwanzo kisha akasema tena, Kilichounganishwa na Mungu mwanadamu asikitenganishe, sasa happa ndipo pana tafasiriwa vibaya kuna watumishi wanadanganya watu kwamba eti ndoa ambayo haijafungiwa kabisani haijaunganishwa na Mungu hivyo inaweza kuvunjwa HUU NI UONGO WA MCHANA KWEUPE kwasabu Yesu hapa anafafanua vizuuri sana ili kutuelewesha nini maana ya kuunganishwa na Mungu,

Kuunganishwa na Mungu siyo madhabahuni no bali ni lile tendo alililiasisi Mungu mwenyewe tangu mwanzo na ndiyo maana Adamu hakufungishiwa madhababhuni wala baba yetu wa imani mzee Ibrahimu hakufungishiwa ndoa madhabahuni tena alioa kwa desturi za kimila za kwao kwa baba yake mzee Tera lakini pamoja na hayo Mungu aliitambua ndoa ya Ibrahimu hii ndiyo sababu alimsahihisha Ibrahimu sehemu zote lakini kamwe hakuwahi kumsahihisha eneo la ndoa yake maana ilikuwa ni ndoa halali japokuwa imefungiwa kwa miungu ya Tera, sasa kuunganishwa na Mungu ni kufuata ile misingi ya kiungu ambayo ni mapatano ya wawili waliyopendana na hakuna aliyelazimishwa kila mmoja amekubali kwa moyo wake wote na mahari ikatolewa na baada ya hayo tendo la ndoa likafanyika hapo tayari wameunganishwa na hakuna chochote kinachoweza kuwatenganisha tena JEHOVA anasema NAKUCHUKIA KUACHANA.>MALAKI 2:16. Pia Mungu amekataza kabisa mke asiachane na mumewe na mume asiachane na mkewe na endapo wataachana na wakae vivyo hivyo bila kuoa wala kuolewa>1KORINTHO 7:10-11.

UKWELI KUHUSU KOSA LA UASHERATI
Kumekuwa na fundisho linalosema mtu anaruhusiwa kumwacha mkewe kwa kosa la uasherati na wananukuu andiko la>MATHAYO 5:31. Sasa leo nataka tulichambue tujue ukweli kuhusu uasherati. kwanza kabisa uasherati siyo uzinzi na uasherati hauwahusu watu waliyokwisha kuoana, uasherati unawahusu watu waliyokutana kimwili kinyume na ile misingi ya ndoa yani makubaliano ya kuishi pamoja huku wazazi wakipewa mahari yao na kumkabidhi binti kwa mume, uasherati unhusu watu ambao wanakutana kimwili kwa lengo tu la kuridhishana miili yao kama vile Garlfrind na Boyfriend wafanyavyo MAUCHAFU HAYO yanayotia kichefuchefu.

Kwenye biblia hakuna uchumba bali kuna mke na mume, yani kibiblia mtu anapomposa mwanamke ili ajekumwoa na mwanamke huyo kukubali kuposwa na wazazi wake kumkubalia mwamume huyo kumwoa mtoto wao hapo anaitwa ni mkewe hii ndiyo kibiblia hapa sizungumzii kidini au kiththebu kulingana na mafundisho ya mapokeo tuliyoyarithi kwa babazetu wa kiroho, ukiisha kumchumbia mwanamke na kukubaliwa huyo anaitwa ni mkeo ijapo bado huna ruhusa ya kulala naye yani kufanya naye tendo la ndoa.mpaka pale utakapoleta mahari ya watu na kukabidhiwa na wazazi wake na kuapata baraka zao,

Nyakati za biblia destuli ya wayahudi ilikuwa mtu akiisha kumposa mke huyu mke anawekwa ndani miezi tisa na katika miezi hiyo tisa haruhusiwa kuonana na mwanaume yoyote hata kaka yake harurusiwi kuonana naye zaidi ya mama na dadazake na wanawake wenziwe na kipindi hiki mwanaume pekee anayeruhusiwa kumuona ni huyo mposaji tu tena anapoenda kuonana naye anaingia chumba hiko huku mlango ukiwa wazi na mama mzazi wa binti pamoja na dada wanasimama mlangoni huku wakilinda kusudi sije watu hawa wakakutana kimwili, sasa kipindi hiki huyu Mume anakuwa kila baada ya siku 40 anaenda kumkagua mkewe aliyemposa kuwa je hana mimba maana mimba yoyote ile ndani ya miezi 9 ni lazima itaonekana na ikionekana tu anatolewa nje na kupigwa mawe hata kufa, sasa katika kipindi hiki ndiyo hata Yusufu alitambua kuwa kumbe Mkewe mtarajiwa anamimba, hiki ndiyo kilikuwa kile kipindi cha ile miezi9 cha kukaguliwa. umeona Yusufu aliambiwa na Malaika kwamba Usiache kumchukua Mariamu MKEO>MATHAYO 1:2. hapa tunaona anaitwa ni mkewe ijapo bado hawajafunga ndoa rasmi sasa hapa ndiyo biblia inaruhusu kumwacha na hili ndilo kosa la uasherati linalotajwa na haliwahusu watu ambao wameshafungandoa na kukutana kimwili hapa haliwahusu kabisaaa watu waliyokwisha kufungandoa hapa wanazungumziwa watu ambao bado wapo katika uchumba sasa mmoja akamfumania mwenzie ni pale mchumba mmoja anapothibitisha kwamba mweniwe siyo mwaminifu hapa ndipo Mungu anaruhusu kuachana.

lakini kwa upande wa wanadoa ambao tayari wameshafungandoa rasmi pindi wanaposalitiana wanapaswa kusamehena tu na kama wasiposameheana hata Mungu naye kamwe hawasamehi dhambi zao>MTHAYO 7:14-15. Na mtu yeyote aliyemwacha mekewe au mumewe kisa alimfumania mtu huyo mbinguni haendi kamwe kamwe kamwe maana kusamehe ni amri na yesu amesema mkinipenda mtazishika amri zangu. kwasabu Mungu ameagiza kusamehe saba mara sabini na yani hata mke au mume anapokosa mara saba kwa siku Mungu anaagiza asamehewe hata akitoka nje ya ndoa mara 490 kwa siku ni lazima asamehewe hilo ndilo agizo la Bwana asikufiche mtu njia ile ni nyembamba ni wachache sana wanaoiona sijui kama na wewe ni mmoja wao, ndiyomaana hata Mtume wenyewe walipomsikia Yesu akisema injili hii wakasema kama ni hivyo ni bora kuishi pasipo kuoa>MATHAYO 19:10. NA Yesu aliposikia hivyo akasema hivi SIWOTE WAWEZAO KULIPOKEA NENO HILI ILA NI WALE WALIYOJAALIWA TU>MATHAYO 19:11. Haya maneno sijui kama wewe, mwenzangu unayachukuliaje? sijui kama na wewe umejaaliwa na kama hujajaaliwa kuwa towashi basi ujue hakika ya kwamba kama unataka kuingia kwenye ndoa basi ujue hakika ukweli ni huu hakuna kuachana kwa kisingizio chochote.

WACHUNGAJI WAZINZI
Leo kuna watu wengi wanaitwa wachungaji ambao wanaishi kwenye ndoa haramu, ndoa feck walishawaacha wake za ujana wao na sasa wanaishi maisha ya uzinzi, Tu wakawaida Na kibaya zaidi wanawafundisha na watu mandisho ya uongo juu ya kuoa na kuacha nisikilize mwana wa Mungu kama unafwata maneno ya wachungaji waliyokwishajifia kiroho zamaani shauri yako lakini mimi nakwambia HAKUNA MCHUNGAJI MWENYE MBINGU bali mbingu ni ya Bwana sasa yeye ameshasema kunawatakaosema Bwana Tulitoa pepo na kufanya mengi na kula mezani pako, lakini yeye atawajibu na jusema ONDOKENI KWANGU SIKUWAJUA NINYI KAMWE. mwana wa Mungu sijui kama unampangogani na roro yako, na wewe mchungaji ACHA MARAMOJA kudanganya watu kama umeamua kuishi maisha ya uzinzi ishi mwenyewe usidanganye na wengine. Mungu siyo mjomba wala Shangazi narudia kwa herufi kubwa HAKUNA KUACHANA KATIKA UKRISTO Mwenye masikio asikie

YANGU NI HAYO TU,

ZIDI KUBARIKIWA

Comments