HIVI UNAJUA KUWA MAJINI (MASHETANI )NI NDUGU ZA WAISLAMU? (JINNIE (EVIL SPIRITS) HAVE SPIRITUAL RELATION WITH MUSLIMS) Sehemu ya kwanza.

Na Mwalimu Daniel Mwankemwa.

UTANGULIZI:
Majini ni viumbe visivyoonekana kwa macho ya kawaida ya wanadamu. Hii ni kwa sababu viumbe hivi viko katika asili ya roho ya kutokuonekana. Majini huitwa pia Ibilisi, Shetani, Pepo mchafu au Joka la zamani.

ASILI YAO:
Majini yalikuwa ni malaika kabla ya kuungana na yule Muasi Mkuu wa Mungu, yaani Lucifer aliyemuasi Mungu mbinguni na kutaka ukubwa wa kufanana na Mungu, na ndipo akatupwa huku duniani yeye pamoja na malaika zake, na huku wakiwa wamenyang’anywa utukufu waliokuwa nao hapo awali. Vita hiyo iliongozwa na Malaika Mkuu wa Mungu wa Mbinguni yaani Jehova kumtupa chini huyo malaika muasi pamoja na malaika zake. Viumbe hivyo vilivyotupwa ndivyo leo vinavyoitwa MAJINI au MASHETANI au PEPO WACHAFU au IBILISI au JOKA LA ZAMANI.

Uf. 12:7-12 “ Kulikuwa na vita mbinguni, Mikael na Malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake, nao hawakushinda, wala mahala pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa yule mkubwa nyoka wa zamani aitwaye Ibilisi na shetani audanganyaye ulimwengu wote, akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. Nikasikia sauti kuu mbinguni ikisema sasa kumekuwa wokovu, na nguvu na ufalme wa Mungu wetu kwa maana ametupwa chini mshtaki wa ndugu zetu yeye awashtakiye mbele za Mungu wetu. Mchana na usiku. Nao wakamshinda kwa damu ya mwanakondoo na kwa neon la ushuhuda wao ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. Kwa hiyo shangilieni enyi mbingu, nanyi mkaao humo. OLE WA NCHI NA BAHARI! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi akijua ya kuwa ana wakati mchache tu”
Hivyo kwa mistari au aya hizo unaanza kupata taswira ya kile tunachijifunza kuliusiana na majini.
Ki- Biblia Malaika ni viumbe walio katika hali ya roho ila wanaweza kuonekana kwa umbile la mwanadamu Mw. 18:1-18, Lk 1:26-28, Kut 3:1-6
Katika Ebr 1:13-14 “ Yuko Malaika aliyemwambia wakati wowote uketi mkono wangu wa kuume hata nitakapowaweka adui zako chini ya nyayo zako? Je, hao si ROHO watumikao wakitumwa kuwahudumia wale watakaourithi wokovu?
Biblia inazidi kubainisha namna ya kuumbwa kwao
Mw. 2:1 “ Basi mbingu na nchi zikamalizika na JESHI LAKE LOTE”

Ni katika jeshi hilo ambapo tunawapata hawa viumbe vya kiroho.
Na katika Kol 1:1:16 “ kwa kuwa katika yeye vitu viliumbwa vilivyoko mbinguni na vilivyo juu ya nchi. Vinavyoonekana na visivyoonekana……”
Jeshi hilo ni huru linaweza kujiamulia lolote na ndiyo maana 1/3 ya hao roho yaani malaika waliasi na kufanya machukizo mbele za Mungu na wakafukuzwa (Uf 12:7-12) na wengine wamefungwa.
Katika Yuda 6 “ Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu amewaweka katika vifungu vya milele chini ya fiza kwa hukumu ya siku ile kuu”
Tunasoma pia katika 2 Petro 2:4
“ Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni akawatia katika vifungu vya giza walindwe hata ije hukumu”

kwa hiyo Majini ndiyo mashetani na mashetani ndiyo majini.Katika kitabu Lawi 17:7
“Wala hawatatoa tena sadaka zao kwa wale MAJINI ambao huwafuata ili wafanye uasherati nao, sheria hii itakuwa sheria ya milele kwao kizazi baada ya kizazi”.
Kwa sababu majini hayo tangu yalipotupwa toka mbinguni wana wa Israel hawakuwa na ufahamu wa kutosha kuyahusu baadhi yao walijikuta wakiyatolea sadaka huku wakiamini kuwa wamemtolea Mungu sadaka. Na kumbuka kuwa mara nyingi wana wa Israel walipotoa sadaka zao nyingi zilikuwa za wanyama na hivyo kutakiwa kuchinja na kutoa damu ambayo ni sehemu kubwa ya chakula cha majini.
Katika Zaburi 106:34-40.
“ Hawakuwaharibu wtu wa nchi kama BWANA alivyowaambia, bali walijichanganya na mataifa wakajifunza matendo yao, wakazitumikia sanamu zao nazo zikawa mtego kwao naam walitoa wana wao na binti zao kuwa dhabihu kwa MASHETANI wakamwaga damu isiyo na hatia, damu ya wana wao na binti zao walio watoa dhabihu kwa sanamu za Kaanani. Nchi ikatiwa unajisi kwa damu.
Ndivyo walivyotiwa uchafu kwa kazi zao, wakafanya uasharati kwa matendo yao. Hasira ya Bwana ikawa juu ya watu wake akauchukua urithi wake.
Hivyo kutokana na kutokuonekana kwao hayo majini yaliwahujumu wana wa Israel hata yakawasababishia wamwasi Mungu kwa kuyatolea sadaka kinyume cha Mungu wa mbinguni aliyehai.
Katika Kumb. 32:17-20.
“ walitoa sadaka kwa Pepo si Mungu, kwa miungu wasioijua, kwa miungu mipya iliyotokea siku zilizo karibu ambayo baba zetu hawakuiogopa,
Humkumbuki muumba aliyekuzaa Mungu aliyekuzaa humkumbuki. Bwana akaona akawachukia kwa sababu ya kukasirishwa na wanawe na binti zake. Akasema nitawaficha uso wangu nitaona mwisho wao utakuwaje maana ni kizazi cha ukaidi mwingi watoto wasio Imani ndani yao.

Pia katika Math 12:43-45
“ Pepo Mchafu amtokapo mtu hupitia mahali pasipo maji akitafuta mahali pa kupumzikia asipate. Halafu husema nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka hata akifa aiona tupu imefagiwa na kupambwa, mara huenda akachukua pamoja naye pepo mengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo, na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza.
Katika Biblia tunaona kipindi Yesu alipotwaa mwili na kuja duniani, hao majini, au mashetani au Ibilisi au Mapepo wachafu yalimfahamu na yalianza kulalamika mbele zake.
Math 8:28-31 “ Naye alipofika ng’ambo katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo (Majini) walikutana naye, wanatoka makaburuni wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile. Na tazama wakapiga kelele wakisema tuna nini nawe mwana wa Mungu? Je, umekuja kututesa kabla ya muhula wetu………………. (MK 5:1-9).
Majini hayo yanafahamu kuwa Yesu ndiye atakayewahukumu ila yalichoshangaa ni kwamba mbona amewahi kabla ya kipindi chenyewe cha yeye Yesu kuyahukumu kwenda Jehanamu ya Moto?
Yesu alikuja duniani ili kumwokoa mwanadamu kutokana na mateso ya hayo majini au mashetani kwa sabahu katika Uf. 12:12 Malaika Mikael alipokuwa anawafukuza hao malaika waasi yaani hao majini au mashetani alisema OLE WA NCHI NA BAHARI ndiyo maana Yesu ilibidi aje duniani kupambana na huyo shetani, Joka, Ibilisi kwa niaba yetu maana sisi tusingeweza na wale, majini walisema kumuambia Yesu ukitutoa tuache tukawaingie nguruwe na ngurume wale wapatao 2000 waliona bora kufa baharini kuliko kuishi na viumbe hivi majini au mashetani miilini mwao na hivyo kutimiza ujumbe wa malaika Mikaeli “ Ole wa nchi na bahari”. Baharini ni sehemu mojawapo ambapo majini huishi.
Unabii wa kuangushwa mji mkubwa uliojisifu sana (Babeli) ulipotolewa, ilitabiriwa kuwa, hayatakuwa tena makazi, bali patabaki yatafanya makazi huko.
Isaya 13:12. lakini huko watalala hayawani wakali wa nyikani na nyumba zao zitajaa bundi, mbuni watakaa huko, na majini atacheza huko.
Ndipo tunaposoma katika Yoh 12:31, Yesu anasema “ sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo, sasa Mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje”.

Itaendeleaaaaaaaaa.



MUNGU akubariki sana.
Anuani yangu ni;

 HUDUMA YA UINJILISTI YA BIBLIA NI JIBU
 S.L.P 45102
 DAR ES SALAAM, TANZANIA.
+255 755 680101
 Email: dmwankemwa@gmail.com

Comments