![]() |
Flora Mbasha |
Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili
nchini Tanzania,Flora Mbasha,amekwenda katika mahakama ya hakimu Mkazi
Kisutu jijini Dar-Es-Salaam,akiomba kuvunjwa kwa ndoa yake na mumewe
Emanuel Mbasha.
Flora anadai kuomba kuvunja ndoa hiyo na apewe talaka ni kutokana na tabia ya mumewe kumpiga,kumnyanyasa na kushindwa kumpatia matibabu.
Katika hati hiyo ya madai anaendelea kudai kwamba mgogoro wao waliwahi kuufikisha kwa ustawi wa jamii,kwa ajili ya upatanishi lakini ilishindikana wakashauriwa walifikishe suala lao mahakamani.
Flora anaiomba mahakama itoe talaka,iamuru aendelee kukaa na mtoto,matunzo ya mtoto yatoke kwa mbasha na wagawane mali walizochuma pamoja.
![]() |
Mwimbaji nguli wa nyimbo za injili Flora Mbasha akiwa na mmewe Emmanuel Mbasha (hapa ni siku za nyuma kabla hawajatengana kwa sababu ya Emmanuel kutuhumiwa kubaka mdogo wake Flora) |
Comments