HERI MWISHO WA NENO KULIKO MWANZO WAKE.

Na Godfrey Miyonjo

MHUBIRI 7:8
BWANA YESU apewe sifa sana,
Wapendwa katika BWANA ninawasalimu katika jina lipitalo majina yote,
Ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kutufikisha siku ya leo tukiwa ndani ya mwezi wa mwisho katika mwaka huu 2014.
Mungu anasema “heri mwisho wa neno” kwa maana ya kwamba Yeye huuangalia mwisho wa kitu, jambo, mtu, n.k,
Mungu haangalii mwaka huu uliuanza vipi, bali anaangalia mwaka huu unaumaliza vipi,

Tunapoelekea kuumaliza mwaka ni vyema kila mmoja wetu angelijua kuwa mwisho huwa kuna heri,
Kwa maana kwamba yale yote yaliyoshindikana ndani ya miezi 11, yanawezekana ndani ya mwezi huu wa mwisho,
Hata kama umeugua kwa miezi 11, mwezi huu wa mwisho ni mwezi wenye heri,

Ni wakati wako wa kumkumbusha Mungu ili atende sawasawa na neno lake,
Huu siyo wakati wa kulalamika na kuwa na hofu ya kufa,
Huu nndiyo wakati wa kuliinua jina la YEHOVA. Wakati wapagani wanaishi kwa wasiwasi wakihofia kutolewa kafara mwisho wa mwaka, wewe mtu wa Mungu mshangilie na kumtukuza BWANA kwakuwa anakwenda kukupatia haja ya moyo wako.

Wapagani wana haki ya kuwa na hofu kwa maana bwana wao naye anakwenda kufunga mahesabu yake mwisho wa mwaka.
Wapagani (wasio na YESU) wana hofu kuu kutokana na dhana kuwa mwisho wa mwaka ni wakati wa ajali za kutisha,
Hii ni dhana ya kishetani kwa maana yeye shetani ndiye hutekeleza uovu (mauaji) mwisho wa mwaka, akitaka kuugeuza ule ukweli wa Mungu kama alivyofanya pale Eden, Rejea MWANZO 3:1,
Shetani kama alivyomdanganya Hawa ndivyo anavyowaaminisha wapagani hivi leo,

MUNGU anataka mwaka huu tuumalize vizuri tukiwa na amani na furaha,
Anataka tuumalize katika kumtii na kumheshimu Yeye,
Asiwepo mmoja wetu mwenye mawazo ya kuumaliza mwaka kwa kumtenda Mungu dhambi, Asiwepo mwenye kuwaza kulewa saana, kufanya uzinzi/uasherati, kuiba/kufanya ujambazi, n.k,

WOTE TUWAZE MEMA, TUTENDE MEMA NA TUISHI KATIKA NEEMA YA YESU KRISTO.

Kama wewe umeishi kwa miezi yote hii 11 ya mwaka huu 2014 pasipo kuwa na YESU (WOKOVU), ni vyema ukaamua kuokoka sasa, ili YESU akuondoe kwenye list ya shetani, usiwe miongoni mwao watakaotolewa kafara ya mwisho wa mwaka.
MUNGU akubariki.
By Geodfrey Miyonjo.

Comments