FOMULA YA KUTAWANYA KONDOO NI KUMPIGA MCHUNGAJI

Na Mwinjilisti John Chinyuli.

Je unaijua hii fomula ya kutawanya kondoo ni kumpiga mchungaji(mtumishi) nisikilize vizuri kuna siku pia mwaka jana niliwahi kuandika mahali hapa jumbe yenye maudhui sawa na hii shetani akitaka kutawanya kondoo huwa anapiga mchungaji maana yake ni nini sasa kiundani....
Shetani atafanya juu chini vyovyote vile anavyoweza aharibu na kuchafua shuhuda za watumishi anajua fika kuwa akifanya jambo hili ataondoa imani yako juu ya hao watumishi na kupelekea kutowasikiliza watakachokufundisha na shetani huwa anafanikiwa sana katika hili maana wakristo wengi huwa hawawaombei wachungaji wao na wachungaji wanakutana na mitihani mingi kweli kweli,na akifanikiwa kukuvuruga katika hili amekuweza maana wao ndio waliobebeshwa na Mungu ujumbe wakupona kwako,kuinuliwa kwako,na kukufunulia siri mbalimbali za Mungu kwa kupitia mafundisho yao zitakazo kufanikisha
Nisikilize lengo kubwa la shetani hapa ambacho huwa anataka ni kukuvuluga wewe na sio mchungaji ambaye amekutwa na hayo utakuta mtu anasema kama tu wachungaji wenyewe ndio wanafanya hivi au kama tu watoto wake wenyewe walevi sembuse mimi wakristo wa hivi ni wafinyu wa mawazo utakuta wengine wanawazomea na kuwasema vibaya ili hali kwenye jambo kama hili walitakiwa kuwaombea
Na vita shetani aliyo iinua siyo ya mchungaji bali lengo lake kubwa ni kuwavuluga wao wakristo (lengo la vita ni kuwapiga wakristo) kwahiyo vita inayoinuka kwa mchungaji siyo ya mchungaji ni ya wakristo wenyewe ila shetani anapitia kwa mchungaji wao ili awatawanye ila ukweli kabisa shetani hapa anachokuwa anatafuta ni wakristo tu kuwaangusha na kuwarudisha nyuma wao,Asikiaye na Afahamu..!
Shetani yupo tayali kuandaa nakuwaanda watu watakao sambaza maneno ya uongo kuwahusu watumishi na kupitia uongo huo utakuta ndugu zangu wakristo wanajiundia vigezo butu kwakusema kama tu wachungaji wenyewe wazinzi au walevi au vile na vile watakavyojisemesha sembuse mimi anatumia njia hiyo na nafsini mwake shetani anamdanganya na mwisho kuingia kufanya dhambi sikia sikatai kuwa hakuna watumishi wafanyao haya au sio nawatetea lengo langu nikutazamishe jambo hili kwa picha hii na ndio maana maandiko yako wazi kabisa yanaposema
''Nitampiga mchungaji,na kondoo watatawanyika'' Marko 14:27b
Halafu tu mbali na huko shetani huwa anauwezo wa kumvuruga mtu yoyote yule maadamu tu akamfungulia mlango(akatenda dhambi) na kumtia aibu sana,haijalishi ni mchungaji au ni nani
Kwahiyo kama kweli unataka Mungu akufanikishe,akubariki,akuponye,akuinue na kukutetea amua kuwa na ustaarabu wako na maisha yako wewe na Mungu tu kumbuka pia kila mtu atalichukua fulushi lake halafu siku hizi utumishi umeingiliwa karibia kila fani imeingiliwa,fani zimevamiwa na ambao hawa kuwa wahusika wa hizo fani na kwa kupitia hili na wengine sio watumishi wakweli hawakuitwa walijiita wafanyao kazi ya Mungu kwa ajili ya matumbo yao na kupata sifa na ndio hao badae waangukao dhambini na kulitia aibu kanisa na utumishi kwa ujumla na kuwafanya wengine kurudi nyuma.
Ujumbe kama huu si rahisi kwa watumishi wengi wa Mungu kueleza maana hudhani wakristo watasema anajisafisha,kwa kuwaeleza vita ya shetani anayo iinua kwangu lengo lake ni kuwarudisha nyuma ,kuwaangusha dhambini na kuwatawanya kwa kupitia mimi,leo mimi nimekueleza lolote utakalo sema sema ili mradi mimi nishakueleza kwahiyo hata ukiingia kwenye kufanya uchuro wako uwe wewe tu umeamua na si kusema mbona hata watumishi wenyewe wako hivi,
Mungu akubariki , 

By Mwinjilisti John Chinyuli.
0767592989 / 0712592989

Comments