HIVI UNAJUA KUWA MAJINI (MASHETANI )NI NDUGU ZA WAISLAMU? (JINNIE (EVIL SPIRITS) HAVE SPIRITUAL RELATION WITH MUSLIMS) Sehemu ya pili

 Inaendeleaaaa

Na Mwalimu Daniel Mwankemwa.
Na katika 1 Yoh 3:8
“ atendaye dhambi ni wa Ibilisi kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi mwana wa Mungu alidhihirishwa ili azivunje kazi za Ibilisi.

Kama tulivyosoma toka sura na aya mbalimbali ndani ya Biblia kuwa majini hayo yanasubiri adhabu Biblia inatueleza atakaye yahukumu.
Math 25:31, 41 “ Hapo atakapokuja mwana wa Adamu pamoja malaika watakatifu pamoja naye…………… Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto ondokeni kwangu mliyolaaniwa mwende katika moto wa milele aliyowekewa tayari Ibilisi na malaika zake”.
Hivyo kwa mujibu wa Biblia Majini yaani mashetani ni Adui yetu na ndiyo maana alipokuja Mohammad yalianza kukanusha kuwa Mungu hana mwana ili kuwavuruga waislamu wasiijue kweli (Soma Quran 112:1-4, Al- Kahf, 18:3) ya kumwamini mwana wa Mungu Yesu.
Kwa bahati mbaya sana mambo yahusuyo majini katika imani ya Kiislamu ni tofauti sana na vile tulivyosoma katika Biblia. Ingawa Quran na Hadithi za Muhammed, Mtume wa Waislamu, Vinatutaka sisi wakristo tumwamini allah S.W. mungu anayeabudiwa na Waislamu Misitikini.
Katika Suratul Waqia 51:56.
“ Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu” katika Quran Suratul Al- Ankabut (Buibui), 29:46-47) “ Wala msibishane na watu waliopewa kitabu (kabla yenu) ila kwa yale (majadiliano) yaliyo mazuri isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao na semeni tunaamini yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwenu na Mungu wetu na Mungu wenu ni mmoja nasi ni wenye kunyenyekea kwake”.
Waliopewa kitabu kwa mujibu wa Quran ni Wayahudi na Wakristo. Je, hoja kuwa Mungu wetu na Mungu wao wanayemwabudu kuwa ni mmoja je ni sahihi?. Tuchunguze kuhusiana na mafundisho ya Allah S.W. wa misikitini kuhusu majini ndipo tutajua ni mmoja au la!.
Muislam yeyote ili imani yake ikamilike ni lazima aamini yanayoonekana na yasiyoonekana katika Suratul Al- Baqarah (Ng’ombe Jike la Njano), 2:1-3.
“ Alif Lam Mym. Hiki ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake ni uongozi kwa wamchao mwenyezi Mungu ambao huyaamini yasiyoonekana (maadaam) yamesemwa na mwenyezi Mungu na Mtume wake) husimamisha sala na hutoa katika yale tuliyowapa.
Quran peke yake ukiichunguza utaona kuwa majini yamechukuliwa kama ni viumbe tofauti na mashetani, wanasema hivyo kwa sababu katika uislamu majini yamepewa hadhi kubwa sana na ya kipekee. Hadhi hiyo ni kwa sababu majini waliamini Quaran.
Tusomapo katika Quran Suratul al- Ahqaf, (Kichuguu cha mchanga) 46:29
“ Na (wakumbushe) tulipokuletea kundi la majini (kuja kwako) kusikiliza Quran. Basi walipoihudhuria walisema (kuambiana):- “ Nyamazeni (msikilizeni maneno ya Mwenyezi Mungu)” Na ilipokwisha (Somwa) walirudi kwa jamaa zao wakiwaonya”.
Na ndani ya Quran kuna sura nzima inayoitwa sura ya majini (Mashetani) hiyo ni sura ya 72. katika sura hiyo inasema 72:1-3, 14. “ Sema: imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini liliisikia (Qurani) likasema hakika tumesikia Qurani ya ajabu inaongoza katika uongofu. Kwa hivyo tumeiamini wala hatutamshirikisha yoyote tena na Mola wetu na kwa hakika utukufu wa Mola wetu umetukuka kabisa. Hakujifanyia mke wala mwana……………………. Nasi wamo miongoni mwetu na wamo miongoni mwetu waliokengeuka waliosilimu hao ndiyo waliotafuta uwongofu.
Kwa hiyo aya hizi zinaonyesha kuwa Quran ilipokuja ndipo majini waliposilimu. Kumbuka kuwa Quran imeanza mwaka 610 B.K kipindi ambacho Biblia tayari ili kuwepo kwa karibu karne 6.
Akifafanua asili ya majini Mwanazuoni mkubwa wa kiislamu aitwaye Abdalllah Saleh Farsy aliye kuwa Kadhi Mkuu Zanzibar, kisha akawa Kadhi Mkuu Kenya katika kitabu alichoandika kiitwacho “ Maisha ya Nabii Mohammad” ule Uk. 31 anasema “ Katika safari yake ya kurejea Taif ndipo walipomjia majini wakasilimu kama inavyoonesha haya katika Suratul Jinn. Majini ni viumbe vyepesi vinavyokaa angani. havina viwiliwili kwa hiyo haviwezi kuonekana na wanadamu ila vinapojibadili kwa umbo lenye kiwiliwili. Na vina uwezo huo wa kujibadili kwa sura ya kuweza kuonekana. WAO NA MASHETANI WANA ASILI MOJA. Kwa hiyo asili ya majini ni shetani.
Suala linalohusu malaika linawasumbua sana waislam hata hawana uhakika wake.
Tumesoma ndani ya Biblia kuwa kuna kundi la malaika waliokosa ambao ndiyo wanaoitwa majini lakini tusomapo Quran inatoa maelezo tofauti.
Quran suratul As- Sajdah, (kusujudu) , 32:13 “ Na tungelitaka tungempa kila mtu uwongofu wake (kwa lazima kama tulivyowapa malaika lakini binadamu amepewa huria ya kufanya alitakalo- lililo jema na baya).
Katika ulimwengu wa Kiislamu Malaika wote ni8 wema na wanamwabudu mungu.
Hapa ndiyo tatizo linapoanzia. Quran iliyokuja baadaye inasema malaika wote ni wema wakati biblia kitalu kilichoitangulia Quran kinasema kuna malaika walioasi na wakafukuzwa katika utukufu wa Mungu.
Katika Quran Suratul, al- Kahf, (Pango) 18:50 “ Na (Kumbukeni) tulipowaambia Malaika, Msujudieni Adamu. Basi wakamsujudia isipokuwa Ibilisi yeye alikuwa miongoni mwa majini na akavunja amri ya mola wake……..”
Katika aya hiyo tunaona ibilisi akilaumiwa kwa kutomsujudia Adamu ingawa amri ya kusujudu walipewa malaika kumbe kwa mujibu wa Quran Ibilisi alikuwa miongoni mwao hao malaika yaani na yeye akiwa malaika.
Kwa sababu Quran haina habari kuhusu malaika walioasi yaani majini ndiyo maana wanapata tabu kuhusu jambo hilo. Na ndiyo maana pamoja na kujua kuwa hayo majini ni mashetani, Muilsamu amehiari kushirikiana nayo kwa kuswali nayo msikitini. Na hata mwislamu huyu anapomaliza kusali husalimia kulia na kushoto akiwasalimia watu malaika na majini (mashetani) waliokuja kushiriki naye katika Ibada yake, soma katika (Irshadul Muslimiin, Sheikh Said Musa, Uk. 38).
Katika Tafsiri ya Quran ya Iman Jalalaini Uk. 6:151 anasema kuhusu majini “ Hao ni watoto wa Ibilisi”
Hii ndiyo sababu hata wanawake wa Kiislamu wakiwa katika kipindi cha hedhi hawaendi msikitini kwa sababu kuna majini na chakula cha majini ni damu. Tafakari kwa hiyo sifa ya hayo majini au mashetani kwa ujumla ni kuwa “ hujaribu kwa bidii sana kuwa karibu na waamini wale wanaosali, kufunga na kusoma Qurani “ (Asili ya majini, Dk. Ahmed H. Sakr Uk. 28) ndiyo maana baadhi ya waislam wao binafsi wasingependa kuwa waislamu lakini majini huwashurutisha kwenda kuswali.
Kwa sababu wao waislamu hawajui kupambanua kati ya majini ambayo ni roho chafu na wale malaika watakatifu wa Mungu Jehova, ndiyo maana hata akiwa katika sala yake hana uhakika kwa sababu huyo jinni (shetani) amemteka na anamfanyia atakavyo na yeye ni mtumwa wa huyo jinni (shetani)
Katika kitabu kiitwacho Mkweli Mwaminifu cha Sheikh Said Moosa Mohamed Al- Kindy wa Muscut Oman, juzuu 1-2 Uk 42 Hadithi Na. 74.
“ Anamwijia mmoja wenu shetani (Jini) katika sala basi anapuliza (anampuliza) katika matako yake, basi (yule mtu) inamuijia fikra ya kuwa umemtoka upepo (kafusa) naye haukumtoka, basi akiona namna hiyo asiondoke (kwenye sala}) mpaka asikie sauti ( ya kutoka upepo) au anuse harufu ( ya huo upepo uliyomtoka, ndio aondoke).
Huyo shetani, au jinni anayekuwa karibu sana na huyu mwamini wa kiislamu hamchezei tu mwislamu katika matako yake kama tulivyosoma hapo juu bali pia anapofanya tendo la ndoa .
Katika kitabu kiitwacho Asili ya Majini, cha Sheikh Dr Ahmad H. Sakr Uk. 116 anasema “ Hadithi ya Mtume inathibitisha jambo hili kuwa majini (mashetani) na watu wanaweza kuoana aliposema kwamba iwapo mtu ataingia katika uhusiano wa kindoa na mkewe anatakiwa ataje jina la Mwenyezi Mungu ajilinde kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya shetani aliyefukuzwa mbali na rehema. Vinginevyo shetani hujiviringisha katika dhakari (sehemu ya siri za mwanaume) ya mtu huyo na atashirikiana naye katika tendo hilo. Tafakari yetu kuwa hiyo jinni anayeshiriki naye tendo la ndoa pamoja naye kwa mkewe ametumwa na huyo huyo Mungu wao. Hiyo ni kesi ya ngedere kumpelekea nyani! Utashindwa tu!
• Huhakikisha haweki wazi utambulisho wake vinginevyo watu wanaweza kumkwepa au hata kukimbia. Jina lake linawatisha watu wengi. Hivyo ni vyema asijitambulishe kama ni shetani , jini.
• Huwapotosha watu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili waende naye Jehanamu, badala ya kwenda peke yake. (Kumbuka hukumu ya Yesu kwa Ibilisi na Malaika zake (Math 25:41)
• Huwakatisha watu tamaa kwa sababu hana cha kuwapa ila matumaini ya uongo (Mf Q. 52:20)
• Huhakikisha kwamba watu wanamheshimu kumfuata shetani maana yake ni kuwa mtu wa namna hiyo amejisalimisha (Kumbuka waislamu wanapowasalimia majini kulia na kushoto katika sala (Irshadul Muslimin Uk 38).
• Huhakikisha kuwa hadhihirishi jina lake kama shetani lakini kama rafiki aliyejificha anayewatakiwa mema.
• Huanzisha vurugu vinginevyo maisha yake huwa ya taabu. Huwa anafurahia kuona watu wakipigan wao kwa wao.

Katika kipengele hiki tunaposoma katika Quran, Suratul – Al- Maidah, (Meza) 5:14.
“ Na kwa wale waliosema sisi ni Wakristo tulichukua ahadi kwao, lakini wakaacha sehemu (kubwa) ya yale waliyokumbushwa kwa hivyo tukaweka baina yao (wenyewe kwa wenyewe) uadui na bughudha mpaka siku ya kiama na mwenyezi Mungu atawaambia waliyokuwa wakiyafanya”
allah S.W. ndiye anayewaletea uadui na bughudha wakristo. Yeye atakuwa nani?
Tafakari.

• Hufundisha uchawi watu wanapaswa watoe kiapo cha utii kwake kabla ya kufundisha uchawi wa aina yoyote. Elimu ya uchawi ni kuwadhuru watu wengine hasa hasa waume na wake.
Katika sehemu hii tumwangalie huyo shetani au jinni anayeruhusu na kufundisha uchawi.
Katika Suratul, al- Bagarah, (ng’ombe jike), 2:102 “ Wakafuata yale waliyoyafuata mashetani wakadai kuwa yalikuwa katika ufalme wa nabii suleimani na Suleiman hakukufuru bali mashetani ndiyo waliokufuru, wakiwa fundisha watu uchawi waliokuwa wakiujua wenyewe tangu zamani. Na uchawi uliteremshwa kwa malaika wawili Haruta na Maaruta katika mji wa Babeli wala malaika hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie hakika sisi ni mtihani wa kutazamwa kutii kwenu basi usikufuru wakajifunza kwao ambayo waliweza kumfarakisha mtu na mkewe na mengineyo wala hawakuwa wenye kumdhuru yeyote kwa hayo ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu……………………
Katika aya hiyo inaeleza kuwa uchawi ni kazi ya Allah na ndiye anaye idhinisha. Yeye atakuwa nani? Na pia kuna waganga wa kienyeji wa kiislamu ambao hutumia Quran katika uganga wao. Hiyo Quran na majini na uchawi, ulioletwa na Allah S.W. vina uhusiano gani? Tafakari
“ Juhudi kubwa anayoifanya shetani (Jini) ni kuleta mfarakano baina ya waume na wake. Kwa kufanya hivyo huhakikisha kuwa wanachukiana wao kwa wao. Kwa ajili hiyo huishia, katika talaka. Kwa hiyo matatizo yanajengwa katika familia hiyo. Utengano au talaka inapotokea, watoto hawawezi kulelewa kisawasawa na mzazi mmoja. Watakosa uimara katika utu wao, shetani (jinni) anapata urahisi kuingia ndani ya mioyo na akili za watoto. Atawaongoza kuelekea mahali pasipofaa na hapo anawafanya wawe wahalifu katika jamii (Asili ya majini, sheikh Dr. Ahmad H. Sakr Uk 39)
Kwa mujibu wa Quran na vitabu vya kiislam huyo anayeamuru talka ni allah. S.W. Mungu wanayemuabudu waislamu.
Katika suratul, Ahzab(Makundi), 33:49.
“ enyi mulioamini mtakapowaona wanawake wenye kuamini, kisha mkawapa talaka kabla ya kuwagusa hamna eda juu yao mtakayohesabu. Wapeni cha kuwauliza na muachane muachano mzuri”

Katika Suratul al- Baqarah, (Ng’ombe) 2:230.
“ Na kama amempa talaka ya tatu basi mwanamke huyo si halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwingine, na mwanamume huyo mwingine akimwacha basi hapo hapana dhambi kwao mume yule wa kwanza na mwanamke huyo kurejeana wakiona watasimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu.”

Kama shetani (jinni) huleta faraka ili talaka zitokee, basi Allah S.W. yeye ameamrisha talaka kwa wafuasi wake bila kujali athari za watoto zitakazotokea. Tafakari yeye ni nani?
Kumuabudu shetani (Jini)
Katika Suratul Sabaa, 34:40-41
“ Na kumbuka siku atakayowakusanya wote, kisha atawaambia malaika, “ Je hawa walikuwa wakikuabuduni?” waseme umeepukana na kila upungufu! Wewe ndiwe kipenzi chetu si hao bali walikuwa wakiwaabudu MAJINI; wengi wao waliwaamini hao majini”

“ Shetani anapoamuru watu wamfuate pia anawaamuru wafanye madhambi na wakose maadili. Huwataka waseme uongo kuhusu Mwenyezi Mungu kutokana na kutokujua kwao. Wanaweza kusema kuwa sisi wanaadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu. Mungu alijifanyisha na kuwa umbile la kibinadamu. Mungu amezaa, na mwanaye niwa pekee. Zaidi ya hayo mwanaye si mtoto tu bali ni Mungu pia. Huyo mwana ni Bwana Yesu. Asiyeamini hivyo huchukulika kuwa ni kafiri au muasi hivyo ameangamia na atakwenda jehanamu” (Asili ya Majini, Sheikh Dr. Ahmad H. Sakr Uk 54)



MUNGU akubariki sana.
Anuani yangu ni;

 HUDUMA YA UINJILISTI YA BIBLIA NI JIBU
 S.L.P 45102
 DAR ES SALAAM, TANZANIA.
+255 755 680101
 Email: dmwankemwa@gmail.com

Comments